Refa Martin Saanya adaiwa kuwabeba Simba kwenye mechi dhidi ya Geita Gold

Refa Martin Saanya adaiwa kuwabeba Simba kwenye mechi dhidi ya Geita Gold

Nini Kimetokea? Kuna Watu wamechoka Kupumuliwa Kisogoni?
Haya sasa Hamtapumuliwa tena, Baada ya 11 Dec Baskeli yenu Ya Miti Itakuwa Imehitimisha Kazi Yake na Mtarudi Kwenye Nafasi Yenu Mnayostahili.....!
Ili nyie mupumuliwe kisogoni si ndio?
 
.
IMG-20211202-WA0000.jpg


Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Jana kulikuwa na mtanange baina ya Simba na Geita Gold. Kwa kweli niwasifu sana vijana wa Geita Gold walivyowapeleka puta wachezaji wa Simba. Kwa hakika Geita Gold walicheza vizuri kuliko Simba.

Kinachonisikitisha ni kuwa goli la wazi la kusawazisha lilikataliwa na refa kuwa mfungaji alimsukuma Shomari Kapombe. Tukio hilo lilirudiwa mara nyingi na mfungaji kamwe hakumsukuma Shomari Kapombe.

Kwa kweli inauma sana ukichukulia kuwa Geita Gold bado ni timu changa. Nawashauri TFF iwachukulie hatua aina ya marefa kama yule wa jana.
 
Na evidence nimekuwekea


Mchezaji anahojiwa hapa anasema nilimgusa kidogo...😁😁😁😁ndio ushamgusa ivyo

IMG-20211202-WA0045.jpg
 

Attachments

  • VID-20211202-WA0043.mp4
    565.5 KB
Na evidence nimekuwekea


Mchezaji anahojiwa hapa anasema nilimgusa kidogo...[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]ndio ushamgusa ivyo

View attachment 2030659
Yaani mtu usukumwe kwenda mbele ukiwa chini halafu utumie msukumo huo kuruka juu na mikono yote juu kama unacheza Get up stand up ya Bob?
 
Jana kulikuwa na mtanange baina ya Simba na Geita Gold. Kwa kweli niwasifu sana vijana wa Geita Gold walivyowapeleka puta wachezaji wa Simba. Kwa hakika Geita Gold walicheza vizuri kuliko Simba. Kinachonisikitisha ni kuwa goli la wazi la kusawazisha lilikataliwa na refa kuwa mfungaji alimsukuma Shomari Kapombe. Tukio hilo lilirudiwa mara nyingi na mfungaji kamwe hakumsukuma Shomari Kapombe. Kwa kweli inauma sana ukichukulia kuwa Geita Gold bado ni timu changa. Nawashauri TFF iwachukulie hatua aina ya marefa kama yule wa jana.
Uku siyo mahara pake peleka kwenye MMichezo na Burdani kama ungekuwa wewe ungefanya je?
 
Marefa wanaharibu mpira wa Tanzania, tuchujue hatua kabla mambo hayajaharibika kabisa.
 
Simba ndiyo inaifanya ligi ya NBC msimu huu chini ya tff ya karia kuwa ‘most corrupted league’ kwenye sayari hii na sijui ni kwanini NBC wamejiingiza kudhamini wizi na ifisadi kama huu,
 
Mpira ili unoge ni lazima uwe na mistake ndo maana hata waliotengeneza game la FIFA wamelitengeneza kuwe na zile mistake za kibinadam unaweza ukawa on side lakin ikapigwa filimbi ya offside lakin hata ikirudiwa inaonekana ulikua onside
Kama ni mpenzi wa playstation utakua unakutana na hivyo vtu PS4
Kwahyo ili mpira unoge ni lazima makosa ya kibinadam yawepo
 
Unajua lazima utafiti ufanyike ili tuweze kubaini hivi ni kweli marefa hufanya makosa kwenye mechi zinazozihusu Simba na Yanga tu. Au kwa sababu ndio mechi tunazozifuatilia zaidi ndio maana tunapiga kelele. Hv huwa mnafuatilia vizuri mechi zinazozihusisha timu ndogo kama KMC na Mbeya city mkaona madhaifu ya marefa pia au mnafuatilia timu pendwa zenu tu. Yanga kapewa penalty dhidi ya Namungo, washabiki wa Simba walitokwa povu kweli na Yanga hawakuona tatzo zaidi ya kuchekelea... Jana shilling imejeuka Simba naye kaambulia mbeleko Yanga leo povu mpaka linamwajika. Soka letu huwa tunasema linaangushwa kwa sababu ya Simba na Yanga lakini naongezea hapohapo kuwa soka letu linaangushwa na mashabiki wa Simba na Yanga.
 
Back
Top Bottom