Rais Samia: Wamesahau Misukosuko Waliyoipata Hapo Nyuma Mpaka wakaikimbia Nchi na Mimi Kuwarejesha kwa 4R Zangu

Lissu aliwaonya mapema sana kwamba msimshangilie huyu mama anaweza kuwa katili kuliko hata Jiwe.

Naona sasa watu wameona picha halisi. Maandamanonya 23rd ndiyo yatatoa hatma ya nini kitafuata.
Lissu kama amechoka na kulewa amani ya Nchi hii aondoke haraka sana hapa Nchini.
 
Nilipoona tu samiamustgo nikabubujikwa na huzuni maana tafsiri yake inafahamika.
 
Uwe na adabu na uache mara moja uropokaji wako.
Lissu kamtukana vipi Mama yako???
Kwani kuambiwa anazuza mali za Tanganyika ni matusi ?

Usiwe na wewe ni Kipofu kwa sababu ya Mapenzi yako kwa Mama Samia. Sote tunampenda na kumheshimu lakini Wewe imezidisha mahaba ya kinafiki hivi kuna binadamu asiyekosea? Ifikie wakati usimtukuze na kumwabudu mtu as if yeye amekamilika kwa kila kitu.
 
Misukosuko Gani waliyoipata?kipindi chake Cha awamu ya sita ndiyo Kuna misukosuko mingi haijawahi kutokea toka Nchi upate uhuru.watu wanatekwa Kila kukicha.TLS walitoa orodha ya waliotekwa kipindi chake wanafika zaidi ya miambili
 
Sativa kamtambua Mafwele Faustine kafanywa nini huyo Mwafwele??
Kwanini unaufanya ubongo wako kuwa kama sponji???🤣🤣🤣
Mambo yakienda vibaya lazima mkuu wa nchi watu wampigie kelele. Hata wewe nyumbani kwako ikitokea shida Watoto au mkeo watakulilia. Mauaji yanayotokea na kupotea kwa Wananchi hivi wewe hili jambo unalichukuliaje?
 
Angalau leo tumejua kwanini watekaji wapo juu ya sheria....
 
Hii nchi sio mali yake, na hakuna mtanzania anaishi hapa kwa hisani yake labda nyie chawa wake. Hao akina Lisu walikimbia kulinda uhai wao chini ya utawala wa dhalimu Magufuli. Na hawakukimbia kama wahalifu, bali mahasimu wa kisiasa wa utawala wa kidhalimu wa Magufuli.

Wamerudi baada ya Magufuli kufariki, na yeye alitumia urejeo wao kihudaa umma kuwa ana roho nzuri. Yeye ndio alifaidika na ujio wao kwani alijichukiulia marks kuwa ni rais mpenda demokarasia. Hapa wamerudi kwenye nchi yao, sio kwenye nchi ya rais Samia kama mali binafsi. Asitegemee na yeye akifanya kama dhalimu Magufuli ,basi hao waliorejea nchini watapaswa kukaa kimya kisa wamerudi akiwa rais yeye.
 
Angalau leo tumejua kwanini watekaji wapo juu ya sheria....
 
Kwa hotuba ya leo ya Samia ni ushahidi huu utekaji na mauji yana mkono wake.
Mkono upi? Tena kama wewe usiongee kitu kabisa.maana wewe ni mropokaji sana na mwenye nia ovu na Taifa letu
 
Wewe upstairs uwezo mdogo sana na akili hauna...leo nimejua tunaongozwa na mtu mwenye uwezo mdogo wa akili ambae hajitambui,diploma ya maarifa ua jamii ndio iongoze akili kubwa uliona wapi
 
Kumtambua bila ushahidi inawezekana vipi ukamuamini mtu wa aina hiyo?
 
Familia yake ni watanzania na ndio maana anahangaika usiku na mchana kutuhangaikia.ili kila mtanzania apate huduma bora na karibu yake kabisa .lakini pia ili kuhakikisha kuwa kila mtanzania anapata milo mitatu iliyo bora na kwa wakati.
Shukuru, kama anaihangaikia familia yako. Lakini familia ya Ally, Soka, and et al, hawatausahau utawala huu uliowatenganisha na wapendwa wao. Ukiwa na Roho wa Mungu, hivi hata Mwashambwa ukiniambia sina akili, ninakuwa nimepungukiwa na nini, hata nione kwa sababu umenitamkia hayo nisiyoyataka, basi uuawe?

Hakika nasema, kiongozi yeyote ambaye utawala wake unaua, hana upendo wala uzuri wowote kwa mtu yeyote, wala Taifa, huyo ni mtumishi wa shetani anayelenga kuliharibu Taifa. Tunaomba Mungu awajalie hekima wananchi, hekima ya kuuvaa ujasiri, ili hekima ya Mungu, kwa kupitia watu wake, atuletee mtawala atakayeusimamisha ushetani unaoendelea sasa nchini mwetu. Tuvipokee kwa moyo wa subira na imani vifo vya jamaa zetu tusivyo na uwezo wa kuvizuia, lakini tukatae kazi ya shetani kupitia mamlaka za serikali zinazoondoa uhai wa binadamu wenzetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…