Rais Samia: Wanaopinga mabahewa ni watoto waliozaliwa mwaka 1990

Rais Samia: Wanaopinga mabahewa ni watoto waliozaliwa mwaka 1990

sisi kama taifa tunajua tumefiwa na baba tuliyemkabidhi nchi yetu, hawa wapokeaji wa mizigo njiani hawajui umuhimu hali zetu tuwasamehe bure. Magari yote ya serikali yangenunuliwa "used" ingependeza sana. kila kitu tutumie used sasa maana imekuwa ni sifa. Alafu waliohoji walisema "used " sio shida tatizo lipo pale kwenye bei tuliyonunuliwa...hapo tumeibiwa. Tunatafuta mwizi wetu, je ni wale waliotuuzia? je ni wahuni walioko serikalini wametupiga changa la macho?..hapa ndio tuna hoja napo sisi kizazi cha 90 😕
 
"Wale wanaopenda tu kufujafuja kila kitu, wafuje lakini warudi nyuma lakini ukute mfujaji mwenyewe kazaliwa miaka ya 90 hajui tulikotoka, anafananisha na Marekani anakokuona na anataka Tanzania ifike kule bila kujua anaojifananisha nao wana miaka 200 ya maendeleo,"- @SuluhuSamia


Tunachojua..Kijana aliyezaliwa mwaka 1990 ambapo sasa hana miaka 32 wengi wa hili kundi wanakabiliwa na tatizo la ukosefu wa ajira,uchumi usioimarika,kukosa kazi rasmi na sio wao pekee wakubeza mambo ambayo kwa upande wa Serikali hayaendi sawa,
Kijana aliyezaliwa mwaka 1990 ambapo sasa hana miaka 32 wengi wa hili kundi wanakabiliwa na tatizo la ukosefu wa ajira,uchumi usioimarika,kukosa kazi rasmi na sio wao pekee wakubeza mambo ambayo kwa upande wa Serikali hayaendi sawa,[emoji818][emoji817]
 
Waliozaliwa 1990 ni watoto??!

Pia nashangaa katika hili.

Kama ni watoto inakuwaje katika Serikali ameajiri watoto?. Kwa maana kuna viongozi wengi wa ngazi tofauti kama Wakuu wa wilaya, Wakurugenzi na n.k ambao ni wa mwaka 1990.
 
Mama Samia amepotea na amepotosha. Hoja halisi ni hizi hapa na alipaswa kuzijibu.

1. Tulikubaliana na tukaahidiwa tunaletewa treni mpya (vichwa vipya na mabehewa mapya), sasa nini kimetokea mpaka tukaletewa mtumba?

2. Mabehewa yalipowasili tukaambiwa ni mapya, tulipochunguza tukagundua ni mtumba. Kwanini serikali inatudanganya?

3. Tuliambiwa (na picha tukaonyeshwa) tunaletewa treni mpya za kisasa. Sasa kwanini tuletewe treni ya zamani mnoo, tena mtumba?

4. Tulijipanga, tukatenga bajeti ya kununua treni mpya ya kisasa. Kwanini leo pesa zetu ziende kununua treni ya kizamani tena mtumba, kwa gharama ya kununulia treni mpya na kisasa?
 
Wabongo tumezidi ulalamishi. Kila kitu hakifai. Tupe ukweli mama.
 
Watendaji wa serikali wanamdanganya rais, na wayasemayo wananchi anaona wanaubeza serikali. Pamoja na hilo la mabehewa, swala la umeme unaelezwa mgao haupo lakini ukweli ni kinyume chake. Mikoani ni giza na miungurumo ya magenerator maeneo kadhaa. Ukizidi kuwabeba na uongo wao, wananchi watakuweka kundi moja nao.
 
Na hilo ndo kundi la wapiga kura sasa.
Lisipoelewa linatakiwa kueleweshwa siyo maneno ya kwenye kanga.

Kwenye matangazo ya Reli na matukio ya TRC mnatumia demo ya bullet train halafu mnaleta "Ngalangala" kisha hamtaki watu waongee.
 
Kauli kama hizi zinatia aibu sana, kwamba vijana wa 1990 sio wananchi na hawana haki ya kuhoji serikali

Kumbuka hao wa 1990 pia ni wapiga kura
 
Ivi serikali haiwezi kufanya tu miradi yake pasipo kutaja taja gharama
Kama ni reli iseme tu sasa tunajenga reli mwaka ujao tunanunua treni
 
"Wale wanaopenda tu kufujafuja kila kitu, wafuje lakini warudi nyuma, ukute mfujaji mwenyewe kazaliwa miaka ya 90 hajui tulikotoka, anafananisha na Marekani anakokuona na anataka Tanzania ifike kule bila kujua anaojifananisha nao wana miaka 200 ya maendeleo”

Rais Samia.
Screenshot_20221221-083135_Facebook.jpg
 
Huku ni kukwepa kuwajibika.Na vilevile,ni changamoto ya kutojua uliposimama na athari za ulimi wa muongeaji kwenda kwenye masikio ya msikilizaji.Mengine siyo lazima sana tuyajibu.Wanawanchi wana hasira na kero zao.Ukiwakoroga kidogo tu,ugomvi!Si ugomvi wa kutwangana makonde.Unaweza kuwa hata ugomvi wa kutazamana kwa macho "mema"!
 
Back
Top Bottom