TANZIA Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli afariki Dunia kwa ugonjwa wa Moyo hospitali ya Mzena jijini Dar

TANZIA Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli afariki Dunia kwa ugonjwa wa Moyo hospitali ya Mzena jijini Dar

Status
Not open for further replies.
Kweli mkuu bila katiba nzuri maamuzi ya msingi kuhusu taifa yanaweza fanywa kwa namna ya kuharibu.
Kabisa! Huenda Lengo lake lilikuwa zuri lakini halikulindwa na katiba!
Sasa ni vyema tukaandika katiba ili uongozi utokane na katiba siyo mtu!
 
Na kuna kitu nakuwa napata hisia...

Kuna watu walio katika uongozi wataanza kujifanya wao ndio Magufuli waliobaki, si ajabu vikatokea vimtu kama kina Sabayer kwa mwamvuli wa kumuenzi the real JPM vikaongoza watu kwa mabavu kupitiliza!
Ni bora hivyo mara 1000 kuliko tukishika kushika uelekeo tofauti.

Haitachukua muda mrefu kuanza kumkumbuka.
 
Ulipopewa jogoo kule Kibiti ulisema na baba yako ameshafariki, yule mtu anaweza kuwa baba yako.

Ulikwenda Bukoba ukawaambia wewe hukuleta tetemeko kwahiyo hutaleta chakula.

Ulisema chuchu moja la sidiria linatosha kushona barakoa.

Ulimwambia Mwalimu Mkuu, kama hujaoa nitakutoa katika hii shule, huwezi kufundisha mabinti wazuri wakati huna mke.
 
Kuna watu wamechangia Kifo cha Rais Wetu Mpendwa. Watanzania Sisi Sio Wavivu wa Kuomba kwa Mungu lakini Hatuwezi Kuomba Gizani Bila Kujua. Kama Tuliweza Kufunga kwa Kuomba Kuhusu Corona Mwaka Uliopita Tusingeshindwa kufunga na Kuomba Kwa Siku 3 kati ya Tarehe 06/3/2021 hadi leo, Huenda Mungu angesikia Maombi Yetu

Kinachoniuma nilishindwa kuingia Kwenye Maombi Serious Nikiwaamini Viongozi wangu waliokuwa wanasema Rais Yupo Salama.

Najuta Sana Kumuamini Mwanasiasa, Magufuli alikuwa mtu wa Kanisani Tusingeshindwa Kumuombea...... inauma Sanaa Anafariki mtu unae mpenda na kushindwa hata kumuombea. Nililiamini Jeshi La Polisis lilokuwa linakamata watu wanaoitwa Wamezusha Taarifa za Uongo kuhusu kuumwa Kwa Rais kumbe ningewasikiliza hao ningekuwa Nimemuweka Rais Kwenye Maombi.

Shame on You Wanasiasa Mliotudanganya na tukashindwa kama Watanzania Kumuweka Rais Wetu Kwenye Maombi. Daima alitusisitiza Kwenye Kufanya Dua lakini Wanasiasa Uchwara wamemuangusha. Pumzika Kwa Amani Rais na Lawama hizi Zimfikie Waziri Mkuu popote ulipo. Zikufikie msemaji Wa Serikali Kwa Kushindwa Kuongea mambo muhimu ya kiserikali na kuja kutudanganya. Lawama Hivi ziwafikie wabunge wote na Wengine. PUMZIKA KWA AMANI RAIS WETU
 
Bro, mimi sijawahi kupiga kura na wala sitopiga kura, ila kifo cha mtu sio cha kufurahia hata kama ametenda mabaya, vipi wewe hapo umetenda mabaya kiasi gani.? Je Mm nmetenda mabaya kiasi gani.? Kila mtu atahukumiwa na Mungu kwa wakati wake
Nishakujibu sijafurahishwa na kifo mkuu mbona unakuwa sio muelewa? Sehemu gani inaonyesha nimefurahi? Nilichosema tutende mema kwa wenzetu, tusiwafanyie wenzetu mabaya kisa ya cheo, pesa or any pride maana dunia tunapita..UBAYA UBAYA TU, MITANO au SABA TENA.
 
Nishakujibu sijafurahishwa na kifo mkuu mbona unakuwa sio muelewa? Sehemu gani inaonyesha nimefurahi? Nilichosema tutende mema kwa wenzetu ,tusiwafanyie wenzetu mabaya kisa ya cheo,pesa or any pride maana dunia tunapita..UBAYA UBAYA TU ,MITANO au SABA TENA.
Best nimecheka na hii comment🤣..neno mitano tena limekufa rasm dah
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom