TANZIA Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli afariki Dunia kwa ugonjwa wa Moyo hospitali ya Mzena jijini Dar

TANZIA Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli afariki Dunia kwa ugonjwa wa Moyo hospitali ya Mzena jijini Dar

Status
Not open for further replies.
Nilivyoamka saa saba usiku nakutana na meseji ya mpenzi wangu kuwa magufuli amefariki.nikaingia instagram nakuta na hizi habari. Nikaingia JamiiForums.
Nikalog out kwanza.
Nikawa naingia kama guest user .
Sikukoment kitu mpaka asubuh ndo nimeanza kukoment.
Binafsi kama siamini vile.
 
"Heri sifa njema kuliko marashi mazuri; Na siku ya kufa kuliko siku ya kuzaliwa. Heri kuienndea nyumba ya matanga, kuliko kuiendea nyumba ya karamu. Kwa maana huo ndio mwisho wa Wanadamu wote, naye aliye hai atautia moyoni mwake.

Huzuni ni afadhali ya kuliko kicheko, maana simanzi ya uso ni faida ya moyo". MHUBIRI 7:1-3
 
Kiukwel gap ya Magufuli hakuna mtu ataliziba, kaacha viatu vikubwa mno hakuna vitakaemtosha.
Kuna wengine wanachukulia ‘Utani’ lakini seriously Tanzania tumepoteza mwanga uliokua unamulika mbali japo ulikua wenye kutuletea maumivu makali machoni petu.

Kuna siku tutasema wote kwa pamoja Bora Magufuli kwa sababu alikua mwenye maono mengi, makubwa na mazuri kiasi kwamba sidhani kama kuna mtu mwingine alie nchini mwenye maono kama yake

Rest In Peace Mr. President [emoji24]
Hata mimi nilimkubali kama wewe, na hata Jana baada ya kupata taarifa niliumia sana mpaka nikashindwa kulala , usingizi uligoma kuja, Yani nilikuwa na maumivu yaliyochanganyikana na furaha kwa mbali.

Ila alifanya mazuri mengi sana na nimemkubali sana, pia mapungufu nayo yalikuwepo yameumiza wengi sana.

Naomba tupage kiongozi ambaye atakuwa na maono Kama Magufuli na mixture Kikwete, JKN .

Pengo la raisi linazibika ila kwa fimilia ndio halitazibika, Mungu aipe faraja familia yake. Katika kipindi hichi kigumu.
 
Hakika taifa letu limempoteza Mtu ambaye si rahisi kumpata, kwakweli ni mshituko mkubwa ndani ya Taifa letu.
naona kiza kinene kimetanda kila kona lkn Tunamuomba Mungu atuvushe salama ktk kipindi hiki kigumu.
Mungu ana watu wengi wewe katika taifa hili hayo ndo yaleyale makufuru tunayoyasema kila siku hamjifunzi tu.
 
We unaamini kafariki jana?kuna protocols za kufuata hawatangazi tu! Possible alikufa one week before,wakaweka mambo sawa kwanza!na kucheki to do list zake na process za msiba na replacements zitaendaje na nani atakua nani before kupeleka public. Msiba Rais ni national and regional issue sio family issues.
Sasa si wawe wanasema ukweli lini alikuwa ameshafariki.

Kwani wakisema trh 9.3 lkn trb za kiserikali zilikuwa zinafanyika kuna dhambi gani.

Serikali za uongo uongo hazipati mafanikio.
 
Maisha ni fumbo.

Tumia muda wako kufanya mazuri kwani siku moja utapotea kama nukta moja ya mchanga baharini na kitakachobaki ni historia yako iwe ya mabaya au mazuri.
Hata kama ulimchukia au kumpenda ila kifo ni kifo. upendo na chuki vyote havina faida sasa hivi.
Binadamu wenye moyo watanielewa.

Sifurahii wala Sisikitiki.
Kweli kabisa, wema unalipa
 
Hii ni kweli?
Mbona hawakutuambia kuwa anaumwa? Kwa hakika hapa serikiali imechemsha. Kuumwa ni ubinadamu. Wangetueleza tu ili tuanze kujiandaa kisaikolojia. Badala ya kutwambia ukweli wanasema oh yuko mzima kabisa anachapa kazi (Majaliwa) au amenipigia simu leo na ametuletea pesa (RC Chalamila). Wakati huo huo watu wanakamatwa kwa kusema tu kuwa Rais ni mgonjwa. Mama Samia, tunakuombea ufungue ukurasa mpya!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom