Rais Uhuru Kenyatta: Nchi jirani zinahitaji siasa ambazo ushindani si uadui na vita

Rais Uhuru Kenyatta: Nchi jirani zinahitaji siasa ambazo ushindani si uadui na vita

Kenya mmekomaa kisiasa. Sisi pia inabidi tuingie mtaani ndo viongozi watapata akili. Ila siku itafika tu ambayo wananchi wengi watasema sasa yatosha kuvumilia. Wenyewe wataingia mtaani.
Tunasubiri 2022 si mbali tutawaona walivyokomaa si kuleta maneno. Kati ya Kenya na Tanzania kweli unasema Kenya imekomaa kisiasa, kukomaa ni kuwa na uvumilivu. Tanzania tumekomaa, siasa si swala kupewa kipaumbele kuliko amani na maendeleo.

Sent from my Infinix X655 using JamiiForums mobile app
 
Kenya kiukweli wako mbali sana ktk demokrasia na kiuchumi. It is an engine of east africa economy. Uhuru Kenyata hakumungunya maneno amemrushia dogo jiwe kuwa upinzani sio uadui wala vita. Sas hivi nchi imegawanyika. Alitukuta wamoja chini ya JK leo anataka atuwache tumepalanyika kwa siasa za visasi. Eti niombee. Tangu lini shetani akaombewa na Malaika!!
Huyo Uhuru wako ana hasira umekatwa mrija wa ulaji wa bure wa madini ya Tanzanite yetu na dhahabu, biashara haramu mpakani, na vile JPM amekataa kushirikiana nao kwenye hila yao ya upigaji kwenye mkopo wa korona. Muulize afungue seva Raila afahamu alipata kura ngapi, halafu afisa mkuu IT Chris Msando nani alimuua kinyama?
 
Yaani Kenyatta aliposikia matokeo ya Tanzania nadhani alikuwa anacheka mpaka anachanganyikiwa, haamini kuwa bado kuna nchi zinaweza kuendesha chaguzi zao ili kukidhi utashi wa kiongozi aliyeko madarakani. Amejiridhisha pasi na shaka kuwa bado watanzania wengi ni maiti, ila hao wachache waliokimbia mortuary atawapokea.
Huyu huyu Kenyata aliyeita majaji wakora?

Sent from my Infinix X655 using JamiiForums mobile app
 
Huyu huyu Kenyata aliyeita majaji wakora?

Sent from my Infinix X655 using JamiiForums mobile app
He even ordered security officers be withdrawned from them just when they were heading to decide on the much-rigged election results. Hadi leo hawapatani kabisw na Chief Justice David Maraga. Amemtenga kabisa na wala hampatii ushirikiano.
 
Kusema kweli tukianza kuchambua mapungufu ya siasa za Kenya wengi hapa mtaishia kushangaa tu. Pamoja na mapungufu ya siasa za Tanzania, bado huwezi kulinganisha na ya Kenya.

Ni watoto wadogo tu ndio hawajui ubabe, unyanyasaji na mauaji yaliyofanyika na yanayofanyika kwa wanasiasa wa Kenya kwa miongo mingi sasa. Nani hajui kilichowakuta Thom Mboya, Robert Auko, Mutula Kilonzo, Pro. George Saitoti na wengine wengi? Au mmesahau kilichomtokea mkuu wa kitengo cha IT cha Tume ya Uchaguzi ya Kenya miaka michache tu iliyopita? Mnataka tuweke hapa orodha ya Wakenya walioko uhamisoni kwa sababu za kisiasa? Kuna mtoto hapa hajui yaliyotokea Kenya baada ya uchaguzi Mkuu mwaka 2017?

Kusema kweli kuilinganisha Kenya na Tanzania kisiasa ni sawa na kulinganisha usiku na mchana. Kwa Afrika Mashariki bado hakuna nchi inaifikia Tanzania kwa siasa za kistaarabu na zinazoheshimu haji za binadamu. Hiyo sio kusema sisi hatuna changamoto. Zipo lakini ni chache na za kawaida kulinganisha na wengine.
Jamaa anajikosha kwa sababu anajua hii ni muhula wake wa mwisho; halafu miadi yake na Dr. William Rutto kaivunja baada ya kutimiza malengo yake. Tunaomba JPM adai tausi wetu warudishwe. Asipewe mtu asiyekuwa na shukrani kama huyu jamaa.
 
Yaani Kenyatta ndio wa kuongelea siasa za Afrika mashariki huyu inamaana asema UgandaTz Burundi na Rwanda .

Tanzania tukiamua yutaenda kumyang'anya makuki yeti ya kizungu tuliompa ikulu Kama zawadi ya kutembelea uwanja wetu mpya wa magharibi kazikazi I mwa tz
 
Uhuru Kenyatta naye kageuka mwalimu wa siasa za vyama vingi eti siasa za vyama vingi sio uadui ICC alipelekwa kwa sababu gani? Vita zile walitwangana na kuuuana kule Kenya Baada ya uchaguzi na akina Raila Odinga zilikuwa za Nini adi Kikwete akaitwa kwenda kuwasuluhisha

Ama kweli nyani haoni kundule
Tazama ya Kale yamepita sasa yamekuwa mapya .....kuna ubaya gani watu ambao huko nyuma walishateleza na kujifunza kukushauri na wewe usiteleze ....kama yeye alishaenda ICC akachomoa ndio mwalimu mzuri

Visingizio kama ooh Tanzania ya Mwalimu Nyerere au Kikwete au Mkapa iliwapatanisha hiyo kwetu ni Past ..na ndio inafanya dunia nzima kujiuliza hawa Tanzania ambayo ilikuwa kwenye njia sahihi wanapatwa na nini leo wanataka kuingia kwenye nchi ambazo hazina UTAWALA BORA ??
 
Jamaa anajikosha kwa sababu anajua hii ni muhula wake wa mwisho; halafu miadi yake na Dr. William Rutto kaivunja baada ya kutimiza malengo yake. Tunaomba JPM adai tausi wetu warudishwe. Asipewe mtu asiyekuwa na shukrani kama huyu jamaa.
Kosa lake kuwaambia ukweli? Hamuoni aibu nchi dunia nzima inaongelewa vibaya. Kwani yeye ndio wa kwanza duniani kuisema Tanzania na mwelekeo wake? no wounder marafiki zetu wamekuwa madikteta kama Uganda , Burundi etc
 
Kusema kweli tukianza kuchambua mapungufu ya siasa za Kenya wengi hapa mtaishia kushangaa tu. Pamoja na mapungufu ya siasa za Tanzania, bado huwezi kulinganisha na ya Kenya.

Ni watoto wadogo tu ndio hawajui ubabe, unyanyasaji na mauaji yaliyofanyika na yanayofanyika kwa wanasiasa wa Kenya kwa miongo mingi sasa. Nani hajui kilichowakuta Thom Mboya, Robert Auko, Mutula Kilonzo, Pro. George Saitoti na wengine wengi? Au mmesahau kilichomtokea mkuu wa kitengo cha IT cha Tume ya Uchaguzi ya Kenya miaka michache tu iliyopita? Mnataka tuweke hapa orodha ya Wakenya walioko uhamisoni kwa sababu za kisiasa? Kuna mtoto hapa hajui yaliyotokea Kenya baada ya uchaguzi Mkuu mwaka 2017?

Kusema kweli kuilinganisha Kenya na Tanzania kisiasa ni sawa na kulinganisha usiku na mchana. Kwa Afrika Mashariki bado hakuna nchi inaifikia Tanzania kwa siasa za kistaarabu na zinazoheshimu haji za binadamu. Hiyo sio kusema sisi hatuna changamoto. Zipo lakini ni chache na za kawaida kulinganisha na wengine.
Those are the matters of the past ambayo hata sisi tunazo past zetu zilizotokea awamu ya kwanza ambazo hata rais nyerere alikiri alikosea. Mfano Operesheni Vijiji watu wengi walikufa kwa kuliwa na wanyama, kulala nje na njaa kutokana na kuhamishwa kwa nguvu kutoka kwenye maeneo yao ya asili na kuhamishiwa kwenye vijiji vya ujamaa. Hata sasa ukiongelea mauwaji na utekaji ndio yameshamiri.

Sasa kwakuwa nao walishapata shida huko nyuma kwa upendo wana haki ya kutukumbusha tusiende huko kwenye shida.
Leo hii Ulaya wanaisema Afrika juu ya vita vya wenyewe kwa wenyewe na kiukooo, lakini ukisoma historia ya ulaya wakati wa primitive age wao waliuwana sana kwenye vita vya kikabila, kabla ya kufikia CIVILIZATION. Ukiwa mtu mjinga wakikusema uache ubaguzi na vita vya wenyewe kwa wenyewe utasema mbona hata nyie mlishawahi kuuwana? that is primitive excuse
 
Siasa zetu zemekua za kishamba sana, kura zilizoandaliwa kwaajili ya watu fulani zinapenyezwa kwenye sanduku la kura na tukihoji tunapewa kibano na vyombo vya dola.
Na mnahimizwa "kulinda amani"!

Ulishaona wapi jambazi anavamia halafu yeye ndie anakuwa wa kwanza kuwaambia anaowavamia wasifanye vurugu na kujilinda!

Mtu wa ajabu sana huyu tuliyempata awamu hii.
 
Unataka kuhalalisha UJAMBAZI wenu na matukio ya Kenya?
Mnaiba kura.mnatengeneza kura feki mnaua wenzenu, ndo SIASA gani hizi?
Hata Kama sisi watoto wadogo Ila tunaona mnayoyafanya mliitisha uchaguzi wa nini wakati mlikuwa mna mipango ya WIZI
Ndio maana tunawaita watoto wadogo!

Ungefuatilia siasa za Kenya hata kwa wiki tu ungemshangaa sana Kenyata anapata wapi kibali cha kuwasema nchi za wenzie
 
Unataka kuhalalisha UJAMBAZI wenu na matukio ya Kenya?.
Mnaiba kura.mnatengeneza kura feki mnaua wenzenu,ndo SIASA gani hizi?.
Hata Kama sisi watoto wadogo Ila tunaona mnayoyafanya mliitisha uchaguzi wa nini wakati mlikuwa mna mipango ya WIZI
Tuna mapungufu ndio lakini hayazidi ya Kenya, ndio point iliyopo
 
Kusema kweli tukianza kuchambua mapungufu ya siasa za Kenya wengi hapa mtaishia kushangaa tu. Pamoja na mapungufu ya siasa za Tanzania, bado huwezi kulinganisha na ya Kenya.

Ni watoto wadogo tu ndio hawajui ubabe, unyanyasaji na mauaji yaliyofanyika na yanayofanyika kwa wanasiasa wa Kenya kwa miongo mingi sasa. Nani hajui kilichowakuta Thom Mboya, Robert Auko, Mutula Kilonzo, Pro. George Saitoti na wengine wengi? Au mmesahau kilichomtokea mkuu wa kitengo cha IT cha Tume ya Uchaguzi ya Kenya miaka michache tu iliyopita? Mnataka tuweke hapa orodha ya Wakenya walioko uhamisoni kwa sababu za kisiasa? Kuna mtoto hapa hajui yaliyotokea Kenya baada ya uchaguzi Mkuu mwaka 2017?

Kusema kweli kuilinganisha Kenya na Tanzania kisiasa ni sawa na kulinganisha usiku na mchana. Kwa Afrika Mashariki bado hakuna nchi inaifikia Tanzania kwa siasa za kistaarabu na zinazoheshimu haji za binadamu. Hiyo sio kusema sisi hatuna changamoto. Zipo lakini ni chache na za kawaida kulinganisha na wengine.
Wameshavuko huko,wmekomaa kisiasa na wanajua nini wanakitaka katika siasa safi!

Hata sisi huko nyuma siasa zetu zilikuwa na ahueni,sasa tuko pabaya!Ukiwa mpinzani jiandae kuandamwa na misukosuko kibao kama utabahatika kuishi!

Its a shame! Nyerere aliacha taifa la wamoja na wandugu,leo hii watu wanasherehekea vifo vya wengine kisa itakadi za kisiasa?
 
Pamoja na ukabila na tension kubwa ya capitalism kenya bado ina excel democracy East Africa

Huu mfumo wetu wa kichina na kirusi ni suala la muda tu kamba inavutwa itakatikia panapotakiwa mifano ni mingi waulizwe Arab springs waeleze jinsi mifumo ya serikali isiyojali demokrasia,Uhuru na economic liberalization ilivyoanguka
 
Mapungufu ya makusudi hayo.
Kwani ccm hawajui Kama KUIBA KURA na kutengeneza kura feki NI kosa?.
Hayo ni makusudi.
Na KUJIONA wapo juu ya sheria.
Kisa tu mwenyekiti wa NEC, mkurugenzi wa uchaguzi, CDF, IGP na jaji mkuu wore wanachaguliwa na mwenyekiti wa CCM
Tuna mapungufu ndio lakini hayazidi ya Kenya, ndio point iliyopo
 
Kosa lake kuwaambia ukweli? hamuoni aibu nchi dunia nzima inaongelewa vibaya. Kwani yeye ndio wa kwanza duniani kuisema Tanzania na mwelekeo wake? No wounder marafiki zetu wamekuwa madikteta kama Uganda, Burundi etc
Inakusaidia nini wewe ukiwa na rafiki mnafiki?
 
Mapungufu ya makusudi hayo.
Kwani ccm hawajui Kama KUIBA KURA na kutengeneza kura feki NI kosa?.
Hayo ni makusudi.
Na KUJIONA wapo juu ya sheria.
Kisa tu mwenyekiti wa NEC, mkurugenzi wa uchaguzi, CDF, IGP na jaji mkuu wore wanachaguliwa na mwenyekiti wa CCM
Hayo mengine ni malalamiko yako tu!

Hata trump saa hii analalamika kuibiwa, ila ukweli ni kwamba wananchi wamemkataa kwenye box la kura
 
Tuna mapungufu ndio lakini hayazidi ya Kenya, ndio point iliyopo
Inawezekana kwa sasa hayazidi lakini dunia inaona dalili za kuelekea kuwazidi sio Kenya tu hadi mataifa mengine yanayojulikana hayana demokrasia kwa kasi.

Leo hii tumekaa wiki karibu tatu bila mitandao ...na hata ikiwepo haiwezi kudownload, jiulize hasara kiasi gani imepatikana kwenye uchumi?

Kuna makampuni yanategemea mitandao kwa kila kitu kuanzia kuuza, kununua, kutafuta wateja, uendeshaji etc
Kuna vijana wamejiajiri kuendesha taxi, TAXIFY, BOLT, UBER
Kuna vijana wanauza bidhaa mtandao duka lao ni INSTAGRAM, FACEBOOOK etc

Hapo hatujaongelea uhuru wa kuwasiliana na kupata habari ambao ni takwa la kikatiba na haki za binadamu kimataifa chini ya "Bill of Rights" ambayo Tanzania imeridhia.
 
Back
Top Bottom