RC Makala: Wafanyabiashara ndogo ndogo kupangwa upya Dar es Salaam, walioko barabarani kuondolewa

Naomba hili AGIZO liwe la nchi nzima. Maana hawa chinga hawana adabu. Kwenye njia za wenda kwa miguu wanapanga biashara zao, kwenye vituo vya kupumzikia abiria wao wamefanya ofisi zao na ukienda STAND za mabasi ndio balaa.
Stand ya MOROGORO imevurugwa na hawa binadamu. Ni uchafuzi kwenda mbele. Wafukuzwe kabisa na waonyeshwe maeneo yanayo wahusu.
 
Safi sana Makala..Kwa hili pongezi kubwa sana. Bado Mwanza..Wamachinga waliharibu maeneo mengi sana..Kuna haja ya kuweka uratibu mzuri kwenye hili tena tunakosa mapato mengi sana.
 
Leo nilipita seemu kwa machinga/wanyonge kucheki mtumba wa kiatu naambiwa 60k
 
Akifanikiwa katika hilo urudi umpongeze.
 
Safi sana Makala..Kwa hili pongezi kubwa sana. Bado Mwanza..Wamachinga waliharibu maeneo mengi sana..Kuna haja ya kuweka uratibu mzuri kwenye hili tena tunakosa mapato mengi sana.
sio huko tu mkuu. hiyo hali ni nchi nzima.
 
Kama ipo hivi basi ninauhakika yule wa Mwanza A.K.A mzee wa kukopy na kupest atalichukuwa hili aisee wanachafua mji sana hawa jamaa.
Yaan dah! Kwakweli wanahitaji wapangwe tuu
 
Kupitia biashara ya umachinga wale jamaa wengine pale Karume wanatengeneza faida ya 2000 tu kwa siku na wanaendesha familia.
 
Kama kunadhambi aisamehewi n wanaopokea pesa za HIZI MEZA pale MBEZI
ukifika kituoni unapotoka kwenda kimara kwenye lamii watu wamejaza MEZA BARABARANI na hakuna aliewahi kuwatoa

hii njia ikumbukwe na wanaoenda airport wanatumia

tunaomba kakayetu Mh Amosi
tusaidie kuwatafutia sehemu nyingine njia iwe wazi

zilemeza ikitokea garii imekosa break maafa yake yatabaki historia kwakweli

tuwalinde walendugu zetu waendelee kula mema ya nchi kwa kuwaondoa NJIANI wakakae sehemu salama
 
Subiri kwanza mkuu litokee semi imefeli break ikishachukua roho kadhaa ndio tutachukua hatua.

Sisi ndio tulivyo.
 
Kupitia biashara ya umachinga wale jamaa wengine pale Karume wanatengeneza faida ya 2000 tu kwa siku na wanaendesha familia.

Kuna machinga wengine wapo vizuri ,kuna mmoja yupo k/koo ana mjengo wa maana full fensi,msoth juu,aluminium window....ukiambiwa mjengo wa mmachinga unakataa.
 
Pale karibu na hospitali ya Regency Upanga wanapika chakula na kukaanga chips katikati ya transfoma kabisa
Hayati alikosa exposure hakuna mji duniani uko ovyo kama dar,mamalishe anapikia kuni chini ya transfoma pembeni kuna bank mbele kuna jengo la ubalozi.Mungu fundi

nda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…