PreGE2025 Rasmi, Mahakama yapiga marufuku shughuli zote za CHADEMA

PreGE2025 Rasmi, Mahakama yapiga marufuku shughuli zote za CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Unakufa mda si mrefu kwa laana ya uliowateka
Hii ni hoja ya mtu aliyekata tamaa kwa maana kila mtu atakufa tu. Hata uwe mzuri kiasi cha kutokuwahi kukanyaga na kuua sisimizi, utakufa tu! Ila kwa Chadema, hiyo ni kwishnei! Ahahahahaha!!
 
Mimi always napenda kuona Upinzani ukiwa strong maana Upinzani ukiwa strong CCM tutakua strong zaidi tutaleta watu wanaokubalika na wenye huwezo kweli kweli wa kujenga hoja kutatua na kutatua kero za wananchi
 
Kutoka Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepigwa marufuku kufanya shughuli zozote zile za kiutendaji na oparesheni mpaka hapo kesi ya msingi iliyofunguliwa na aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Zanzibar Saidi Issa Mohamed na wenzake wawili (2) dhidi ya Baraza la Wadhamini na Katibu Mkuu wa CHADEMA itakaposikilizwa

Jaji Hamidu Mwanga anayesikiliza kesi hiyo namba 8323/2025 amesema zuio hilo la muda linakuja kufuatia maombi yaliyowasilishwa Mahakamani hapo na Mawakili wa waleta maombi wakiongozwa na Wakili Gido Thomas Simfukwe ambao waliiomba Mahakama kuweka zuio hilo hadi kesi ya msingi inayoanza kusikilizwa Juni 24.2025 isikilizwe, ambapo kwenye kesi ya msingi waleta maombi wanadai kuwa CHADEMA imekuwa ikiitenga Zanzibar katika masuala mbalimbali ikiwemo mgawanyo wa raslimali fedha nk

Akitangaza uamuzi huo, Jaji Mwanga amesema suala hilo ni la kisheria na haliitaji ubishani kwa sababu limefafanuliwa vyema kwenye sheria ya vyama vya siasa,

Wakati maamuzi hayo yanatolewa, upande wa utetezi (CHADEMA) haukuwa na mwakilishi yeyote Mahakamani, hiyo ni baada ya aliyekuwa Wakili wake Jebra Kambole kutangaza kujiondoa kwenye shauri hilo hatua iliyopelekea Mahakama kuendesha kesi kwa upande mmoja,

Kwa muktadha huo, ni wazi sasa shughuli za kisiasa za ndani (kiutendaji) na za oparesheni kama vile mikutano ya hadhara, vikao vya CHADEMA, vimezuiliwa kwa muda.




View attachment 3363251

Hii ndio picha ya Hakimu wa Mahakama Kuu Hamidu Mwanga aliyetoa uamuzi wa kuipiga CHADEMA marufuku

View attachment 3363259

Source: Jambo
Funking judge , fuckis justice
 
Kuna tofauti ya kesi ya jinai na madai. Mlaumu wakili wenu kwa kujitoa hivyo kesi kusikilizwa upande mmoja.Na kwenye kesi za madai hayo ni mambo ya kawaida.
Njama tu hizo
 
Ndio maana wamekupelekeni Mahakamani kwa huo ubaguzi wenu
Waliopelekwa mahakamani ni chadema kwa hakika watashinda hiyo kesi mapema tuu japokua ni kesi ambayo imeanzishwa ili kudhibiti mawimbi kwa mikono, suala ya ubaguzi wazanzibari ni wabaguzi kupita kiasi mimi kwa binafsi yangu siwapendi kama ambavyo wao hawa tupendi
 
huyo jamaa toka akiwa na mbowe ofisini sijawahi kumkubali,anaonekana tu kichwani hamna akili
 
Achaa ushamba wako akina lema mpka kutangazwa washindi baadhi ya wafuasi wa chadema walibaki vilema kwanza kupigania matokeo yasipindishwe
Halafu unajisemea kabisa ulikuwa unafanya kazi BOT kwa akili hizo kisoda labda ulikuwa mfagizi kitu kidg cha reforms ili uwanja uwe sawa umeshindwa kuelewa
hamna reform yoyote mnayopigania zaidi ya kutaka kuweka watu wenu wale ela, sasa BOT inahusiana nn na tone tone kijana? hamna mtu mwenye akili timamu ama umaskini unamsumbua atafuata agenda za watu waliovichaa
 
No Reforms No Election si kauli ya kupinga uchaguzi kwa utashi wa kisiasa bali ni wito wa haki na demokrasia ya kweli. Tunadai marekebisho ya msingi katika mfumo wa uchaguzi ili kuhakikisha kila kura ina thamani, na matokeo yanayoakisi sauti ya wananchi

#NoReformsNoElection
umeelewa nlichosema ama umeruka tone tone
 
umeelewa nlichosema ama umeruka tone tone
No Reforms No Election si kauli ya kupinga uchaguzi kwa utashi wa kisiasa bali ni wito wa haki na demokrasia ya kweli. Tunadai marekebisho ya msingi katika mfumo wa uchaguzi ili kuhakikisha kila kura ina thamani, na matokeo yanayoakisi sauti ya wananchi

#NoReformsNoElection
 
No Reforms No Election si kauli ya kupinga uchaguzi kwa utashi wa kisiasa bali ni wito wa haki na demokrasia ya kweli. Tunadai marekebisho ya msingi katika mfumo wa uchaguzi ili kuhakikisha kila kura ina thamani, na matokeo yanayoakisi sauti ya wananchi

#NoReformsNoElection
1749576986377.png


ukifika apa waambie wewe ni mwana kikundi wa tone tone, watakuruhusu bila kukuchangisha chochote
 
Back
Top Bottom