Rais Samia: Wanaopinga mabahewa ni watoto waliozaliwa mwaka 1990

Vijana mnapoambiwa mshiriki shughuli za kisiasa kwa nguvu zenu zote Kama kupiga kura za kuwachagua mnaowaamini au kuchaguliwa mnabeza na kuleta dharau eti Nani akakae foleni au Nani akakimbizane na polisi kulinda kura yake isihesabiwe asikokuchagua!
Oneni Sasa mnavyobagazwa na wazee eti hamruhusiwi Kijiji vile vibovu mnavyoletewa!
Mnajua hiyo mitambo ya tetenasi mmeletewa ninyi vijana na watoto wenu? Hawa wazee hawatayatumia mabehewa hayo Bali watapanda ndege ambazo gharama zake hamzimudu na hayo mav8 brand new ambayo ninyi hamtakuja kuwa nayo!
Shirikini chaguzi na shughuli zote za siasa ambazo ndizo zinazoamua uishije leo na kesho!
 
hakuna kitu kizuri na kinachorahisisha maisha kama ukweli, kwani haujitaji nguvu nyingi kuutetetea, na wala huwezi kujichanganya hata siku moja kama ukiwa mkweli
Umemaliza mkuu, πŸ“Œ
 
Kwahiyo Marekani ilivyokuwa na miaka 60 ilikuwa kama sisi? Huyo mama anashindwa kujua kwamba serikali ina sheria ya manunuzi inayotaka ununuzi wa vitu vipya. Na hata kama ni mitumba, mbona bei yake inazidi ya mabehewa mapya? Hapo sio suala la kuzaliwa lini, bali ni uhalisia wa bei.
 
Hivyo ndivyo watu wasumbufu hujibu hoja, hujibu kwa kuwagawa ili abaki na kundi moja la kuwaburuza.
Watoto vs Watu wazima na wazee
Waha vs makabila mengine.

Alitakiwa ajibu kwa nini serikali imeyanunua hayo machumachuma.
Anakimbilia kebehi na dhihaka.
 
Hivi utaratibu wa kuandaa hotuba kwa viongozi wanapotembelea maeneo mbali mbali bado upo?
 
Pale umri wa mtu unapotaka kutumia kubadiri used mabehewa yawe mapya..!!
 
Ila kusema kweli kuna mambo yanachekesha sana.
Mbona yeye bi tozo kuna mambo anatufananisha na marekani, uk, nk...
Utamsikia "wenzeti marekani..."

Dunia ni kama kijiji, watanzania wanataka vitu vizuri. Wanaviona kwenye tv na mitandaoni!
 
Mimi nimezaliwa miaka ya 2000s na bado naendelea kupinga hadi kesho
Kwani hao waliozaliwa before 1990 ndio wana IQ kubwa ama vipi
Hata akipinga mtoto wa 2015, haijalishi ukweli ni kwamba tumepigwa, tena na kitu kizito sana
 
Hao Vijana anaosema Mhe. Rais wa Mwaka 1990 akumbuke ndiyo watakaolipa hilo deni, kwahiyo ni haki yao kuhoji.

Mhe. Kigwangala endelea kuwahimiza Vijana wenzako wa 1990 kuendelea kuhoji Kila Fedha ya Serikali inayokopwa na Serikali hii ili zitumike vizuri kwa maana wao ndiyo watakaolipa Madeni hayo kupitia Kodi zao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…