Rais Tshisekedi siku zake zinahesabika

Rwanda ni dalali tu wa kuina madini DRC kupitia M23. Wezi ni mabeberu na Uganda, DRC hawezi kupigana vita na Mabeberu
Tuache kulaumu mabeberu Kila kitu mbona Zimbabwe walipoenda kumuokoa Kabila Mkubwa waliiba Dhahabu pamoja na majenerali wa Angola??

Pia hapo DRC tayari Kuna kampuni halali kabisa za mabeberu zinachimba madini Sasa why walete vita wakati mkataba wanao tayari?

Huwa sielewi hii dhana hata kidogo, hata Uganda tayari Total Energy Wana mkataba wa kuchimba mafuta ila juzi tu imetokea Ebola watu wanadai eti mabeberu wanataka kupora mafuta kupitia Ebola?? Yaani anaporaje kitu alichomilikishwa tayari??
 
nini lengo kuu la m23?
 
Kwa namna yoyote ile Rwanda hawezi ipiga Congo, ila Congo ni raisi sana kuipiga Rwanda. Njia pekee Rwanda anaweza shinda vita na Congo ni kwa kumu eliminate Tshekedi, otherwise Rwanda mwenyewe hayupo tayari Kigali ifumuliwe aanze ijenga na upya.
Hahahahahaha kweli? Ndo unaamini hivo? Vipi! Unakumbuka mkuu wa majeshi Rwanda aliwahi kuwa mkuu wa majeshi DRC?! Ni wapi kwingine umewahi sikia? Je,hilo wamelisahau? Kaa kimya,subiri mziki wenyewe. Omba tu washambulie uone. Rwanda hainaga uwanja wa vita, zinapigwa huko huko. Kwa hiyo, subiri usicheze kabla mziki haujapigwa
 
DRC ya baada ya 2003 after Second Congo war ina nafuu kuliko utengamano uliokuwepo miaka ile ya vita kali. Tatizo lililobaki kwa jeshi ni kuwa na baadhi ya vilaza waliounganishwa jeshini kama makubaliano ya kuacha mapigano. Hao wapuuzi ndio hawakuwa na mafunzo na wanaongeza idadi tu ya wanajeshi, na jeshi lina wazee wengi. Idadi ya wanajeshi ni zaidi ya 100,000 ila wajinga wajinga wengi tu.
Kwenye mafunzo na nidhamu ndio hamna kitu kabisa.

Kwa sasa waasi ni rejareja zaidi. Ingawa kwenye silaha bado Congo hawajakaa sawa. Mwaka huu vita ya Ukraine ilipoanza walikuwa na vifaru nadhani ni modernized T-64 walikuwa wafanye shipment kwa Congo ila wakavitumia. Procurement inayohitajika ni kubwa na ya miaka kadhaa.

Pamoja na hayo, sioni Rwanda inaishindaje DRC wakipigana sasa hivi. Nasisitiza endapo hakuna external influence kwa yeyote
 
Unataka ushahidi? Ni kwanini waasi wakipigwa wanakimbilia Rwanda na sio Burundi?
 
Kama ni historia basi Azerbaijan mwaka huu na mwaka juzi isiingeishinda Armenia maana pale 1993/94 Armenia iliwashinda.
Mazingira ya 1st na 2nd Congo war yalishabadilika kwa Congo ile
 
Kama ni historia basi Azerbaijan mwaka huu na mwaka juzi isiingeishinda Armenia maana pale 1993/94 Armenia iliwashinda.
Mazingira ya 1st na 2nd Congo war yalishabadilika kwa Congo ile
Sasa mkuu kama M-23 tu inawazidi nguvu majeshi ya Kinshasa let alone ADF na Mai Mai kipi kinakupa confidence wanaweza itandika RPF?.
 
Mkuu Kwamba majeshi ya waasi ndio yanawatu lege lege? How comes Bosco Ntaganda alipokua muasi aliwatandika hao DRC ila akijiunga na majeshi ya serikali eti ndio redundant? Au mtu kama Makenga aliyepigana vita tokea akiwa na umri wa miaka 17 eti alipojiunga serikalini enzi zile za mkataba wa March 23 ndio anageuka mzigo??

Kama majeshi ya serikali ni imara kivipi yanatandikwa na waasi? huko ituri ilibidi wananchi waokolewe na UPC na sio majeshi ya serikali maana hakuna yalichoweza saidia!! Ndio eti kusema jeshi ni dhaifu kisa waasi wamejiunga nalo!!

Naona una overrate sana nguvu ya Kinshasa
 
Kwa akili yako unadhani wale waasi wasio na mafunzo, nidhamu, weredi wala command walioburuzwa maelfu kwa maelfu wakaungwa jeshini kisa walikuwa tu wamemilikishwa silaha wakati wa negotiations ndio wawe sawa na wanajeshi waliofunzwa? Kama walikuwa wanajeshi kamili kwanini walitakiwa kupewa mafunzo after kujiunga jeshini. Mtu kajiunga leo kwenye kikosi cha waasi kwa kulazimishwa au njaa zake, after some days yameletwa makubaliano na anatakiwa ajiunge jeshi la taifa, huyo ndio awe active combatant kulinda mipaka adui akivamia.

Kesi ya Bosco Ntaganda ni tofauti, ukisema sio mwanajeshi basi hata Kagame sio. Wote si wanapigana ile 1994 na hadi DRC ilimpa option ya kuwa General jeshini akakataa. Sultan Makenga ni the same, ana mafunzo. Na hiyo haimaanishi wapiganaji wao walikuwa competent kutumika kwenye jeshi la taifa. Kupigana ukiwa muasi hata mafunzo ya wiki tu yanatosha.
 
Mkuu nchi iwe na demokrasia au isiwe na demokrasia hilo haliwezi kuwa kigezo cha nguvu ya kijeshi.
Nchi inaweza kuongozwa na kidikteta tena na mzee kama China na bado ikawa na nguvu kubwa kijeshi kuliko ile yenye demokrasia ya kubadilisha raisi kila siku.
 
Yep wewe umeandika kile ambacho wakongoman wengi hawataki kukizungumzia au kukisikia.

Tshisekedi na jeshi lake la ndombolo ya solo hawezi kupambana na hawa jamaa hata akiungana na Congo Brazavile wote watapigwa tu.
 
Ndio maana mkuu nikakuuliza kama hao waasi sio competent why wanawachapa jeshi la serikali Kila siku? Yaani sio Nkunda, Ntaganda, Makenga n.k Ina maana askari wasio na mafunzo Wala elimu ni Bora kuliko jeshi la DRC!!

Kumbuka hata Kabila Senior alipindua Mobutu kutumia "vitoto" Sasa kwa namna hii unadhani Hilo jeshi ambalo linazidiwa Competence na rebels ndio Lina uwezo wa kutandika sio jeshi tu Bali Battle-hardened army kama RDF?

Embi tuweni serious, msimuingize Fatshi mkenge
 
Ngoja tusubiri tuone yatakayojiri.
Kwanini Kagame ni jeuri hivi? Nani anampa hii jeuri?
Kagame ana uhakika wa kuitandika Congo wakati wowote na sehem yoyote ndomaana unamuona ana kiburi. Laiti Congo wangekuwa vizuri kijeshi na ki silaha basi kitambo angekuwa ashanywea.

Congo wamejaza wacheza ndombolo yasolo jeshini, wakati Rwanda wamejaza wapiganaji wa vita wenye weledi wa mapigano. So Kagame atakosaje jeuri?
 
Jeshi la Congo limejaza walevi na wacheza ndombolo ya solo, kwahiyo hawawezi kupambana na vijana waliotoboka roho na kuamua kupambana kwa mustakabali wa maisha yao
 
sawa ila rwanda tatizo ni huo uhutu na utusi hapo ndo kuna shida, je kwenye management ya kagame ushawai ona top military au inteligence position yuko mhutu? yani wale top kabisa kuna wahutu? kama hakuna je ni kwa nini wakati wahutu ni 80% ya population?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…