Rais Uhuru Kenyatta: Wakenya hawapaswi kujilinganisha na mataifa yanayoficha taarifa za COVID-19

Aliyasema hayo baada ya Wakenya kumtaka alegeze masharti ya Covid-19 wakitolea mfano wa Tanzania ambayo imelegeza masharti ya Covid-19 kwa kiasi kikubwa kama siyo kuyaondoa kabisa.

Kenyatta aliwaambia Wakenya kuwa Kenya ni nchi ya kidemokrasia ambapo uhuru wa habari ni mkubwa na hivyo wasijilinganishe na nchi ambazo hazina uhuru wa habari na ambazo zimekuwa zikificha taarifa za mwenendo wa Covid-19.

Chanzo cha habari hii kimeongeza kuwa kwa mara ya mwisho Tanzania ilitoa taarifa za covid-19 tarehe 29 April, 2020; na waandishi wamepata msukosuko mkubwa walipojaribu kuandika ukweli wa maambukiziya Covid-19 nchini

Kenya imerekodi visa 17,975 vya maambukizi ya covid-19, vifo 285 huku wagonjwa 7,833 wakipona.
 
Wanaotangaza na wasiotangaza, tofauti yao ikoje?

Huwezi kusema NEW CASES kwa siku ni 15,000+ halafu FATALITIES tangu ugonjwa uingie ni 500+, kisha ukaogopa kwamba eti ni tishio duniani.

Records zinaonesha NJAA inaua zaidi ya ugonjwa wowote duniani, tena kila baada ya sekunde wanadondoka watu.

Wao na SA waendelee tu kupimana tu, watangaziane, sisi huku uswahili hali ni shwari haswaa. Mpaka sasa hatujafunga shule hata moja na hakuna hivyo vifo, kama ni kuumwa na kupona, ndio zetu.
 
Ila Tanzania Uhuru wa vyombo vya habari ni mkubwa sana, ndo maana habari za msiba wa rais Mstaafu BM Mkapa, zimeandikwa pasi kikwazo chochote.
 
Wacha kudanganya ulimwengu wewe! Watu wanakufa kila kuchao; eti hamna korona!
 
Tatizo unapochukua pesa za watu ni lazima huwaonyeshe kua unafanya kazi, hapo Uhuru anajaribu kuwafurahisha EU na USA amabao wamefadhili hizo COVID funds.
Na Magufuli anawafurahisha wanani kwa kuficha korona?
 
Si afadhali Kenya wanajitahidi, sisi tumekaa tu tukijidai hakuna korona kumbe watu wanakufa kila leo, tunaficha ukweli!
 
Ila takwimu anazotoa zinaongeza hofu, atafute namna ya kuzitoa. Ajue korona tutaishi nayo kama ukimwi.
 
Aendelee tu na curfews, restrictions na borders' shutdown mpaka apate dawa au chanjo. That might happen in 2023.
 
#truth.
Isiwe kama Tanzania wanaodai coronavirus imeisha kumbe inaua mitaani.
 
Reactions: BAK
On the same page UK, very well said.

 
Hicho ndicho kinachoendelea. Tumeshadanganywa kwamba COVID19 haipo Tanzania lakini ukweli ni kwamba bado vifo vinatokea na kudaiwa wamekufa kwa ugonjwa wa kubana mbavu kumbe ni COVID19.

#truth.
Isiwe kama Tanzania wanaodai coronavirus imeisha kumbe inaua mitaani.
 
Kama kungekuwa na EAC federal government, top brass ingekuwa hivi:

President: Uhuru Kenyatta

VP: Bob Wine au Tundu Lissu au Zitto Kabwe

PM: Paul Kagame au Freedom Mbowe au John P Magufuli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…