Rais wetu Samia acha hotuba za kujitetea juu ya jinsia yako, wewe ni Rais siyo Rais mwanamke

Hilo Si sawa kabisa Yeye ni Rais bila kujali jinsia Yake, na Yeye ana maono makubwa na uelewa mkubwa wa matatizo ya nchi na namna ya kuyatatua kushinda wanaume na viongozi walioko.
 
Akisema sana yeye ni rais mwanamke hata tuliokuwa tunasahau tunamuona rais tu tunakumbushwa kwamba yeye ni rais mwanamke.

Apige kazi tu, kila mtu anajua yeye mwanamke.

Au kuna mtu kasema Rais Sasha Fierce Queeen Bee ni mwanamme?
 
What is this?? Huu ni uzembe.
Kumbuka sheria nyingi za madini zilikuwa zinatungwa kwa sponsorship ya makampuni ya migodi, sasa tena huyu kamuleta mwajiliwa wa huko huko? Iliyokuwa TMAA kabla ya kuvunjwa ilijaa waliokuwa waajiliwa wa makampuni ya migodi, halafu yakawasukuma kuja TMAA kupitia kwa mafisadi kama Rostam na Ngereja, halafu tukategemea TMAA idhibiti utoroshwaji wa madini. Rais wetu anakurupuka sana kuhangaikia teuzi za kinamama.

Yupo yule mwingine kamuibua toka NGO eti awe mshauri wa uchumi! Tangu lini uchumi wa NGO ukaendesha serikali. Hapo niliona uelekeo wake kwa kuwa naye alikuwa huko huko kwenye NGO, akili haijabadilika kwamba hii sasa ni serikali. Tutasema tumpe muda lakini siku njema huonekana asubuhi.
 
Umemsahau Angela M. Yaani mwanamke shupavu kabisa. Hivyo na Rais wetu ni shupavu. Mpaka sasa hivi ni shupavu wetu. Apige kazi sisi tuko nyuma yake tuna msapoti hata moral tu siyo kwa vyeo jamaa yule juha alivyosema eti tunaomsifia na kumpongeza tunataka kazi. Shwetani yule angejua kuwa wengine hapa ni waajiri asingefungua mdomo. Mimi nimeajiri idadi kubwa ya Watanzania na sitaki cheo cha kupewa maana mimi ni boss wa kujitengeneza. Yaani mijitu mingine ni hovyo sana. Yaani kweli itawezekanaje kundi lote la wanaomsifia Mh. Rais awape kazi au kuwateua. Nonsense.
 
Hakika Mabeyo ndiyo mtu pekee ambaye mama asimuache. Wengine waliobaki atafakari sana.
 
mama anapoteza muda na mambo yake ya gender. sisi tunaiishi Katiba ya Jamhuri. she is a President of the Republic because of the Katiba na sisi tunaishi humo.
 
Mkuu umenikumbusha Specioza Kazibwe wa Uganda sijui kwa sasa yuko wapi huyu mama
Kuna watu muna uvivu wa kujisomea. Mazoea ya kupewa notisi hadi chuo kikuu. Tafuta hotuba za watu wafuatao walipokuwa ktk nafasi zao za juu:

Specioza Kazibwe wa Uganda
Joyce Banda wa Malawi
Ellen Johnson
 
Unaambiwa hivi ukikwaruzana na mtu halafu akakwambia usifikiri mimi naogopa huo urefu wako au hicho kitambi chako jua alishaona hicho ni kikwazo kwake kukushambulia.
 
Nadhani kutakuwa kuna kundi ndani ya system linalombeza Mh Rais wetu kuwa hawezi kwa sababu ni mwanamke.Maana ni wazi wananchi tumeonyesha kumkubali Rais wetu bila kuzingatia jinsia yake.Kutakuwa kuna power mongers zinamsakama mama kwa kigezo cha jinsia yake.
 
Wewe una theory mgando nani kakwambia mama pale hashiki mimba?

Unless were Sio mwafrika, it is taboo for an old lady to be breast feeding a small child at the same time as her siblings!!! Ndio maana nikakuita wewe MWANGA/MCHAWI KUFIKIRIA MAMBO KAMA HAYO!!!
 
Sa mbona mnaumia?
Binafsi siumii, lakini naona aibu kama itajaonekana kwamba rais wetu ni mama tu wa mtaani anayejivunia mambo ya hovyo. Kwani ungependa rais anayejivunia kalio kubwa au kujua kulitikisa?
Hujawahi pata aibu kwa matendo ya mwingine au hata usiyemfahamu? Hope una uelewa wa maana.
 
Sioni aibu kwa matendo ya mtu mwingine. Aibu ni zake mkuu
 
Well put, well said. Yeye achape kazi na hakuna anayehangaishwa na jinsia yake zaidi ya ithibati yake. Hata hivyo, si vibaya kuwaambia wananchi ukweli kuwa bado kuna wanaodhani kuwa mwanamke ni dhaifu. Nakubaliana naye kuwa mwanamke hajaumbika dhaifu zaidi ya mazingira yaliyomfinyanga na kumkandamiza. Tumpe nafasi afanye kazi badala ya kumshambulia. Kama wanaume tunasema kuwa 'kama wewe ni mwanaume' fanya kadha wa kadha, kuna kosa gani kwa mwanamke kuchora mstari mchangani au ni hofu ya kijinsia imeanza kuingia.
 
Anajiangusha na kujidharaulisha. Yupo too defensive. Hakuna anaedharau mwanamke ...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…