Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Holela Holela itatucosti sana ! 😳Je, hakuna hatua za kisheria na kinidhamu? Ni kina nani waliohusika na usimamizi na uthibitishaji wa kazi iliyokuwa ikiendelea?
Taarifa zisizostaajabisha ni zipi ?!Yaani Nastaajabika sana kusikia hizi taarifa za zisizo na ukweli juu ya watu walio kufa.
Duh 🙄 !Huku ni machakani
😳🙄😱 !Mama unatoa bilioni 100 kwa polisi kununua washawasha za uchaguzi na unatoka milioni 300 mpaka 400 kununua magari ya wakurugenzi wa wilaya wanao engua wagombea. Lakini huwezi kutoa pesa za kununua vifaa vya uokoaji. Hakuna mtu anafukuzwa TZ hata watu wakifa siku hizi. Ripoti unazoomba ni fake kila siku unaomba ripoti fake ambazo hazitoki na hazitatoka. Mnajali chama, ndugu zenu na marafiki . Wananchi mnawajali ili tu wawaweseshe kuendelea kuiba na kujinufaisha nyie na ndugu zenu. Wananchi wamekuwa mbumbumbu hawawezi hata kulalamika tena kama vile wafanyakazi wenu na sio nyie wafanyakazi wao. Hii nchi ni Mungu tu ndiyo anaeeza kuiokoa kwasasa na tukiweka imani atafanya hivyo
Hawana vifaa vya uokoaji. Tuna nunua ma V8 ndio kipau mbele.Timu ya waokoaji yapasa kujieleza sio sili wamechelewa sana kwa uokozi
MxiuuuuuuuuuuuuuKiongozi mwenye upendo wa kweli
Vifaa vya uokozi, 🤣🤣🤣🤣🤣.Taarifa inasomwa ikitokea wapi wangu!!
Hili ni tatizo kubwa !
Acha uongo,Alisafiri kabla ya maafa kutokes
Tatizo una akili ndogo ya kuelewa ujumbe.Jitahidi kuficha upuuzi wako na hao ccm wenzako.Unatuonyesha picha na taarifa kuwa hao ccm walienda eneo la tukio,kisha wamekaa na kupiga picha ya pamoja,hebu tuambie uwepo wao ulikuwa na tija gani kwenye zoezi la uokoaji?
Kipindi mz.Lowasa alipokuwa Waziri Mkuu,jengo la chang'ombe village [keko]lilianguka,Mz.Lowasa alisimamia zoezi la uokoaji pamoja na wahusika wa hilo jengo kuwajibishwa, tofauti na hawa jamaa zako walienda kupiga picha ya pamoja ili tuone kuwa walikuwepo hapo,,Hivi hamna aibu hata kidogo?Tuondoleeni upumbavu wenu.
Live from BrazilKwani uko wapi mama
Tukubaliane tu kwa pamoja hii nchi kwa sasa inajiendea tu yenyewe kama gari bovu lisilo na derevaRais Samia ambaye amesafiri kwenda Jijini Rio de Janeiro nchini Brazil 16 Novemba, 2024 kwa mwaliko wa Rais wa Brazil, Luiz Inácio Lula da Silva kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa nchi Wanachama wa Kundi la G20, amezungumza na Wananchi kufuatia kuporomoka kwa ghorofa Kariakoo Jijini Dar es Salaam.
Rais Samia amesema “Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kuporomoka kwa ghorofa katika eneo la Kariakoo Jijini Dar es Salaam. Nimekuwa nikipata taarifa za mara kwa mara kuhusu zoezi la uokoaji kutoka kwa Waziri Mkuu na nimekuwa nikifuatilia zoezi hilo kwa karibu zaidi.”
Pia soma: Live Updates Kuporomoka kwa Ghorofa Kariakoo Nov 16: Watu 7 wengine waokolewa
Amesema “Hadi saa nne asubuhi leo, jumla ya watu 84 wameokolewa na kufikishwa hospitalini kwa ajili ya kupatiwa matibabu. Kati ya hao majeruhi 26 bado wanaendelea na matibabu. Pamoja na hao kwa huzuni kubwa tumepoteza wenzetu 13 katika tukio hilo.”
Aidha ameongeza kuwa “Serikali itabeba gharama za matibabu kwa wote waliojeruhiwa, na kuhakikisha waliofariki wanastiriwa ipasavyo. Nitoe pole kwa ndugu, jamaa na marafiki walioguswa na tukio hili. Niwaombe watanzania wote tuwaweke kwenye maombi wote walioathirika na tukio hili na kuwaweka kwenye maombi waliotangulia mbele za haki.”
Salamu za Pole za Awali za Rais Samia: Rais Samia atoa pole kwa waathirika Kariakoo. Aagiza kufanywa kila linalowezekana kufanikisha zoezi la uokoaji na tiba kwa majeruhi
“Serikali itaendelea kutoa taarifa zaido kuhusu zoezi la uokoaji hadi hapo zoezi hilo litakapokamilika. Hadi sasa sababu za kitaalamu za jengo hilo kuporomoka bado hazijachunguzwa na kubainishwa, kwani kipaumbele chetu kwanza ni kuwaokoa wenzetu waliokuwa ndani ya jengo hilo.”
“Nashukuru mashirika binafsi na wananchi wote waliojitolea na waliotoa ushirikiano katika zoezi hilo. Nashukuru pia Madaktari wanaoendelea kuhudumia majeruhi. Nampongeza Waziri Mkuu, Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam na timu zao kwa kusimamia kazi kubwa ya uokozi.”
“Baada ya uokozi kukamilia, namtaka Waziri mkuu kuongoza timu ya Wakaguzi majengo, kukagua majengo yote ya eneo la Kariakoo na tupate taarifa kamili ya hali ya majengo ya Kariakoo yalivyo.”
Soma taarifa ya mwaka 2013: Magorofa 64 hatarini kuanguka Kariakoo
Aidha, Rais Samia ameagiza Jeshi la Polisi kupata taarifa kamili kutoka kwa Mmiliki wa Jengo lililoporomoka, kuhusu ujenzi ulivyokuwa unafanyika. Aidha, amesema taarifa zote za uchunguzi zitakapopatikana zitawekwa wazi kwa wananchi wote
Hivi ile sera ya maafa ndio inaelekeza hivyo?Rais Samia ambaye amesafiri kwenda Jijini Rio de Janeiro nchini Brazil 16 Novemba, 2024 kwa mwaliko wa Rais wa Brazil, Luiz Inácio Lula da Silva kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa nchi Wanachama wa Kundi la G20, amezungumza na Wananchi kufuatia kuporomoka kwa ghorofa Kariakoo Jijini Dar es Salaam.
Rais Samia amesema “Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kuporomoka kwa ghorofa katika eneo la Kariakoo Jijini Dar es Salaam. Nimekuwa nikipata taarifa za mara kwa mara kuhusu zoezi la uokoaji kutoka kwa Waziri Mkuu na nimekuwa nikifuatilia zoezi hilo kwa karibu zaidi.”
Pia soma: Live Updates Kuporomoka kwa Ghorofa Kariakoo Nov 16: Watu 7 wengine waokolewa
Amesema “Hadi saa nne asubuhi leo, jumla ya watu 84 wameokolewa na kufikishwa hospitalini kwa ajili ya kupatiwa matibabu. Kati ya hao majeruhi 26 bado wanaendelea na matibabu. Pamoja na hao kwa huzuni kubwa tumepoteza wenzetu 13 katika tukio hilo.”
Aidha ameongeza kuwa “Serikali itabeba gharama za matibabu kwa wote waliojeruhiwa, na kuhakikisha waliofariki wanastiriwa ipasavyo. Nitoe pole kwa ndugu, jamaa na marafiki walioguswa na tukio hili. Niwaombe watanzania wote tuwaweke kwenye maombi wote walioathirika na tukio hili na kuwaweka kwenye maombi waliotangulia mbele za haki.”
Salamu za Pole za Awali za Rais Samia: Rais Samia atoa pole kwa waathirika Kariakoo. Aagiza kufanywa kila linalowezekana kufanikisha zoezi la uokoaji na tiba kwa majeruhi
“Serikali itaendelea kutoa taarifa zaido kuhusu zoezi la uokoaji hadi hapo zoezi hilo litakapokamilika. Hadi sasa sababu za kitaalamu za jengo hilo kuporomoka bado hazijachunguzwa na kubainishwa, kwani kipaumbele chetu kwanza ni kuwaokoa wenzetu waliokuwa ndani ya jengo hilo.”
“Nashukuru mashirika binafsi na wananchi wote waliojitolea na waliotoa ushirikiano katika zoezi hilo. Nashukuru pia Madaktari wanaoendelea kuhudumia majeruhi. Nampongeza Waziri Mkuu, Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam na timu zao kwa kusimamia kazi kubwa ya uokozi.”
“Baada ya uokozi kukamilia, namtaka Waziri mkuu kuongoza timu ya Wakaguzi majengo, kukagua majengo yote ya eneo la Kariakoo na tupate taarifa kamili ya hali ya majengo ya Kariakoo yalivyo.”
Soma taarifa ya mwaka 2013: Magorofa 64 hatarini kuanguka Kariakoo
Aidha, Rais Samia ameagiza Jeshi la Polisi kupata taarifa kamili kutoka kwa Mmiliki wa Jengo lililoporomoka, kuhusu ujenzi ulivyokuwa unafanyika. Aidha, amesema taarifa zote za uchunguzi zitakapopatikana zitawekwa wazi kwa wananchi wote
Sio sasa tu, mimi naona muda wote ni hivyo!!Tukubaliane tu kwa pamoja hii nchi kwa sasa inajiendea tu yenyewe kama gari bovu lisilo na dereva