Rais Samia: Watu 13 wamefariki kwenye jengo lililoporomoka Kariakoo. Serikali kugharamia matibabu ya majeruhi na kuhakikisha waliofariki wanasitiriwa

Rais Samia: Watu 13 wamefariki kwenye jengo lililoporomoka Kariakoo. Serikali kugharamia matibabu ya majeruhi na kuhakikisha waliofariki wanasitiriwa

Tumepoteza watanzania wengi.
Tunalia
Wafiwa hawafarijiki
Vilio vimeenea kila upande.
Tafarijiane wenyewe kwa wenyewe.
Mungu awafariji.
Poleni sana.
 
Je, hakuna hatua za kisheria na kinidhamu? Ni kina nani waliohusika na usimamizi na uthibitishaji wa kazi iliyokuwa ikiendelea?
Holela Holela itatucosti sana ! 😳
Tuache hii mambo ya Business as usual !
Mnaokabidhiwa kazi mufanye kazi kweli kweli !
Acheni hii mambo ya Holela Holela 😱🤦🏽‍♂
 
Hizo tume hazina maana wanakula pesa bureeee hakuna watafanya...
Wenye kajengo ni makada na wanaogopa kuharibu mzunguko pesa kkoo...
 
Mama unatoa bilioni 100 kwa polisi kununua washawasha za uchaguzi na unatoka milioni 300 mpaka 400 kununua magari ya wakurugenzi wa wilaya wanao engua wagombea. Lakini huwezi kutoa pesa za kununua vifaa vya uokoaji. Hakuna mtu anafukuzwa TZ hata watu wakifa siku hizi. Ripoti unazoomba ni fake kila siku unaomba ripoti fake ambazo hazitoki na hazitatoka. Mnajali chama, ndugu zenu na marafiki . Wananchi mnawajali ili tu wawaweseshe kuendelea kuiba na kujinufaisha nyie na ndugu zenu. Wananchi wamekuwa mbumbumbu hawawezi hata kulalamika tena kama vile wafanyakazi wenu na sio nyie wafanyakazi wao. Hii nchi ni Mungu tu ndiyo anaeeza kuiokoa kwasasa na tukiweka imani atafanya hivyo
😳🙄😱 !
 
Katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025, ni muhimu kufikiri kwa makini kuhusu uongozi wetu na jinsi unavyoshughulikia masuala ya msingi yanayoathiri maisha ya wananchi. Ni jambo la kushangaza na kukatisha tamaa kuona Rais wetu akielekea kwenye mikutano ya kimataifa, wakati nyumbani kuna maafa makubwa yanayohitaji uongozi wake wa karibu. Kutojishughulisha na masuala haya ni uthibitisho wa kutokujali hisia na mahitaji ya watu waliomchagua.

Kama ilivyo kawaida katika nchi nyingi, viongozi wanapokumbana na matatizo makubwa, kama vifo vya raia zaidi ya 13, inatarajiwa kuwa watachukua hatua za haraka na kuonyesha mshikamano na jamii. Lakini badala yake, tunaona Rais akifanya mipango ya safari ambazo hazina umuhimu wa dharura. Ni kweli kwamba wakati mwingine wanaweza kukabiliwa na majukumu mengine, lakini je, kweli kuna jambo lolote muhimu zaidi kuliko maisha ya watu? Hii ni dhahiri ya kutojua na kukosa uelewa wa hali halisi ya wananchi.

Kila kifo ni hadithi ya maisha, na kila mmoja wa waliokufa alikuwa na familia, marafiki, na jamii ambayo inakabiliwa na maumivu na huzuni. Hivyo, ni jukumu la Rais kuonyesha uongozi wa kweli, kutojificha nyuma ya kisingizio cha majukumu mengine. Kuwa muungwana hakumaanishi tu kusema maneno ya faraja; inahitaji vitendo vinavyothibitisha kwamba unajali na unaguswa na hali halisi ya raia.

Wakati tunaposema "huyu ni mtu wa watu," tunatarajia kuona mabadiliko katika matendo yake, na sio maneno matupu. Ni rahisi kwa viongozi kusema wanaweza kuja kwa wananchi wakati wa kampeni, lakini je, wanajali kweli? Tunaona kwamba wengi wao wanatumia lugha nzuri ili kupata kura, lakini wanaposhika madaraka, wanajitenga na matatizo ya wananchi. Tunashuhudia viongozi wakifanya ahadi ambazo hazitekelezwi, na hatimaye wanarudi kwa raia wakati wa kampeni nyingine, wakitumia maneno kama "mama atosha" kama kivuli cha ukweli wa hali halisi.

Ni muhimu pia kutambua kwamba Rais anapaswa kuwa na washauri wazuri, lakini ni wazi kwamba katika baadhi ya matukio, amekosa ushauri mzuri. Kuwa na washauri wazuri ni muhimu, lakini pia ni jukumu lake mwenyewe kutafakari na kuona ni nini kinachotokea katika jamii. Kufanyika kwa maafa, kama vile vifo vya watu 13, ni dalili tosha ya kwamba kuna haja ya maamuzi ya haraka na ya busara. Kutangaza maombolezo ya kitaifa si tu ni ishara ya kuheshimu waliokufa, bali pia ni njia ya kuonyesha kwamba serikali inajali na inatambua maumivu ya raia wake.

Kwa hivyo, tunahitaji kujiuliza: Je, Rais huyu anatoshea kuendelea kuwa kiongozi wetu? Je, tunahitaji mtu ambaye anaweza kujiweka mbali na matatizo ya raia? Tunahitaji kiongozi ambaye anaweza kuungana na wananchi, ambaye anajali na kuonyesha uongozi wa kweli katika nyakati za shida. Wakati wa uchaguzi wa 2025, ni muhimu kwa wapiga kura kufikiri kwa makini na kufanya maamuzi ambayo yataweza kubadilisha hali hii ya uongozi.

Kwa kumalizia, ni wazi kwamba ni wakati wa kutafakari maisha na vipaumbele vyetu kama taifa. Tunahitaji kiongozi ambaye atajali hisia za wananchi, ambaye atajitolea kwa watu na ambaye ataonyesha uongozi kwa vitendo, si maneno tu. Hii ni nafasi yetu ya kuamua mustakabali wa taifa letu, na ni muhimu kuhakikisha kwamba tunachagua viongozi wanaoleta mabadiliko ya kweli na endelevu.
 
Taarifa inasomwa ikitokea wapi wangu!!
Hili ni tatizo kubwa !
Vifaa vya uokozi, 🤣🤣🤣🤣🤣.
Hapa hakuna Rai..
hapo ni dar karibu na ikulu, je ikitokea huku Mwanza,Arusha,Mbeya, 😳
 
Attachments

  • 5880760-c61cb7caa9e2ca2ff375b1dbd0b70979.mp4
    5.7 MB
Jitahidi kuficha upuuzi wako na hao ccm wenzako.Unatuonyesha picha na taarifa kuwa hao ccm walienda eneo la tukio,kisha wamekaa na kupiga picha ya pamoja,hebu tuambie uwepo wao ulikuwa na tija gani kwenye zoezi la uokoaji?
Kipindi mz.Lowasa alipokuwa Waziri Mkuu,jengo la chang'ombe village [keko]lilianguka,Mz.Lowasa alisimamia zoezi la uokoaji pamoja na wahusika wa hilo jengo kuwajibishwa, tofauti na hawa jamaa zako walienda kupiga picha ya pamoja ili tuone kuwa walikuwepo hapo,,Hivi hamna aibu hata kidogo?Tuondoleeni upumbavu wenu.
Tatizo una akili ndogo ya kuelewa ujumbe.

Najaribu kukwambia hao walioenda hapo wakati hawana Msaada ni sawa na wewe kudai Samia akatishe ziara ambako anaweza kufanya mambo mengi ya uwezo wake kama mtawala arudi Nchini kuja Kukaa na kuongea kama wewe na hao wa kwenye picha.

Mwisho usiwe mpumbavu,Samia akisafiri Urais wake haujasafiri pia,Bado anaendelea na jukumu lake la kuhimiza na kusaidia Uokoaji Kwa uwezeshajo.

Wewe badala ya kuokoa uko jf unaweza, pumbavu zako
 
Kwa Sasa tuwe na tahadhari kubwa tukienda kariakoo.Majengo mengi yanajengwa mapya kiholela pasipokuzingatia usalama na serikali haichukui hatua yeyote.Hivi vifo vilivyotokea havikustahili kabisa kama serikali ingekuwa inatimiza wajibu wake katika ujenzi.
 
Rais Samia ambaye amesafiri kwenda Jijini Rio de Janeiro nchini Brazil 16 Novemba, 2024 kwa mwaliko wa Rais wa Brazil, Luiz Inácio Lula da Silva kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa nchi Wanachama wa Kundi la G20, amezungumza na Wananchi kufuatia kuporomoka kwa ghorofa Kariakoo Jijini Dar es Salaam.

Rais Samia amesema “Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kuporomoka kwa ghorofa katika eneo la Kariakoo Jijini Dar es Salaam. Nimekuwa nikipata taarifa za mara kwa mara kuhusu zoezi la uokoaji kutoka kwa Waziri Mkuu na nimekuwa nikifuatilia zoezi hilo kwa karibu zaidi.”

Pia soma: Live Updates Kuporomoka kwa Ghorofa Kariakoo Nov 16: Watu 7 wengine waokolewa

Amesema “Hadi saa nne asubuhi leo, jumla ya watu 84 wameokolewa na kufikishwa hospitalini kwa ajili ya kupatiwa matibabu. Kati ya hao majeruhi 26 bado wanaendelea na matibabu. Pamoja na hao kwa huzuni kubwa tumepoteza wenzetu 13 katika tukio hilo.”

Aidha ameongeza kuwa “Serikali itabeba gharama za matibabu kwa wote waliojeruhiwa, na kuhakikisha waliofariki wanastiriwa ipasavyo. Nitoe pole kwa ndugu, jamaa na marafiki walioguswa na tukio hili. Niwaombe watanzania wote tuwaweke kwenye maombi wote walioathirika na tukio hili na kuwaweka kwenye maombi waliotangulia mbele za haki.”

Salamu za Pole za Awali za Rais Samia: Rais Samia atoa pole kwa waathirika Kariakoo. Aagiza kufanywa kila linalowezekana kufanikisha zoezi la uokoaji na tiba kwa majeruhi

“Serikali itaendelea kutoa taarifa zaido kuhusu zoezi la uokoaji hadi hapo zoezi hilo litakapokamilika. Hadi sasa sababu za kitaalamu za jengo hilo kuporomoka bado hazijachunguzwa na kubainishwa, kwani kipaumbele chetu kwanza ni kuwaokoa wenzetu waliokuwa ndani ya jengo hilo.”

“Nashukuru mashirika binafsi na wananchi wote waliojitolea na waliotoa ushirikiano katika zoezi hilo. Nashukuru pia Madaktari wanaoendelea kuhudumia majeruhi. Nampongeza Waziri Mkuu, Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam na timu zao kwa kusimamia kazi kubwa ya uokozi.”

“Baada ya uokozi kukamilia, namtaka Waziri mkuu kuongoza timu ya Wakaguzi majengo, kukagua majengo yote ya eneo la Kariakoo na tupate taarifa kamili ya hali ya majengo ya Kariakoo yalivyo.”

Soma taarifa ya mwaka 2013: Magorofa 64 hatarini kuanguka Kariakoo

Aidha, Rais Samia ameagiza Jeshi la Polisi kupata taarifa kamili kutoka kwa Mmiliki wa Jengo lililoporomoka, kuhusu ujenzi ulivyokuwa unafanyika. Aidha, amesema taarifa zote za uchunguzi zitakapopatikana zitawekwa wazi kwa wananchi wote
Tukubaliane tu kwa pamoja hii nchi kwa sasa inajiendea tu yenyewe kama gari bovu lisilo na dereva
 
Hivi ile sera ya maafa ndio inaelekeza hivyo?
 
Back
Top Bottom