Rais Uhuru Kenyatta: Nchi jirani zinahitaji siasa ambazo ushindani si uadui na vita

Rais Uhuru Kenyatta: Nchi jirani zinahitaji siasa ambazo ushindani si uadui na vita

Tume huru itakuja siku tukichapana kwanza na dola. Kama ilivyokuwa Kenya. As far as kuna amani tume huru tusahau. Nyerere alikosea sana kutuacha bila katiba mpya.
Kweli kabisa. Hii nchi toka Nyerere aondoke kila mtu anajifanyia lake.

Waliokuwa wanadai kuwa CCM ina wenyewe kwa sasa wanaonja joto la jiwe.
 
Nani kawindwa?
Zanzibar wamekufa 13,Lissu alipigwa risasi zaidi ya 16 mchana kweupe makazi ya viongozi,wapinzani awamu hii wamekaa mahabusu sana kwa kesi zisizo na kichwa wala miguu,akina Nusrat Henje wanataabika mahabusu.

Ben saanane kapotezwa na watu ambapo alilalamika na kuweka namba zao humu na aina ya vitisho walivyompa,Mawazo ameuwawa hadharani,Roma mkatoliki kutekwa,Wapinzani kuharibiwa mali zao,wapinzani kubambikiziwa kesi!

Hakuna awamu imekuwa na ukatili kwa wapinzani kama hii ya 5!Miaka 5 inafunika miaka 30 ya mwinyi,mkapa na kikwete!
Shame!
 
Subiri pigo la Jumuia ya Madola ( UN), EU na USA... nao useme the same!!
I hope unaishi nje au chanzo chako cha fedha kipo nje ya Tanzania la sivyo utakuwa una akili mbovu kudhani vikwazo havitaadhiri maisha yako na ndugu zako.
 
Siasa zetu zemekua za kishamba sana, kura zilizoandaliwa kwaajili ya watu fulani zinapenyezwa kwenye sanduku la kura na tukihoji tunapewa kibano na vyombo vya dola.
Kamwe unafiki haujawahi kumwacha mtu salama.
 
Vipi ameongelea pia yale mauaji ya watu 1500 yaliyosababishwa na yeye ile 2007?
Wameshavuka hayo na ndio maana sasa wanafanya siasa safi!Wakiona watu wanataka kutumbukia huko,wanatoa angalizo kwani wao wameyaishi hayo!

Tutamchukia kila mtu anayetushauri vizuri?Maana kila anayesema ukweli mnamuona adui!Tutabaki na China na Uganda tu ambao they dont care!😁
 
I hope unaishi nje au chanzo chako cha fedha kipo nje ya Tanzania la sivyo utakuwa una akili mbovu kudhani vikwazo havitaadhiri maisha yako na ndugu zako.
Kwa hiyo unaminya haki ya wengine kwa kigezo tu kwamba hata hivyo vikwazo vikija vitawaumiza na wao siyo!!

Subiri mapigo yaja!
 
Tatizo kuingia mtaani kwa sasa tumeshashindwa bado tunavumilia.Hivyo for the time being wabunge waende tu bungeni. Hii ya kuingia mtaani itakuja yenyewe pale Magufuli atakuwa katika mwaka wake wa 14 akitawala. Hata wana CCM wenyewe wengi watakuwa wamemchoka. Hapo ndo saa ya ukombozi wa kweli itatimia.

Waende wakafanye nini labda, maana kama Ni hotuba zao kila mara zinazuiwa, na zikiachwa ni zile zilizohaririwa. Na hata ikitokea anachangia wasichopenda, miongozo inakuwa kibao ili kuzuia ujumbe wake kufika kwa umma.

Kibaya zaidi hata mbunge wa upinzani hasa cdm akilazimisha kuchangia wasichopenda, anatolewa kwa kudhalilishwa ili kujengewa taswira mbaya kwa umma kuwa ni mleta Fujo. Labda kama unataka waende kuchukua posho, na kusifia kama anavyofanya huyo mmoja wa cdm aliyeko huko bungeni kwa sasa. Tafadhali usipandikize siasa za kikondoo ndani ya cdm.
 
Hongera Kenyatta,huku kwetu siasa ni uadui,Jiwe uelewa wake upo chini mno
 
Kenya mmekomaa kisiasa. Sisi pia inabidi tuingie mtaani ndo viongozi watapata akili. Ila siku itafika tu ambayo wananchi wengi watasema sasa yatosha kuvumilia. Wenyewe wataingia mtaani.
Hapa Kenya tunasema Tanzania imekomaa kisiasa, sijui tumuamini yupi?
 
Unapendeza tufanye nini katika hii hali mpya kisiasa?. Michango ya mawazo ni lazima katika hali kama hii kisiasa.
Michango ya kusema tumeshindwa kisayansi, huku tumeona vyombo vya dola vikisimamia kura za wizi na umwagaji damu? Labda wapinzani nao waingie msituni tayari kutafuta uongozi.

Timu yako ikifungwa kwa mbinu za mchezo unaweza kuangalia umekosea wapi, lakini iwapo kabla ya mechi wachezaji wako wanne wametolewa kwa kadi nyekundu, halafu mechi ikiwa inaendelea ukiwa na wachezaji pungufu, refa anapuliza filimbi kila ukifika 18 ya wenzako.

Kisha wakati huo huo unaona walinzi wa uwanja wanarusha mpira zaidi ya mmoja uwanjani, halafu goli likifungwa na hiyo mipira iliyorushwa uwanjani refarii anahesabu goli! Sasa kama ww ni kocha au mchezaji unayesemekana umepoteza mechi, unarekebisha udhaifu gani kwenye timu yako hata kama kweli upo?

Hapo utasema una timu mbovu au ni kuwa hakuna mchezo? Hapo ndipo Magu alipofikisha Siasa za nchi yetu, mpaka akina Kenyatta wanaishia kutusanifu.
 
Siasa za Kenya haziwezi kuwa mfano kwetu hata siku moja. Kenya wana nini cha kutufundisha kwenye siasa? Kenya tuwaige kwenye ujenzi wa barabara ambazo hata sisi tunazijenga.

Siasa mbaya kuwahi kujua hapa Africa ya Mashariki ni siasa ya Kenya. Angalia hata kwenye mgawanyo wa rasilimali.

Mwisho; Kwanini Kenya siku hizi inawashwa washwa na siasa za Tanzania? Wapi panawasha tuwakune?
 
Hiyo ni kweli kama ushindani huo ungefanyika kisiasa na sio kutumia vyombo vya dola. Ni sawa na Tyson ajisifie kuwa ni bonge la bondia kwa kumn'gata Evander Hollyfield! Na unathubutu kabisa kujisifia mbele ya wanaume kuwa umeshinda, halafu huwa unajiita msomi! Huwa sishangai Wazungu wakituita manyani, maana hakuna tofauti kati ya msomi na ambaye hajasoma.
Wachangiaji Utopolo kama we were wakati huu hatakiwi. Sasa hivi tunazungumzia tukio ambalo lipo mbele yetu na lazima tukabiliane nalo. Suala la kuonewa halina maana tena, kama kuonewa tumekwisha kuonewa.

Kutoka hapa kwenda mbele kunatakiwa vichwa vya kweli tupate njia sahihi ya nini cha kufanya sawia.

Unalalamika ili iweje ? na kutendwa umekwisha tendwa. Kama chama hakuna tena Chadema katika political elective posts, Uongozi hafifu sana, party strength kwa electorate kipo chini pia.

USIPOTEZE MUDA KUFIKIRIA YAJAYO, KWANZA SASA HIVI UNAFANYA NINI NDIO KESHO INAKUJA.

1) JE, NI AJALI? JEE AJALI ILIPANGWA?
2) TULIJITAYARISHA VIPI NA HII AJALI?
3) TUNA UWEZO WA KUHIMILI AJALI NYINGINE IKITOKEA MUDA MFUPI UJAO?
4) CHAMA KINA RESOURCES ZA KUFANYA MABADILIKO AU MAREKEBISHO YA GHAFLA YA SERA ?

5) WANACHAMA WANAMCHANGO GANI LEO KAMA KUTAKUWA NA MAAMUZI MAZITO?

6) JE, tumefanya uchambuzi wa uchaguzi uliopita na reviews zote
7) JE, tume study consequential benefit au loss ya election hii 2020.
 
Ni lini Kenya imependa Tanzania iliyotulia kisiasa?
Ni lini Kenya imependa Tanzania inayojielewa Kiuchumi?
Kenya inaitaka na kuitamani Tanzania dhaifu hadi kesho.
 
Kenya hawana siasa zaidi ya ukabila na 2022 watauana. mark my words.

Uko sahihi, je sisi tunaweza kuwacheka? Au itakuwa ni mwenye chongo kucheka kengeza? Kabla Magu hajaingia madarakani tulikuwa afadhali kwa nchi zote za Afrika mashariki, je kwa sasa tunaweza kujivunia nini dhidi ya nchi nyingine zinazotuzunguka?
 
Sasa hivi tunavumilia mwaka 2028 wenyewe tutaingia barabarani pale Magufuli atakuwa anamalizia muhula wa tatu kuingia wa nne. Hatutahitaji kina Mbowe wala Zitto.Wenyewe tutatoka.
Magufuli will never seek for a third term But, atakakayeingia baada ya Magufuli atakuwa zaidi yake Mara 10...ombea uishi Hadi 2025 itakuwa ballaa nakwambia...nchi hii inahitaji a no nonsense leader. And I am also thinking Burundi will become part and parcel of Tanzania...watch out for the major changes and Dynamics of politics in this region of Africa
 
Back
Top Bottom