Ripoti ya CAG 2021-2022: Rais Samia ataka baadhi ya mashirika yasiyo na tija kufutwa

Dah maza Hana hata meno maskini anaongea kama mtu aliyejikatia tamaa,eti mtu ana mikopo mi5 afu kasepa,kwani Maafisa waloshuhulikia hiyo mikopo si wapo?haya hili nalo wakalitazame 🤣🏃
 
TRC isifutwe bali atafutwe mwendeshaji, ikiwezekana kampuni ya nje ya nchi. Watumishi wa Serikali jawana kabisa weledi wa biashara au uchumi.
Hatujakoma kwa yaliyotokea kwa wahindi? Mwekezaji aliklchukua spare part hadi vichwa vya tremi akapeleka kwao
 
Hata hivyo ni sawa maana kama ATCl haijawahi kua na faidi lakini private companies wanapambana ivo ivo, so tatizi ni ile kasumba ya mali ya serikali ndo inafanya watu wawe wazembe na wapigaji.... na hatabkuwapa wazungu waendeshe bado watabanwa tuu na wahuni kwakua watajua nanmna ya kuwawajibisha wasipotekeleza intrest zao
 
Baada ya ripoti ya CAG Kutolewa na kueleza madudu ya GPSA, Rais Samia Hassan amependekeza taasisi hiyo ya umma ifutwe au iundwe upya.

Kwa kauli hii ya Rais bila shaka huu ni uamuzi kamili wa kuizika rasmi GPSA .
 
Wamemtuma kijana wao neppie ili kuua ttcl wameona haitoshi. Hivi kusema ttcl wana mkongo eti hakuna ushindani sawa, hapo ni suala la hasara kwa shirika la ttcl au ni kukingia kampuni binafsi ushindani. Kwani serikali kukusanya kodi toka raia ni biashara? Kazi ya kodi ni nini kama sio pia kuendesha mashirika ya huduma muhimu kwa faida ya jamii. Kwa nini waone uchungu shirika kama ttcl likitoa huduma kwa bei nafuu kwa raia. Halafu ujue huyu mama hakuna kitu anajua. NDC ni shirika la biashara? Au hajui kazi ya NDC? Wanaacha kusimamia uadilifu na tija badala yake wanalihujumu ttcl kwa maslahi yao kwenye mashirika binafsi. Mtu kama magufuli asiye na mawaa alitoa nguvu yake kuimarisha ttcl sasa wahuni wameingia kutaka kuliua shirika.
 
Ifike muda mheshimiwa rais aruhusu mchakato wa katiba mpya uendelee ili tupate viongozi kutoka vyama vyote vya siasa.
Viongozi wengi wa CCM ndio wezi wa mali za watanzania maskini.
Halafu utasikia waziri fulani anasema "tuwe wazalendo".
Na wengine wanavaa tai na suti zenye rangi ya bendera ya Taifa.

Inauma sana.
 
Hata serikali ikiwemo Ikulu ikifanyiwa tathmini tunaweza kuja na pendekezo ivunjwe kwa kukosa tija.
Nataka kufanya comment kama ya kwako .naona hata ikulu ibinafsishwe tu jamani maana hatuwezi kuwa na rais asiyekuwa na tija wala kuumiza kichwa kujua changamoto ni ipi kitu kikiienda ndivyo si vyo tunakimbilia ubinafsishaji kama shortcut
 
Mambo mengine Serikali yetu iwe inajifikiria,hivi unawezaje kukuza uchumi bila njia za Reli.wewe kama Serikali kwa nini usisimamie mpaka hiyo TRC itengeneze faida.
Watawala wanapenda sana shortcut yaani kitu kikishindikana na kikaaenda ndivyo sivyo solution ni ubinafsishaji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…