RC Amos Makalla hawezi hata kutoa hotuba!

RC Amos Makalla hawezi hata kutoa hotuba!

We si unasifia kila wanachokifanya wateule na marafiki wa mama, leo imekuwaje tena
 
Tangu ateuliwe kuwa RC wa mkoa wa DSM hajawahi kufanikiwa ktk jambo lolote lile

Mtangulizi wake alianzisha kampeni ya kupanda miti ya mapambo kwenye barabara zote na sehemu za njia panda (roundabouts) zilipambika kweli kweli. Lkn Amos Makalla amefika miti yote imekauka.

Amos Makalla aliazisha kampeni ya usafi wa jijini akaipa jina kabisa. Akateua mpk mabalozi wa usafi .Kampeni hii imekufa kifo cha mende.

Kichekesho kikubwa ni pale alipofanya maamuzi ya kukurupuka ya kukataza mabasi ya mikoani kushusha abiria kwenye stendi binafsi. Wenye mabasi wakamgomea.


Hebu sasa soma sehemu ya hotuba yake ya leo wakati akitoa salaam kama mkuu wa mkoa mwenyeji wa shughuli ya utiaji saini mradi wa SGR (Tabora -Kigoma) leo 20 December, 2022.
"Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla anazungumza:
Hali ya usalama ni shwari, nashukuru kwa Shilingi Bilioni 12.3 ulizotupa za kujenga madarasa 618, nikuhakikishe hakuna mtoto ambaye hatakwenda shule

Dar ndio Jiji la kibiashara, sisi ni wanufaika wa kwanza wa mradi wa SGR, hivi karibuni ulinipa fursa ya Kwenda kuifunza mambo ya usafi Rwanda, wanakushukuru kwa kufungua biashara.

Unayoyafanya yameandikwa kwenye ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi, chama cha siasa kazi yake ni kushika dola, unayoyafanya unatekeleza kile kilichopo kwenye ilani.

Ukishaona mtu mzima anacheza michezo ya kitoto kwa mfano ‘hide and see’ au kujipikilisha ujue mambo sio mazuri, juzi tumesikia wenzetu wanachagua Bunge la Mtandao, linaitwa Bunge na lina Spika, sasa hapo tunaona kabisa wanacheza mchezo wa hide and see, wamechanganyikiwa, hii ni kutokana na kazi nzuri unayofanya".


Hotuba hii imekaa kitoto Sana. Haina focus, anapuyanga huku kisha anahamie kule.

Hivi huyu RC wa hovyo kiasi hiki anabebwa na nani hadi kuwekwa kwenye huu mkoa ambao ndiyo uso wa nchi??
Wivu kwa mwanaume mwenzio haufai......aliepata kapata kama unajua ofisi zie si uende ukatoe ushauri.......watanzania mnafeli wapi???

Unajua kuna ma engn wazuri sana ma di ukiweka lugha yetu awapandishi sasa kama anafanya kazi we huioni nenda ofisini ukatoe ushauri na wala hana shda kumwona mkuu.........
 
Hahahaaaaaaa samehe mkuu
Chawa wana kazi na awamu hii hawataki kabisa chawa kwenye siasa wamehamia humu
Roho imekuuma? Unajuaje nimetoboa au la? Fahamu kuzaliwa tu mjini tayari una digrii...

Makalla kaingia CCM na kuanza harakati za kusaka ikulu chini ya wanamtandao hado kuwa mwekahazina wa CCM kipindi ambacho wewe ulikua bado unachambia vikopo vya kutu huko Chato.
 
Back
Top Bottom