Maisha ya kulelewa na mama ni mazuri kama akiwa nidhamu,hatukatai kuwa na mahusiano kwani kila mtu anayo,ila angalia wewe ni nani na mwanao anajifunza nini kupitia ww kubadilisha wanaume na yy anaona.
Monalisa yule pale ana watoto watatu,kila mmoja na baba yake lkn hushawahi kumuona ana wapost wanaume anao date nao,au kupigwa denda in public ? na unaweza ukakuta Monalisa anadate na wanaume wengi kuliko Kajala ila mambo yake hayanyi mbele watoto wake.
Kama anataka kujiachia ,ajiachie kama akimpata wanaume aliye tayari kupeleka mahali kwa mzee Masanja na wahalalishe mahusiano yao kwa ndoa,then ajiachie atakavyo na huyo mme wake na si kubadilisha wanaume mbele ya watoto wako.Kataa au kubali matendo ya mzazi yawe mazuri au mabaya mara nyingi ndiyo yanayo mjenga mtoto.
Hajachelewa kwa Paula,amnyang'anye simu,afute acc zake zote za social media na ampige marufuku ya kutumia simu.Ampeleke shule advance ambayo ina malezi mazuri na isiyo ruhusu kutumia simu na yeye mwenyewe awe na nidhamu la sivyo dogo atapotea mazima.