Rasmi: Mbwana Samatta asaini miaka minne na nusu Aston Villa

Hongera Samatta.

Ma shaa Allah, Allah akuzidishie kila heri kwako na kwa Uislam.

In shaa Allah kwanza kabisa uwe balozi mwema wa Uislam kwa vitendo vyema vya Kiislam.

Allah akuepushe na husda za walimwengu, akuepushe na fitna za makafiri. Allah akuepushe na vishawishi vya kishetani, Allah akuepushe na shari za wasiwasi zinazoletwa na watu na majinni waovu.

Aaaaaaamiiiiiiiiiiiiiiiiiiiin.
 
Dah Uislamu tena mpaka huku; si hayo tungekuwa tunayaacha kwenye vitabu vya yule mwenzetu wa Dola na Kanisa, halafu huku tuongee mpira tu? Huoni pia kuwa unamdhalilisha Samatta kwa kuwa ameajiriwa kwa furaha na waanglikana, tena mlezi wa timu yake mpya ni mwana mfalme (Prince William) ambaye ndiye mkuu wa kanisa la waangalikana?
 
Ma shaa Allah. Heri kubwaaaa hiyo.

Uislam hauna tatizo na kuajiriwa na Mkristo au yeyote yule mradi hakuzuii kuabudu - kumbuka hilo.

Sasa unataka nisimuombee dua njema?

Uislam usikutishe kijana ni mwema sana, hata wewe pengine ni Muislam lakini hujijui tu na haujuwi tu ni nini maana
ya Uislam.

Kwa kukujuza tu kuhusu Uislam unatufundisha nini kuhusu Wakristo soma hii...

Hakika utawakuta walio shadidi kuliko watu wote katika uadui kwa walio amini ni Mayahudi na washirikina. Na utawakuta walio karibu mno kwa mapenzi ni wale wanao sema: “Sisi ni Manasara.” (Al-Maidah Surah, 5:82)

Manasara = Wakristo.
 
Hashimu Thabit naye alitutangaza sana ..Wamarekani wengi walikuwa hawaijui Tanzania
 

Sitaki tujadili mambo ya dini hapa kwani dini nyingine ni sensitive sana wanapoambiwa mambo wasiyotaka kusikia. Kuna jamaa akiitwa Salman Rushdie aliwahi kuandika mambo kuhusu uislamu dunia ya uislamu ilirindima sana.

Kuhusu kuabudu kwenye mikataba ya ajira ni jambo la mtu binafsi siyo jambo la mwajiri. Kama anatakiwa mazoezini, lazima awepo, hawezi kuja na kisingizio cha nilikwenda kuabudu
 
Du hatari nani makafiri? hao wanaomlipa mshahara au huku mbagala. kwanza makafiri huwa hawana husda ni sisi tunaolala makanisani na misikitini ndio shida yetu.
 
Ni hatua nzuri sana nitakuwa nawaombea kushinda mechi zao ili wabaki EPL sababu mimi Liver na Villa sio wapinzani wetu nitawaombea kila mechi yao washinde wabaki katika league ndio muhimu kwa sasa na imani atasaidia team yake.
 
Bora sasa maana kila siku ilikuwa ni tetesi za kuwindwa tu na timu fulani.

Akomae sasa ili hata ikishuka uwezo wake binafsi umbakishe EPL.

Hongera kwake.
 
Hutaki kujadili "mambo ya dini hapa" wakati wewe ndiye uliyeanza mjadala? Kwa sababu tu FaizaFoxy kamuombea dua Muislam mwenzake aliyepata mafanikio, si ndiyo?

Salman Rushdie ukisoma kitabu chake utakuta hakuna zaidi ya matusi, kautukana Uislam, kamtukana Malkia wa Uingereza, kautukana Ukristo, sijuwi kama wewe kakubakisha. Lakini AlhamduliLlah Waislam pekee ndiyo waliothubutu kulikaripia hilo na kutoyakalia kimya matusi hayo.

Nnashangaa wale mliotukanwa halafu mkachekelea. Au kutukanana kikwenu ni kawaida? Kumbuka tu, Waislam hawamchelei yeyote ataeutukana Uislam na mitume yake.

Hatupigwi la kushoto sisi tukageuza na la kulia. Usisahau hilo, ingawa nakuona unaanza kwa mbali huku unajifanya siyo wewe. Kumbuka kuwa nipo na sipigiwi nnacheza seuse nikipigiwa?

Kimekuuma mimi kumuombea dua Samatta? Unanchekesha!
 
Nigrastratatract, Mkuuu yaani una msifia mwanadamu mwenzako kama vile unamtukuza mungu kuna walakini hapo hata kama ni ushabiki hii sasa too much mkuu sisi sote ni wanadamu tumeumbwa kwa mfanano mmoja na utofauti mdogo sana kama nitakukwaza samahani ila hupaswi kumsifia mwanadamu kiasi hiki kama vile ni mungu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni hatua nzuri sana nitakuwa nawaombea kushinda mechi zao ili wabaki EPL sababu mimi Liver na Villa sio wapinzani wetu nitawaombea kila mechi yao washinde wabaki katika league ndio muhimu kwa sasa na imani atasaidia team yake.
Ikitokea liver ikakumbana na villa utasimama upande upi ??
 
Aston Villa inafurahi kutangaza rasmi kumsaini Mbwana Samatta kutoka KRC Genk.Mshambuliaji huyo amemwaga wino kwenye mpango wa miaka minne unusu chini ya idhini ya kibali cha kazi na idhini ya kimataifa.

"Nimefurahi sana," Samatta alisema. "Ni hatua kubwa kwangu katika kazi yangu. Ni hatua kubwa kwa nchi yangu pia. Kila mtu alikuwa akitafuta Mtanzania kucheza kwenye Ligi Kuu za kimataifa hatimaye nimewatoa kimasomaso.

"Ninajua mengi juu ya Aston Villa. Nilikuwa nikitazama rekodi ya Ligi kuu wakati Gabby Agbonlahor alipokuwa hapa."
Mbwana Samatta amefunga mabao 10 kwa timu yake ya awali ya Genk katika mashindano yote msimu huu ikiwa ni pamoja na bao alilolifunga huko Anfield dhidi ya Liverpool kwenye Ligi ya Mabingwa.

Meneja wa villa Dean Smith alionesha furaha yake baada ya saini kuwekwa ."Nimefurahiya sana tumefanikiwa kumleta Mbwana Samatta klabuni,"

"Amefunga mabao katika kipindi chote cha kazi yake na ninatarajia kufanya kazi naye."

Samatta atakuwa Mtanzania wa kwanza kucheza kwenye Ligi Kuu lakini hataweza kushiriki kwenye mechi ya nyumbani ya Villa dhidi ya Watford Jumanne.

Villa wamecheza mechi zao tatu za mwisho bila mshambuliaji anayetambuliwa baada ya kumpoteza mchezeshaji wa mbele mwenye asili ya Brazil Wesley kwa msimu wote baada ya kupata jeraha la goti lililodumu huko Burnley Siku ya Mwaka Mpya.

Samatta ndiye mshindi wa tatu kwa timu ya Aston Villa kupata usajili wa dirisha la uhamisho kufuatia saini mbili za mkopo baada ya watangulizi wake kiungo wa kati Danny Drinkwater kutoka Chelsea na kipa Pepe Reina kutoka AC Milan.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…