TANZIA Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli afariki Dunia kwa ugonjwa wa Moyo hospitali ya Mzena jijini Dar

TANZIA Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli afariki Dunia kwa ugonjwa wa Moyo hospitali ya Mzena jijini Dar

Status
Not open for further replies.
Kweli
View attachment 1724937

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Joseph Magufuli amefariki dunia.

Taarifa rasmi iliyotolewa kwa umma na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan kupitia Televisheni ya Taifa (TBC) leo usiku Machi 17, 2021 saa 5 usiku imeeeza kuwa Rais Magufuli amefariki dunia leo majira ya saa 12 jioni kwa maradhi ya Moyo akiwa katika Hospitali ya Mzena jijini Dar. Rais Magufuli alilazwa tarehe 6 Machi katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kwa tatizo la moyo wa mfumo wa umeme ambalo limekuwa likimkabili kwa takirbani miaka 10.

Nchi itakuwa katika kipindi cha maombolezo kwa siku 14 na bendera zitapepea nusu mlingoti

View attachment 1728353

View attachment 1728367

WASIFU:

Dkt, John Joseph Pombe Magufuli ni mwalimu na mtalaamu wa kemia akiwa na Shahada ya Uzamivu (PhD).

Kuzaliwa

Alizaliwa Oktoba 29 mwaka 1959 huko Chato mkoani Geita, Kaskazini magharibi mwa Tanzania.

Elimu

Magufuli alipata elimu ya msingi katika shule ya msingi Chato kuanzia mwaka 1967 hadi 1974.

Mwaka 1975 alijiunga na Seminary ya Katoke iliyo Biharamulo, Kagera kwa Elimu ya sekondari na kisha kujiunga na shule ya sekondari ya Lake iliyoko Mwanza hadi 1978 alipohitimu.

Mwaka 1979 alijiunga na shule ya Sekondari ya Upili ya Mkwawa, Iringa kwa ajili ya masomo ya kidato cha tano na sita na kuhitimu Mwaka 1981.

Mwaka 1981 hadi 1982 alisomea Stashahada (Diploma) ya Ualimu wa masomo ya Sayansi katika Chuo cha Ualimu cha Mkwawa, Iringa Masomo makuu yakiwa Kemia na Hisabati

Akiwa kazini, Magufuli aliamua kujiendeleza kwa kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) mwaka 1985 hadi 1988 alipotunukiwa Shahada ya Ualimu katika masomo ya Kemia na Hisabati.

Mwaka 1991 hadi 1994 alisomea Shahada ya Uzamili ya Kemia (Msc. Chemistry) katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Tanzania na Chuo Kikuu cha Salford, Uingereza

Mwaka 2009 alitunukiwa Shahada ya Uzamivu (PhD) ya Kemia kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

Mafunzo ya Kijeshi

Kati ya Mwaka 1983 na 1984, Magufuli alipitia mafunzo ya kijeshi kwa mujibu wa sheria kwenye Kambi za Jeshi la Kujenga Taifa Makutupora - Dodoma, Makuyuni - Arusha na Mpwapwa - Dodoma.

Kazi

Baada ya kufuzu Stashahada ya Ualimu, alifundisha masomo ya Hisabati (Mathematics) na Kemia (Chemistry) katika shule ya Sekondari Sengerema kuanzia mwaka 1983.

Baada ya hapo akafanya kazi kama Mkemia katika Chama cha Ushirika cha Nyanza huko Mwanza hadi mwaka 1995.

Siasa

Nyota ya Magufuli liana kung’aa katika siasa, alipogombea na kushinda ubunge eneo la Chato mwaka 1995. Mwaka huo huo aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Ujenzi, nafasi aliyohudumu hadi Mwaka 2000.

Baada ya uchaguzi Mwaka 2000, aliteuliwa kura Waziri wa Ujenzi, nafasi aliyohudumu hadi Mwaka 2006 alipohamishwa kwenda Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi alipokaa hadi Mwaka 2008.

Mwaka 2010, aliteuliwa kawa Waziri wa ujenzi kwa mara ya pili na kudumu kwenye nafasi hiyo hadi Mwaka 2015.

Urais

Mnamo Tarehe 12 Julai 2015, alichaguliwa kuwa mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Akiwa na Samia Suluhu Hassani kama mgombea mwenza.

Tarehe 29 Oktoba 2015 alitangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ushindi wa kura 8,882,935 sawa na 58.46%.

Magufuli aliapishwa kama Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 5 November 2015.

Muhula wa Pili

Mnamo tarehe 30 Oktoba 2020, Tume ya Uchaguzi Tanzania ilimtangaza John Pombe Magufuli kama rais kwa muhula wa pili kwa kupata kura milioni 12.5 hiyo ikiwa ni sawa na asilimia 84 akiwa amemshinda mshindani wake wa karibu, Tundu Lissu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) aliyepata kura milioni 1.9.

Baadhi ya Nukuu zake:

"Ni nafuu wakuchukie... uonekane wewe sio Mwanasiasa mzuri (Unpopular) kwasababu sikuja kutafuta Mchumba. Nimekuja Kufanya kazi za Watanzania." - Septemba 7, 2017

Soma pia: Nukuu toka kwa Rais Magufuli (QUOTES)

Baadhi ya Hotuba zake:

Hotuba ya Rais Magufuli kufungua Bunge la 12: Utumbuaji majipu utaendelea ili kuhakikisha Watumishi wanatenda kazi kwa mujibu wa Sheria na Kanuni - Novemba 13, 2020

Bungeni Dodoma: Rais Magufuli avunja Bunge la 11. Asema ajira 6,032,299 zimetengenezwa, Viwanda vipya 8,477 vimeanzishwa - Juni 16, 2020
Kweli kisasi aachiwe Mungu
View attachment 1724937

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Joseph Magufuli amefariki dunia.

Taarifa rasmi iliyotolewa kwa umma na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan kupitia Televisheni ya Taifa (TBC) leo usiku Machi 17, 2021 saa 5 usiku imeeleza kuwa Rais Magufuli amefariki dunia leo majira ya saa 12 jioni kwa maradhi ya Moyo akiwa katika Hospitali ya Mzena jijini Dar. Rais Magufuli alilazwa tarehe 6 Machi katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kwa tatizo la moyo wa mfumo wa umeme ambalo limekuwa likimkabili kwa takirbani miaka 10.

Nchi itakuwa katika kipindi cha maombolezo kwa siku 14 na bendera zitapepea nusu mlingoti

View attachment 1728353

WASIFU:

Dkt, John Joseph Pombe Magufuli ni mwalimu na mtalaamu wa kemia akiwa na Shahada ya Uzamivu (PhD).

Kuzaliwa

Alizaliwa Oktoba 29 mwaka 1959 huko Chato mkoani Geita, Kaskazini magharibi mwa Tanzania.

Elimu

Magufuli alipata elimu ya msingi katika shule ya msingi Chato kuanzia mwaka 1967 hadi 1974.

Mwaka 1975 alijiunga na Seminary ya Katoke iliyo Biharamulo, Kagera kwa Elimu ya sekondari na kisha kujiunga na shule ya sekondari ya Lake iliyoko Mwanza hadi 1978 alipohitimu.

Mwaka 1979 alijiunga na shule ya Sekondari ya Upili ya Mkwawa, Iringa kwa ajili ya masomo ya kidato cha tano na sita na kuhitimu Mwaka 1981.

Mwaka 1981 hadi 1982 alisomea Stashahada (Diploma) ya Ualimu wa masomo ya Sayansi katika Chuo cha Ualimu cha Mkwawa, Iringa Masomo makuu yakiwa Kemia na Hisabati

Akiwa kazini, Magufuli aliamua kujiendeleza kwa kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) mwaka 1985 hadi 1988 alipotunukiwa Shahada ya Ualimu katika masomo ya Kemia na Hisabati.

Mwaka 1991 hadi 1994 alisomea Shahada ya Uzamili ya Kemia (Msc. Chemistry) katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Tanzania na Chuo Kikuu cha Salford, Uingereza

Mwaka 2009 alitunukiwa Shahada ya Uzamivu (PhD) ya Kemia kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

Mafunzo ya Kijeshi

Kati ya Mwaka 1983 na 1984, Magufuli alipitia mafunzo ya kijeshi kwa mujibu wa sheria kwenye Kambi za Jeshi la Kujenga Taifa Makutupora - Dodoma, Makuyuni - Arusha na Mpwapwa - Dodoma.

Kazi

Baada ya kufuzu Stashahada ya Ualimu, alifundisha masomo ya Hisabati (Mathematics) na Kemia (Chemistry) katika shule ya Sekondari Sengerema kuanzia mwaka 1983.

Baada ya hapo akafanya kazi kama Mkemia katika Chama cha Ushirika cha Nyanza huko Mwanza hadi mwaka 1995.

Siasa

Nyota ya Magufuli liana kung’aa katika siasa, alipogombea na kushinda ubunge eneo la Chato mwaka 1995. Mwaka huo huo aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Ujenzi, nafasi aliyohudumu hadi Mwaka 2000.

Baada ya uchaguzi Mwaka 2000, aliteuliwa kura Waziri wa Ujenzi, nafasi aliyohudumu hadi Mwaka 2006 alipohamishwa kwenda Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi alipokaa hadi Mwaka 2008.

Mwaka 2010, aliteuliwa kawa Waziri wa ujenzi kwa mara ya pili na kudumu kwenye nafasi hiyo hadi Mwaka 2015.

Urais

Mnamo Tarehe 12 Julai 2015, alichaguliwa kuwa mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Akiwa na Samia Suluhu Hassani kama mgombea mwenza.

Tarehe 29 Oktoba 2015 alitangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ushindi wa kura 8,882,935 sawa na 58.46%.

Magufuli aliapishwa kama Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 5 November 2015.

Muhula wa Pili

Mnamo tarehe 30 Oktoba 2020, Tume ya Uchaguzi Tanzania ilimtangaza John Pombe Magufuli kama rais kwa muhula wa pili kwa kupata kura milioni 12.5 hiyo ikiwa ni sawa na asilimia 84 akiwa amemshinda mshindani wake wa karibu, Tundu Lissu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) aliyepata kura milioni 1.9.

Baadhi ya Nukuu zake:

"Ni nafuu wakuchukie... uonekane wewe sio Mwanasiasa mzuri (Unpopular) kwasababu sikuja kutafuta Mchumba. Nimekuja Kufanya kazi za Watanzania." - Septemba 7, 2017

Soma pia:

1) Nukuu toka kwa Rais Magufuli (QUOTES)

2) Magufuli: Kila atakayetaka kuiokoa nafsi yake atapoteza...

VIDEO:

Baadhi ya Hotuba zake:

Hotuba ya Rais Magufuli kufungua Bunge la 12: Utumbuaji majipu utaendelea ili kuhakikisha Watumishi wanatenda kazi kwa mujibu wa Sheria na Kanuni - Novemba 13, 2020

Bungeni Dodoma: Rais Magufuli avunja Bunge la 11. Asema ajira 6,032,299 zimetengenezwa, Viwanda vipya 8,477 vimeanzishwa - Juni 16, 2020

Ni kutokana na korona. Korona ikimpata mwenye maradhi mengine haponi.
 
Wanadamu ni wanafiki sana leo natafuta comment zenu sizioni.

Ila ndivyo ilivyo vitu vyema havidumu Mungu amlaze pema peponi.

Hakika rais Magufuli alikuwa mtu wa Mungu binafsi namfananisha na Mussa aliyetumwa kuwapeleka watanzania kwenye nchi ya matunda ,maziwa na asali.

Naamini Mungu hatatuacha wapweke bali atatuletea Joshua ambaye atatufikisha Tanzania kwenye nchi ya ahadi.

Amen!
Kweli alimuweka mbele sana Mungu na ndivyo inavyotakiwa kwa kila mwanadamu.Hata hivyo hii kwa Mungu mwenyewe anaweza kuiona ni kama dhihaka pale anaposhindwa kuwaweka mbele na wale wanaosimamia mipango ya Mungu duniani kama vile masheikh.
Kwa vile masheikh walikuwa na masononeko na dua zao za kichinichini hivyo ni rahisi Mungu kuwasikiliza na kumlaani yule anayewadhalilisha hata ikiwa kinywani kwake anamtukuza Mungu.
Moja ya adhabu Mungu aitoayo kwa aliyemlaani ni ugonjwa wa kiharusi....kushindwa kutoka ndani na kusema angalau kwa muda fulani.
 
Of course time heals everything. Mabaya yake tutasamehe na mazuri yake tutayaenzi.
We will tell our kids the story of his life and let them have their own opinions.
 
Kuna vita kubwa ndani ya maccm Mkuu ili huyu mama asichukue nafasi hiyo. Ngoja tusikilize itakuwaje huu mvutano.
Katiba inalazimisha Makamo achukue kiti hicho.
Kama kuna wana CCM wanahangaikia nafasi hiyo watateseka tu.
Na nadhani wazee wa chama hicho watakuwa upande wake.
Achana tuone
 
Kifo ni nini! naona mnakoment tu, kifo kinatisha jamani tumwombe MUNGU atupe amani na tuienzi kuongoza watu million sio kazi ndogo, Mwenyezi MUNGU akupeni wepesi tunaingia katika wakati mgumu watanzania, pumzikeni kwa amani marais wetu mliotuachia taifa nakutangulia katika umauti, mama janeth MUNGU akupe faraja wewe na watanzania wote
Kifo kinaumiza lakini kipo.
Ukiwa mwenye kukumbuka kifo mara kwa mara utawatendea wenzako yaliyo mema
 
R.I.P jembe tutakukumbuka sana tena sana maana ni mengi umeyafanya Mungu akupubguzie adhabu ya kaburi,[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
 
Nilivyoamka saa saba usiku nakutana na meseji ya mpenzi wangu kuwa magufuli amefariki.nikaingia instagram nakuta na hizi habari. Nikaingia JamiiForums.
Nikalog out kwanza.
Nikawa naingia kama guest user .
Sikukoment kitu mpaka asubuh ndo nimeanza kukoment.
Binafsi kama siamini vile.
Unazingua kwanini ulog out
 
Chadema hawana mamlaka juu ya kifo.walionena na kuandika hawakuandika kama chadema. Walitoa maoni yao na kuhabarisha umma juu ya yanayoendelea hata hivyo kutokana na chuki na ushabiki wa kijinga watu mkaanza kuishambulia chadema. Huu no ujinga uliopitiliza !!
Sasa kama ni hivyo kwann lisu kupigwa risasi akalaumiwa magufuli kwani yeye ndo alishika mtutu?
 
Apumzike kwa Amani

Kila jambo na wakati wake lakini yote hayawezi kututenga na upendo wa Mungu

Kuna wakati wa Furaha, huzuni, Mateso, Shida na Mahangaiko. Yote hayo tunayopitia hayawezi kututenga na upendo wa Mungu

Nitakulilia Mungu wangu daima wakati wa shida, Raha, Taabu na Furaha, Nitaziungama dhambi zangu daima mbele yako

Wote tupo safarini, Safari yetu ni moja na hapa Duniani tunapita

Tuishi kwa upendo, kusaidiana na kuombeana wakati wote bila kujali tofauti zetu za kimaisha, kisiasa au kiuchumi

Eee Bwana Tuhurumie, Tuhurumie tunajileta mbele yako kwani sisi ni wakosefu kwa mawazo, Maneno na vitendo, Tufanye kuwa watu wapya maishani mwetu kwa msamaha wako

Eee Bwana wewe ndie Wajua maisha yetu dakika moja ijayo, Hakuna yeyote ajuae kesho yake kama ataamka mzima au mfu

Tuhurumie sisi wakosefu, Tusamehe dhambi zetu

TAGA boy, porojo zako za humu bora umeziombea rehema.
 
Oh! Magufuli Umezima Ghaflna kama mshumaa kwenye upepo Mkali!!!
Watanzania walikuwa bado wanadhani tutakuwa pamoja ktk miaka hii 5 iliyo baki lkn wapi umetuacha tukiwa midomo wazi........oh...ohhh
umetuacha kwenye kiza kinene!!
machozi yanatutoka, nani atatusemea? nani atatutetea? nani ....nani?
nani atapaza sauti bila kigugumuzi kuwa tetea wanyonge?
wengi tulikuwa na matumaini makubwa ktk awamu yako hii ya pili ya miaka 5......
watanzania tumeumia sana sana.
Mbuyu umeanguka njia zote zimeziba hakuna pa kupita.
pumzika kwa Amani JPM.
Daima utabaki ktk vitabu vya historia ya Tanzania na Afrika kwa ujumla.
 
Mmvii yupo mtaani anapeta tuu, anawaangalia tuu na kuwacheka akina bashite na msukuma waliosema ikulu hakuna ambulance na hawaendi wagonjwa,,, kweli Mwenyezi Mungu hadhiakiwi!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom