TANZIA Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli afariki Dunia kwa ugonjwa wa Moyo hospitali ya Mzena jijini Dar

TANZIA Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli afariki Dunia kwa ugonjwa wa Moyo hospitali ya Mzena jijini Dar

Status
Not open for further replies.
Innalillah Wainnailah Rajiun
Wote tutapita huko Mungu atupe mwisho mwema.
 
Kwa nini viongozi wetu wametudanganya?
Yawapasa wajiuzulu, kwa nini waongopee taifa, wataweka wapi sura zao?
 
Wewe jamaa Sasa hivi nakufuatilia Sana post zako.
Nimegundua unajua mambo mengi Sana mazito ya nchi hii.
Ulikua mtu wa kwanza kusema
Soooooooooooooo sad.
Kwa kifupi nimekukubali.asante sana.ukaendelea kutoa yaliyokua yanajiri nyuma ya pazia.
Salute sir.

Hawa wasaidizi wote wa Rais waliokuwa naye hadi dakika ya mwisho; waliokuwa wakidhibiti habari na pesa wanatakiwa kuona aibu na Kukamatwa watuambie vizuri

Huwezi kukaaa na taarifa za mgonjwa ambaye hawezi kujitetea na kumfanya kama mateka kwa wiki mbili hakuna taarifa; walikuwa na nia Gani; lazima waandike maelezo vizuri; haiwezekani; Magufuli ni Rais na hakuwa mfungwa !!!!!!

Diwani Athumani pia anatakiwa kuwa responsible kama kweli naye alikua anajua na hanakushauri ...
Nina imani kabisa Watanzania wangependa kumsaliaa Rais wao regardless tofauti za kiitikadi
Hii ni kosa kuwa sana pia kwa Bashiru Ali na wafuasi wote hao !!! wana kesi ya kujibu kama sio mahakamani ni kwa wananchi ...na immediately wanapoteza sifa ya kuendelea hata kuratibu msiba huuu kwani inaonekana wao siku zote hizi walikua busy na mambo mengine
 
Sijui kwanini nawaza na kujiaminisha nchi inarudi kwa JK. Namwona mtu kama JK kakamata rimoti kontroo kwa mbali....
JK mtu wa maneno maneno atatuharibia nchi tena; labda kama Mkapa angekuwa hai angekuwa ni nguzo nzuri lakini siyo huyu JK! Watu wanamkumbuka JK kwa meneno maneno ya kujisikia vizuri, hela kutoka njia za mkatomkato na mishen town lakini siyo kwa mambo thabiti ya kitaifa.
 
Wengi wameumizwa sana.
Ajabu ya Mungu, utawala wake ulikataza wananchi kumuombea Lissu apone, na yeye hatukupewa fursa ya kumuombea!
Mungu amrehemu
 
Katika hotuba yake kule Tanga alikohoa na kulazimika kuweka maiki pembeni

Leo wakati anatangaza naomba ufanye tathmini namna alivyokuwa amavuta pumzi kwa shida kidogo kisha utapata jibu.
 
Samia akiona analazimishwa Bashiru awe Makamu ajue na yeye atakuwa fixed ili chatoz waendelee kutawala

Bashiru na wenzake wa genge wanatakiwa kuwa ndani ; wote waliokua wanadhibiti ugonjwa wa Rais ; walificha habari kwa maslahi yao kwa nia Ovu ya kupata madaraka
 
Waliotudanganya ni wawili tu... Majaliwa na yule mkuu bwana Chalamila

Mama yetu alisema ukweli kabisa. ..

Tumuunge mkono mama yetu....
Majaliwa nae akatuambia kuwa Rais ni mzima anaendelea kuchapa kazi. Ina maana alisema uongo? Tena akiwa msikitini? Kwanini hakusema ukweli ili watanzania tuungane kumuombea Rais wetu?
 
JK mtu wa maneno maneno atatuharibia nchi tena; labda kama Mkapa angekuwa hai angekuwa ni nguzo nzuri lakini siyo huyu JK! Watu wanamkumbuka JK kwa meneno maneno ya kujisikia vizuri, hela kutoka njia za mkatomkato na mishen town lakini siyo kwa mambo thabiti ya kitaifa.
Sasa tufanyeje tena? Ndio ishakuwa hivyo tena...
 
Bro, mimi sijawahi kupiga kura na wala sitopiga kura, ila kifo cha mtu sio cha kufurahia hata kama ametenda mabaya, vipi wewe hapo umetenda mabaya kiasi gani.? Je Mm nmetenda mabaya kiasi gani.? Kila mtu atahukumiwa na Mungu kwa wakati wake
#mwacheAtangulieTutamkuta
 
Kabisa aisee hawakukosea waliosema Mwenyezi Mungu Mkubwa. Dhuluma za kutisha nchini kuanzia bomoa bomoa, wakulima, Wafanyakazi, wafanyabiashara, wapinzani, mauaji ya kutisha, manyanyaso, udhalilishaji etc wote hawa walimshtakia Mwenyezi Mungu.
Unapata faida gani kuandika hayo yote mkuu? Kuna mabaya amefanya, ni kweli lakini pia kuna mema mengi sana kayafanya..

Hayo mabaya yake tumemsema huku kwa miaka zaidi ya mitano sasa, kwa hili lililotokea angalau tuache kumsimanga..
 
Majaliwa nae akatuambia kuwa Rais ni mzima anaendelea kuchapa kazi. Ina maana alisema uongo? Tena akiwa msikitini? Kwanini hakusema ukweli ili watanzania tuungane kumuombea Rais wetu?

Msimlaumuu, alikua anaongea tu kufunika hali hakuwa na taarifa sahihi; kina Bashiru; Msigwa; Dotto; Dr. Hassan na wengine ndio walikuwa wanajua

Ndio maana mnaona in frustration aliamua hata kukata ziara akatulia maana kauli yake ilimuaibisha
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom