Gavana umesema Uongo. Roho Mtakatifu/Roho wa Mungu katajwa sehemu nyingi. Agano Jipya takribani mara 90.
Mwanzo 1:2 Roho wa Mungu aliatamia giza lililo kuwa juu ya maji yaliyo ifunika nchi kuonesha kile kikichoatamiwa kilikuwa kitakatifu. Alimuingia Mariamu Mama wa Bwana Yesu kuonesha mimba ile na kilichoko tumboni mwake ni Kitakatifu.
Sauli Mfalme wa kwanza wa Israel baada ya Taifa hilo kuongozwa na Waamuzi alingiwa na Roho Mtalatifu akacheza kama manabii aliokutana nao wakati anatoka kupakwa mafuta akirudi nyumbani kwa baba yake kutoka kuwatafuta punda waliopotea kutimiza mpango wa Mungu juu ya Sauli. Hii inaonesha Manabii wa kweli wa Mungu acha akina balamu walikuwa wamejazwa Roho w a Mungu.
Kusema kweli ukitafakali Hannah mama wa kuhani Samweli naye alijawa na Roho Mtakatifu. Kama utaunganisha maneno yale yaliosemwa siku ya Pentekosti kwamba wamelewa mvinyo mpya asubuhi. Eli alimtuhumu Hannah kuwa kalewa asubuhi asijue kuwa alijawa Roho wa Mungu na aliye muongoza kufanya maombi kwa kuugulia 1Samweli 1 na Matendo 2. Kimsingi hii mistari uliyo inukuu ya Yohana ilitimilizwa hapo Matendo 2.
Mkristo aliye mkubali Bwana Yesu, Akatubu dhambi zake aka Batizwa na kuwekewa mikono na Mtumishi wa kweli wa Mungu jua fika ana Roho wa Mungu ndani yake.
Ni kuulize Gavana huyo Mtume ambaye shetani na mawakala wake hudanganya wafuasi wa imani hiyo kwa kutumia nukuu za Mistari ya Biblia kuhusu Roho Mtakatifu. Je alikuwa ndiye àliye kuwa akiatamia juu ya maji wakati wa uumbaji? Je ndiye aliye atamia mimba ya Bwana Yesu tumboni mwa Mariamu mamaye Yesu? Jibu ni rahisi hapana. Ndio uone shetani alivyo baba wa uongo na hata mawakala wake walivyo waongo na wapotoshaji wa Neno la Mungu/Biblia. Wamewadanganya wengi kwa mamilioni ha kakika wameishia na wataendelea kuishia motoni kama Neema na Rehema za Mungu hazitafungua akili zao na kuamua kufuata njia sahihi na kuachana na hii njia ya uongo.
Kinachotokea kufanya kutokuona kujidhihirisha kwa huyo Roho wa Mungu ni dhambi za baadhi ya wa Kristu. Ukitenda dhambi unamuhuzunisha Roho wa Mungu hivyo hawezi kujidhihirisha nackuonesha nguvu na uweza wake.
Hili la Biblia kuwa ziko matoleo mengi nilikuambia huko nyuma wale wasiku ya Pentekosti walipojawa Roho Mtakatifu walishuhudia matendo ya Mungu kwa lugha za mataifa yote ya Dunia. Usitegemee Biblia ya kufanana Nenobkwa Neno angalia maudhui ya mstari husika.
Kumbumbuka hili shetani ni baba wa uongo wote. Hivyo hivyo mawskala wake huko mitandaoni unako nukuu haya maandishi yako. Jeepushi na uwakala wa shetani maana hatima yako itakuwa lile tanuri liwakalo moto milele yote/jehanamu.