Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Aliyemtangulia mfalme.Na Kijazi alikufa kwa mshituko wa moyo
Nijibu maswali haya acha maneno mingi mingi.
1. Wanao shudia mbinguni ni nani?
2.wanao shudia duniani ni nani/ nini/ akina nani.
Ukijibu haya maswali mawili then nitakufafanulia ili uelewe kwa nini huo mpangilio uko hivyo.
Hahaha nimemdharau zaidi aise...sijui y
Kujibu maswali yako na tuanzie hapa
WANAFUNZI WA YESU
Na majina ya hao mitume kumi na wawili ni haya; Wa kwanza Simon aliyeitwa Petro, na Andrea nduguye; Yakobo wa Zebadayo, na Yohana nduguye; Filipo, na Bartholomayo; Tomaso, na Mathayo mtoza ushuru; Yakobo wa Alfayo; na Thadayo; Simon Mkananayo, na Yuda Iskariote, naye ndiye mwenye kumsaliti. (Marko 10:2-4)...
Hujajibu maswali yangu kwa sababu umejua ukiyajibu nitatolea ufafanuzi zaidi na watu humu watapata ufahamu utakao wafanya wajielewe na watatafakari kujua kuwa hee! Kumbe huku tuliko shetani katulaghai kwa kutumia sehemu tu maneno ya Manabii wa Mungu ikiwemo Musa na akamtumia nabii wake kuanzisha dini yake.
Kwa maelezo ambayo nimesha ya toa huko nyuma kwa mfano mwenye akili kesha jua Roho Mtakatifu ni nani na ni nini kwa mujibu wa Biblia. Na sitegemei Biblia itumike tena na mawskala wa shetani kusema nabii fulani ndiye Roho Mtakatifu na alitabiriwa na Biblia kwamba atakuja baada ya Yesu.
Shetani na mawakala wake watafute sehemu nyingine ya kumhalalisha si Biblia.
Vitabu | Mtunzi |
| Judges (Waamuzi) | Huenda akawa ni Samueli |
| Ruth (Ruthu) | Huenda akawa ni Samueli |
| First Samuel (1 Samueli) | Hajulikani |
| Second Samuel (2 Samuel) | Hajulikani |
| First Kings (1 Wafalme) | Hajulikani |
| Second Kings (2 Wafalme) | Hajulikani |
| First Chronicles (1 Mambo ya Nyakati) | Hajulikani |
| Esther (Esta) | Hajulikani |
| Job (Yobu) | Hajulikani |
| Ecclesiastes | Hajulikani |
| Jonah (Yona) | Hajulikani |
| Malachi (Malaki) | Hakuna chochote kinachojulikana |
Vitabu | Watunzi |
| Gospel of Matthew (Injili ya Mathayo) | Hajulikani (“Japokuwa yupo Mathayo aliyetajwa katika orodha tofauti za wanafunzi wa Yesu… mwandishi Mathayo kwa kiasi kikubwa hana jina” (The New Encyclopaedia Britannica, Mj. 14, uk. 824). |
| Gospel of Mark (Injili ya Marko) | Hajulikani (“Japokuwa mtunzi wa Marko huenda akawa hajulikani…” (The New Encyclopaedia Britannica, Mj. 14, uk. 826). |
| Gospel of Luke (Injili ya Luka) | Hajulikani (“Sheria ya Muratori inamtaja Luka, tabibu, mwandani na mfuasi wa Paulo; Irenaeus anamuonyesha Luka kuwa ni mfuasi wa Injili ya Paulo. Eusebius anamuweka Luka kuwa ni tabibu wa Antiocha, ambaye alikuwa na Paulo ili kuipatia Injili mamlaka ya kiutume” (The New Encyclopaedia Britannica, Mj. 14, uk. 827). |
| Gospel of John (Injili ya Yohana) | Hajulikani (“Kutokana na dalili za ndani, Injili hii iliandikwa na mwanafunzi mpenzi ambaye jina lake halijulikani” (The New Encyclopaedia Britannica, Mj. 14, uk. 828). |
| Acts (Matendo) | Mtunzi wa Luka (The New Encyclopaedia Britannica, Mj. 14, uk. 830.) |
| I, II, III John (1, 2, 3 Yohana) | Mtunzi wa Yohana (The New Encyclopaedia Britannica, Mj. 14, uk. 830). |
Nimekujibu labda akili yako ni ya mgando. Hivi hizi habari zote za yesu, Roho Mtakatifu na mitume wengine , wewe si umezipata kwa kusoma biblia.
Kwa hivyo Mwanzo unatakiwa ufahamu kuwa Biblia si kitabu kinachotoka kwa Mwenyezi Mungu.
Vitabu vitukufu vilivyoteremshwa na Allaah Aliyetukuka ni Suhuf (nyaraka) za Nabii Ibraahiym (‘Alayhis Salaam), Taurati ya Nabii Muusa (‘Alayhis Salaam), Zaburi ya Nabii Daawuud (‘Alayhis Salaam), Injili ya Nabii ‘Iysa (‘Alayhis Salaam) na Qur-aan ya Nabii Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).
Biblia ni neno lililotokana na neno la Kigiriki Biblios lenye maana ya mkusanyiko wa vitabu vingi.
Biblia yenyewe inatuhakikishia kuwa kuna mikono ya waandishi iliyoingia katika kutunga walichotaka ndani yake.
Hii ni kwa mujibu wa Yeremia 8: 8:
“Mnawezaje kusema: ‘Sisi tuna hekima, sisi tunayo sheria ya Mwenyezi-Mungu,’ hali waandishi wa sheria wameipotosha sheria yangu?”
Kulingana na wanazuoni wa Biblia, hata utunzi wa vitabu vya Agano la Kale na Anaajiyl (wingi wa Injili) zenyewe zina shaka na utata.
Taurati
Vitabu vitano vya kwanza vya Biblia (Pentateuch - Mwanzo, Kutoka, Walawi, Hesabu na Kumbukumbu la Sheria.) kiada zinanasibishwa na Nabii Muusa (‘Alayhis Salaam), hata hivyo, zipo aya nyingi sana katika vitabu hivi ambazo zinaashiria kuwa haiwezekani kwa Nabii Muusa (‘Alayhis Salaam) kuwa aliandika kila kitu ndani yake.
Kwa mfano, Kumbukumbu la Sheria 34: 5 – 8 inayosema:
“Basi Mose (yaani Musa) mtumishi wa Mwenyezi Mungu akafariki huko nchini Moabu kulingana na neno la Mwenyezi Mungu alilosema. Mwenyezi Mungu akamzika katika bonde la Moabu, mkabala wa mji wa Beth-peori; lakini mpaka leo, hakuna mtu ajuaye mahali alipozikwa. Mose alikuwa na umri wa miaka mia moja na ishirini alipofariki; macho yake yalikuwa hayajafifia, na alikuwa timamu na mwenye nguvu. Waisraeli waliomboleza kifo chake kwa muda wa siku thelathini kwenye nchi tambarare ya Moabu. Kisha siku za matanga na maombolezo ya kifo chake zikaisha”. Ni dhahiri kuwa mtu mwengine ndiye aliyeandika aya hizi kuhusu kifo cha Nabii Muusa (‘Alayhis Salaam).
Katika kiambatisho cha RSV kilichopatiwa anwani “Books of the Bible – Vitabu vya Biblia”, yafuatayo yameandikwa kuhusu utunzi wa zaidi ya thuluthi ya vitabu vilivyobakia katika Agano la Kale:
Vitabu MtunziJudges (Waamuzi) Huenda akawa ni Samueli Ruth (Ruthu) Huenda akawa ni Samueli First Samuel (1 Samueli) Hajulikani Second Samuel (2 Samuel) Hajulikani First Kings (1 Wafalme) Hajulikani Second Kings (2 Wafalme) Hajulikani First Chronicles (1 Mambo ya Nyakati) Hajulikani Esther (Esta) Hajulikani Job (Yobu) Hajulikani Ecclesiastes Hajulikani Jonah (Yona) Hajulikani Malachi (Malaki) Hakuna chochote kinachojulikana
Hata Zaburi nayo ina matatizo kwani katika Sura ya 72: 20 inasema: “Mwisho wa sala za Daudi mwana wa Yese”. Lakini Zaburi inaendelea hadi Sura ya 150. Je, ni nani aliyeandika Zaburi 73 – 150? Sura ya 73 ina kichwa cha habari: Haki itatawala (Zaburi ya Asafu). Je, huyu Asafu ni nani?
Apocrypha
Zaidi ya nusu ya Wakristo duniani ni Wakatoliki. Nakala yao ya Biblia ilichapishwa mwaka wa 1582 kutoka kwa Jerome’s Latin Vulgate (Biblia ya Kikatoliki ya Jerome), na kunakiliwa tena hapo Douay mwaka wa 1609. Agano la Kale la Roman Catholic Version (RCV – Nakala ya Kikatoliki) ina vitabu saba zaidi kuliko KJV inayotambulika na Waprotestanti. Vitabu hivi vya ziada zinajulikana kama Apocrypha (yaani utunzi wenye shaka) na zilitolewa kutoka katika Biblia katika mwaka wa 1611 na wanazuoni wa Biblia wa Kiprotestanti.
Anaajiyl
Aramai ilikuwa ndio lugha iliyokuwa ikitumiwa na Mayahudi huko Palestina. Kwa hiyo, inaaminika kuwa Yesu na wanafunzi wake walizungumza na kufundisha kwa Kiaramai. “Simulizi za kwanza ya mdomo za matendo ya Yesu na kauli zake bila shaka zilisambaa kwa Kiaramai. Hata hivyo, Injili nne ziliandikwa kwa ukamilifu wake kwa maneno mengine, Kiyunani ya kawaida, lugha iliyokuwa ikitumika katika dunia ya Kistaarabu ya Mediterania, ili kutumikia wengi katika Kanisa, ambayo ilikuwa ni ya Kiyunani (wenye kuzungumza Kigriki) badala ya Kipalestina. Mabaki ya Kiaramai yalikuwepo katika Anaajiyl za Kiyunani. Kwa mfano, katika Marko 5: 41, “Kisha akamshika mkono, akamwambia, ‘Tal’itha cu’mi’, maana yake, ‘Msichana mdogo, nakuambia amka’”. Pia Marko 15: 34: “Saa tisa alasiri Yesu akalia kwa sauti kubwa, ‘Eloi, Eloi, lama sabachthani?’ maana yake, ‘Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?’” (Encyclopedia Americana, Mj. 3, uk. 654).
Injili ya Marko katika Agano Jipya, japokuwa inachukuliwa na wanazuoni wa Kanisa kuwa ndio kongwe kabisa kati ya Anaajiyl, haikuandikwa na mwanafunzi wa Yesu. Wamehitimisha wanazuoni wa Biblia, kutegemea na dalili zinazopatikana katika Injili, kuwa Marko mwenyewe hakuwa mwanafunzi wa Yesu. Zaidi ya hayo, kulingana na wao, haijulikani kamwe huyu Marko alikuwa nani kwa uhakika. Mwandishi wa kale wa Kikristo, Eusebius (325 BI), alipokea kuwa mtunzi mwengine wa zamani, Papias (130 BI), alikuwa wa kwanza kuinasibisha Injili kwa John Mark (Yohana Marko), mwandani na mfuasi wa Paul (Paulo). Wengine wametoa rai kuwa huenda alikuwa mwandishi wa Petro na ilhali wengine wanaona kuwa huenda alikuwa mtu mwengine kabisa.
Hiyo ndiyo hali ya Injili nyingine. Japokuwa Mathayo, Luka na Yohana yalikuwa majina ya wanafunzi wa Yesu, waandishi wa Injili hizo waliokuwa na majina ya wanafunzi hao mashuhuri, lakini ni watu wengine ndio waliotumia majina yao ili maelezo yao yapate kusadikika. Kwa hakika, Injili zote zilisambaa hapo awali bila majina. Baadaye majina yenye kuaminika yalipatiwa kama watunzi wa Injili hizo na watu wasiojulikana katika kanisa za awali.
Vitabu WatunziGospel of Matthew (Injili ya Mathayo) Hajulikani (“Japokuwa yupo Mathayo aliyetajwa katika orodha tofauti za wanafunzi wa Yesu… mwandishi Mathayo kwa kiasi kikubwa hana jina” (The New Encyclopaedia Britannica, Mj. 14, uk. 824). Gospel of Mark (Injili ya Marko) Hajulikani (“Japokuwa mtunzi wa Marko huenda akawa hajulikani…” (The New Encyclopaedia Britannica, Mj. 14, uk. 826). Gospel of Luke (Injili ya Luka) Hajulikani (“Sheria ya Muratori inamtaja Luka, tabibu, mwandani na mfuasi wa Paulo; Irenaeus anamuonyesha Luka kuwa ni mfuasi wa Injili ya Paulo. Eusebius anamuweka Luka kuwa ni tabibu wa Antiocha, ambaye alikuwa na Paulo ili kuipatia Injili mamlaka ya kiutume” (The New Encyclopaedia Britannica, Mj. 14, uk. 827). Gospel of John (Injili ya Yohana) Hajulikani (“Kutokana na dalili za ndani, Injili hii iliandikwa na mwanafunzi mpenzi ambaye jina lake halijulikani” (The New Encyclopaedia Britannica, Mj. 14, uk. 828). Acts (Matendo) Mtunzi wa Luka (The New Encyclopaedia Britannica, Mj. 14, uk. 830.) I, II, III John (1, 2, 3 Yohana) Mtunzi wa Yohana (The New Encyclopaedia Britannica, Mj. 14, uk. 830).
Gavana Maneno yako mengi hayasaidii.
Musa hakushushiwa Tourati. Mungu alikutana na Musa Mlimani Sinai na kumuandikia vibao viwili vya zile Amri 10.
Wana wa Asafu walichaguliwa na Daudi ilikuwa sehemu ya kusifu na kumuabudumu Mungu katika hema ya kukutania. Daudi alikuwa na Roho wa Mungu/Mtakarifu baadacya kupakwa mafuata na Swameli,. Na huyu Roho wa Mungu ndio alimsaidia katika kuandika na kuimba Zaburi kutokana na changamoto mbalimbali za maisha yake. Kumbuka Daudi alimumbia na kumpigia kinubi mfalme Ssuli kupoza yule roho mchafu aliye mvaa na kumuingia kutoka kwa Mungu baada ya Sauli kukengeuka na kunyanganywa Ufalme na Roho wa Mungu na kumtoka ndani yake. Tafuta kwenye Biblia utaona.
Kama hujui Roho Mtakatifu ni kitu gani mpaka kufikia kudanganywa kuwa ni mtume au nabii. Wakati ukweli ni Roho wa Mungu anaye ishi ndani ya watu wake.
Walioandiki Agano Jipya waliongozwa na Roho Mtakatifu. Yohana na Paulo ni mfano mmoja wapo.
Sehemu pekee katika Biblia alipotajwa Roho Mtakatifu ni katika Yohana 14:26;
“Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote niliyowaambia.
“Ni kipi kile ambacho Roho Mtakatifu ameleta au kufundisha kwa miaka 2000 iliyopita?26.Wakristo wanasema kwamba Msaidizi maana yake ni Roho Mtakatifu
(Yohana 14:26) Yesu alisema katika Yohana 16:7-8. “Lakini mimi nawaambia iliyo kweli; yawafaa ninyi mimi niondoke; kwa maana mimi nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu;” Hii haiwezi kumaanisha Roho Mtakatifu; kwa vile Roho Mtakatifu inasemekana kwamba alikuwepo hata kabla ya Yesu hajazaliwa kama ilivyo katika Luka 1:41 “Elisabeti akajazwa Roho Mtakatifu”.
Hapa, Roho Mtakatifu vile vile alikuwepo wakati wa Yesu: sasa vipi hii imaanishe kwamba ni sharti aondoke Yesu ndipo Roho Mtakatifu aweze kuja?
Katika Yohana 16:7-8, inasema; “Bali mimi nikienda zangu, nitampeleka kwenu. Naye akiisha kuja, huyo atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na hukumu.”
Je, hii “Yeye” hapa inamaanisha nini? Je, viwakilishi hivyo havimaanishi mtu mwanamume?
Je, Roho Mtakatifu anazungumza na Wakristo wema na waovu vile vile?
Je, Roho Mtakatifu yu pamoja nao wakati wote au wakati fulani tu?
Je, ni wakati gani anaanza kumtembelea mtu atakaye kuwa Mkristo?
Utasemaje kuwa wewe ni Mkristo ikiwa Roho Mtakatifu yu ndani ya Mkristo mwingine?
Inakuwaje Wakristo wengi wanawapumbaza watu kwa kudai kwamba Roho Mtakatifu yu ndani yao tu! Na baadaye wanabadilisha dini?
Je, Roho Mtakatifu anaamuru kile ambacho Wakristo wanapaswa kukifanya bila ya uhuru wa kuchagua hata kidogo au anawaongoza tu na wao wana uhuru wa kufuata au kuto fuata?
Ikiwa Roho Mtakatifu anaamuru kile Wakristo wanachopaswa kukifanya, kwa nini Wakristo wanafanya maovu na madhambi?
Vipi unaweza kuuelezea ubadilishaji wa dini na kuingia dini na imani mbali mbali kunakofanywa na Wakristo wengi?
Je, Wanaambiwa kufanya hayo na Roho Mtakatifu?
Ikiwa Roho Mtakatifu anawaongoza Wakristo tu, na wako huru kufanya wanavyotaka, sasa ni vipi tutajua kwamba waandishi wa Biblia hawakufanya makosa wakati walipoziandika?
Ikiwa Wakristo wanaamini kwamba Roho Mtakatifu huwajia na kuzungumza nao kila siku, kwanini hawamuulizi Roho Mtakatifu kuhusu chapisho lipi la Biblia wanalopaswa kulifuata kwa vile kuna machapisho mengi?