RC Makala: Wafanyabiashara ndogo ndogo kupangwa upya Dar es Salaam, walioko barabarani kuondolewa

RC Makala: Wafanyabiashara ndogo ndogo kupangwa upya Dar es Salaam, walioko barabarani kuondolewa

Leo RC Makalla amekaa na madiwani kuwaelezea nia yake ya kuwapanga upya wamachinga ktk jiji hili la kibiashara

Chanzo: ITV habari

Wamachinga walipewa Uhuru usiyokuwa na mipanga kiasi kwamba waligeuka kuwa kero kwa kila mtu.

Uamuzi wa RC Makalla uungwe mkono ili hawa wanyonge wafuate utaratibu. Na wawe na maeneo maalumu ya kufanyia kazi zao. Wasizagae hovyo.
Naunga mkono hoja
 
Hayati alikosa exposure hakuna mji duniani uko ovyo kama dar,mamalishe anapikia kuni chini ya transfoma pembeni kuna bank mbele kuna jengo la ubalozi.Mungu fundi
Dar ingekuwa jiji la mfano hata sisi tukiingia tujisikie kuwa Tanzania kuna mji mzuri. Sasa hivi huko Buguruni, Ubungo, Karume, Tegeta hapana tofauti na Lindi
 
Kuna machinga wamejenga mabanda yaani utadhani maduka ya nguo baadhi ya maeneo, leo hapo ubungo darajani upande wa msikiti nimekuta ugomvi jioni hii mtembea kwa miguu amekanyaga Nyanya daah nimeacha timbwili hapo.....wamepanga service road yote.
Bara bara ya Sam Nujoma ni uchafu mtupu. Kweli watu wanatafuta Liziki lakini si kwa mrundikano ule
 
Siyo hivyo tuuu yaani imefika mahali Mamalishe wanapikia kuni karibu na sheli...

Mwendazake aliwalemaza sana hawa watu et nao wanakubali kujiita wanyonge. Leo hii kuna wapumbavu hawa wajasiliamali wamejazana sana pale kona ya gerezani wanauza maji ya kunywa wanaokota makopo wanajaza mpaka juu chupa ya jambo ina kizibo cha mirinda, hayo maji waliko chota wanajua wenyewe yana usalama gani.. basi tu ilimradi nao ni machinga na wanaambiwa wasibugudhiwe, ndo watunyweshe maji machafu ???

Hii nchi mi na mlaumu sana Nyerere aliwafukuza wazungu mapema sana, ilitakiwa tuendelee kutandikwa viboko mpaka miaka ya 2005 tupewe uhuru tungestaarabika sana ona nchi kama South Africa wamepata uhuru 93 kwa viboko na wamenyooka hata kama baadh yao ni maskin ila maskini walio staarabika.
Mungu a
Dar ingekuwa jiji la mfano hata sisi tukiingia tujisikie kuwa Tanzania kuna mji mzuri. Sasa hivi huko Buguruni, Ubungo, Karume, Tegeta hapana tofauti na Lindi
Yule mzee alikuwa ovyo kabisa
 
Huwa tunatengeneza matatizo na kuja kuyatatua, kifupi tunaenda mbele na kurudi nyuma kila uchwao...kesho atakuja mwingine mtetezi wa wanyonge atasema fanya biashara kila mahala...
 
Hii ingefanyika Tanzania nzima.Hawa wapangishe frame ya duka,ili kuingiza mapato ya serekali kwenye kodi ya zuio(with holding Tax)Frem nyingi kwenye miji,zimejengwa,hazina wapangaji,wakipatikana wapangaji na kodi ya zuio,imepatikana.Wengi wanaingiza faida kubwa,lakini hawalipi kodi.
Mkuu ni kweli frame ziko nyingi na hazina wapangaji hivyo jiji liwatake wamachinga wakapange. Tatizo la wamac hinga wengi hawataki kulipa kodi za frame na kodi ya Serikali wao ni faida tu.
 
Hahahaaaa........machinga ni jeshi kubwa bwashee!
Acha propaganda mkuu, hakuna nchi isiyokuwa na utaratibu.
Leo hii unaweza kutamani kuishi Ulaya kwa sababu watu wa Ulaya wana utaratibu, unaenda kuuza machungwa geti la Ikulu au kupanga viazi kando ya barabara ya mjini katikati it's nonsense ina maana watu wa mipango miji walisoma wrong Profession?

Acheni siasa za maji taka kama kweli mna nia ya kuitoa hii nchi hapa ilipo kwenye ujinga na ushabiki wa kutuliza njaa zenu
 
Huo ujinga upo had mikoani..barabara mbili moja inafinywa watu wanapanga meza
Tusiwalaumu tu wamachinga, mpaka mmachinga anafinya barabara kwa ajili ya biashara zake mamlaka husika ipo wapi?
Ukipita kwenye lango la chuo cha IFM na Wizara ya Afya ni aibu
Naona hata wale ndege wa nyumba nyeupe TAUSI hawana sehemu ya kuvijari kama zamani.
 
Siasa ndiyo imechangia kuliharibu jiji..wanasiasa wenye mawazo muflisi kama haya ndio wamesababisha jiji limekuwa la vibanda kile sehemu. Huwezi kutofautisha manzese na posta. Na hii imezagaa maeneo yote,...Mwanza kule ndio kabisa hata gari haliwezi kupita.

Arusha pia, yaani nchi nzima. Hili liwe tamko la Waziri Tamisemi kwa nchi nzima.
 
Hili la wamachinga ni time bomb
Rais Samia asiliendee kichwakichwa, litamuondolea kuaminika na kuungwa mkono na maelfu ya wamachinga akiliendea kwa pupa

Hakuna short term solution kwenye ishu ya wamachinga, linahitaji bajeti, ujenzi wa miundo mbinu ya kuwaaccomodate n. k

Isitoshe, Wamachinga walihakikishiwa na serikali kutosumbuliwa, Sasa Samia atimize ilani na ahadi waliyoitoa kwa wamachina mwaka 2020, la sivyo hii ni hadaa.

Serikali ya Magufuli ambayo Samia alikuwa makamu wake iliwahakikishia Wamachinga kutowasumbua, na hadi 20000 za vitambulisho ikawatoza, Sasa iweje awageuke? —Hii itamsumbua sana Samia, It is a political gamble akifanya hili KWA SASA BILA MIUNDO MBINU YA KUWAACCOMODATE WAMACHINGA

Tuchague moja, kile tunachokiita uchafu wa Machinga, au jeshi la vijana lililokata tamaa kwa kushindwa kujiajiri.
 
Back
Top Bottom