Rais wetu Samia acha hotuba za kujitetea juu ya jinsia yako, wewe ni Rais siyo Rais mwanamke

Unajua kwanza haya maswala ya jinsia ni aina ya ubaguzi ambao mimi kwa namna nautazama hauna tofauti na ubaguzi wa rangi.

Hivi kuna haja gani ya kutaka kuonekana ni mwanamke au mwanaume katika kazi au sehemu yoyote tukiachia chooni.

Nadhani bado jamii yetu haijaweza kuelewa maana ya jinsia katika swala maendeleo. Na ndio maana wanawake wa sasa mbali na kupata fursa tofauti na wenzao wa miaka ya 1980's kurudi nyuma, bado Wanajiona wao ni underprivileged minority kumbe ni upuuzi mtupu.

Mimi huwa nachukia sana kampeni za kijinsia maana kwa Tanzania ukizungumzia maswala ya changamoto za jinsia then automatically watu wanahisi unawazungumzia wanawake. As if neno jinsia ni sawa na kusema mwanamke.

Ushamba ni mwingi sana eneo hilo, huwa sipendi hata kujihusisha mazungumzo yake....
 
Mkuu upo sahihi kabisa na kingine aangalie asije akafanya mambo ili aonekane bora kuliko wanaume,afanye kwa kadri ya ilani yao na utashi alojaliwa ,Hapo alipo amezungukwa na wanafiki ambao wanamuingiza mkenge
siku hadi siku
 
Tatizo, huko pia atakwenda kupewa support kama mwanamke. Nchi kama US siyo mfano mzuri maana nao bado wanaona ni ajabu m'ke kuwa kiongozi wa nchi. Ndo maana hata makamu wao alituma salamu maalumu, 'za kike.'
Nadhani wanafahamu weaknesses za mwanamke na hii kitu huwa nawaambia sana watu watazame.

Ukiona kuna jambo mzungu anakusisitiza sana ufanye ila yeye kwake hakitilii mkazo then jiandae siku za mbeleni huko kupata majanga.
 
Nijuavyo mambo ya sex yameshaleta taabu dunia hii. Siyo tu M and F siku hizi wapo akina transexual/transgender, gay.... nao wanataka watambuliwe siyo kwa mahusiano ya gender bali ya sex. Tusipoteze muda kujadili mambo ambayo hayajawa na nafasi ktk jamii yetu.
 

Mkuu umesema jambo la maana sana! Kama hakuna mtu amemwambia kuwa jinsia yake ni tatizo, hana haja ya kuzungumzia jinsia yake!! Ameonesha kuwa sexist na sasa ndio anaweza kuanzisha tatizo kwa kufikiria tu kuna tatizo. Nchi hii imekuwa na madiwani, wabunge, mawaziri na hata makamu wa Rais wanawake - hatuna ubaguzi wa kijinsia kiasi cha kuzungumzwa na kushadidiwa kiasi hiki.

Ninahisi ni yule Rais atasumbua wanaume kwa maneno kama “usinione mwanamke ukanidharau”! Hajui hata atakaposhindwa au kuweza hatapimwa kwa mzani wa jinsia bali utu/imani/tabia na taasisi yake tu!!
 
Rais kupewa support na mwanamke mwenzake siyo jambo baya maana kumbuka tupo kwenye mission ya Beijing.

Muhimu ni kuprove kuwa anaweza kufanya vizuri zaidi.
Udhaifu wa kupeana support kimakundi tunaujua na hauna msaada. Ndo maana hata mashuleni sasa hakuna haja ya kuwatenga wenye ulemavu, wanajichanganya na wengine. Kujitenga inawanyima nafasi ya kujiona wako sawa, wanaendelea kujiona wako tofauti. Ndo maana hata viti maaalumu Bungeni wengi wansubilia kupendelewa eti wana changamoto kumbe uzembe tu. Kuna watu wana PhD bado wanatafuta viti maalumu. Shit!
 
Nadhani anatuma ujumbe kwa kundi fulani huko huko juu. [emoji144]‍♀️[emoji144]‍♀️
 
Nimeanza kuona eti wanawake sasa wanataka kila nafasi idadi iwe sawa, badala ya kutafuta uwezo wao kama yeye Samia, sasa wanataka hata nafasi wasizokuwa na uwezo nazo. wanapigiana vigelegele; Yaani wapewe vitengo kwa kuwa tu kuna mwanamke ameweza kuwa rais. Wengine ndo hata tabia hazieleweki.

Tunataka mwanamke na mwanaume au kwa ujumla m-TZ anayeweza kuwa kiongozi na awe na tabia ya uongozi. siyo kupiga kelele ndo ajione yuko strong.
 
Bado hajiamini.
 
Nakubalina nawe katika hoja ya kwanza, lakini napingana nawe katika suala la Malkia Elizabeth, yule ni ceremonial leader hana majukumu makubwa ya kiserikali, mwenye majukumu ya kuongoza serikali ni waziri mkuu...so Malkia hana stress za kiongozi!
 
Nakubalina nawe katika hoja ya kwanza, lakini napingana nawe katika suala la Malkia Elizabeth, yule ni ceremonial leader hana majukumu makubwa ya kiserikali, mwenye majukumu ya kuongoza serikali ni waziri mkuu...so Malkia hana stress za kiongozi!
Ceremonial leadership siyo title ya muda mrefu sana
 
Hii nchi ni ngumu sana kuongozwa na mwanamke wa kariba yake.... Ataendeshwa sana na hii itamfanya aendelee kufanya maamuzi ya hovyo kama alivyofanya uteuzi wa DG wa Tume ya madini kumteua Janeth Reuben former Barrick HR Manager .. ndio maana JK anaonekana master mind. Kaacha manguli anaenda kuweka mtu wa rasilimali watu ...yetu macho sijui kama Buzwagi itafungwa.
 
Yeye sio Rais wa kwanza mwanamke hapa Duniani na hata kuwa wa mwisho,ajiamini japo najua ni kiwewe bado cha kuzoea madaraka makubwa confidence yake bado maana imekuwa ghafla
 
Ndo imeshatokea tu lakin kuna changamoto nyingi rais mwanamke., wakati akienda kujifungua nchi itakuwa kwenye likizo mpaka amalize siku 40, akiwa mja mzito nako pia ni changamoto kuna miezi fulani pale hataweza kuwajibika sawa sawa.
Ujauzito gani kwa umri wake ule mkuu
 
Au yule Makel (kama sijakosea) wa Ujerumani
 
Anachukua tahadhari juu ya mfumo dume!

PENGINE BAADA YA TAREHE 30/4 TUNAWEZA ONA MABADILIKO BAADA YA KUWA MWENYEKITI. HIVI SASA ANACHUKUA TAHADHARI NDIO MAANA ANAFICHA MAKUCHA!! PIA HUU NI MWEZI WA RAMADHANI KUHUTUBIA MCHANA NA SWAUMU SIO MCHEZO!!!
MAMA SAMIA HUU MWEZI MTUKUFU APUNGUZE KAZI ZENYE SHURUBA WAFANYE WASAIDIZI ZAIDI!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…