Ripoti ya CAG imefichua madudu mengi ya awamu ya tano, kulikuwa na ufisadi wa kutisha

Yaan hapa ndipo ninapowanyooshea CCM wanaharibu then wanatwambia walichoharibu kwa kujiegemeza kwa Rais(mtu) ili kutengeneza Imani kwa chama na aliyepo madarakani. Nae ataharibu watakuja kusema ili tumwamini aliyesema n.k na wananchi tunakubali tu. Nyerere alifanya, wakaja kumbeza kupitia mwinyi, nae akaharibu, mkapa akaharibu, kikwete usiseme, magu nae Kama mnavyosikia. Na ujanja wa CCM ni kuhakikisha wao ndio wanaibua madudu mengi ili kumpa credibility aliyepo madarakani. Kwa kifupi CCM anajigeuza kwa wananchi kwa kuwa mpinzani wa aliyoyafanya anavyoona kuna faida ya kufanya hivyo kwa wananchi na wananchi nao wanajaa. Wakijaa anarudi kuwa mtawala na anaharibu tena yaan ni mwendelezo. So everything is f*ucked.
 
Hakuna kitu hapo. Hizi ni mbinu za kuwafanya watu wamsahau SHUJAA.
Wanaona Power yake bado imejaa mioyoni mwa watu, kwa hiyo njia pekee ni kuonesha kana kwamba SHUJAA hakuiweza kazi.
Kwa kutumia akili ndogo kabisa, kama kulikuwa na ubadhirifu huo, aliwezaje:-
(1)Kujenga Ikulu na kuhamia Dodoma ndani ya miaka 5?
(2)Kuifikisha Nchi uchumi wa kati ndani ya miaka 5?
(3)Kuanza kujenga Bwawa la umeme la Mwalimu Nyerere ndani ya miaka 5?
(4)Kuanza Kujenga SGR ndani ya miaka 5?
(5) Kujenga Flyovers kwa miaka 5?
(6)Kununua ndege hizo kwa miaka 5?
Hayo ni machache tu kati ya mengi aliyoyafanya kwa muda mfupi kabisa na ikumbukwe kuwa, Watangulizi wake wote hawakuweza kufanya hata moja kati ya hayo kwa miaka yote 10 waliyokaa madarakani. Kwa sababu hayupo, ndo yanaibuka hayo. Kwa vyovyote vile ilivyo au itakavyokuwa,
Ukweli utabaki pale pale kuwa, JPM alikuwa SHUJAA.
 
Tatizo lipo kwa wakuu wa Idara husika, na viongozi wenye wajibu wa kusimamia Matumizi ya fedha za serikali.
wahusika ktk ubadhirifu au matumizi mabaya ya fedha za serikali wachukuliwe hatua bila kuoneana aibu.

kuleana na kuoneana aibu ndio kutaiangamiza taifa letu, hatua kali zichukuliwe.

Hata Hayati JPM ange kuwa haki ange chukua hatua kali vivo hivyo tunategemea kwa Rais wetu Mama Samia atachukua hatua kali kwa kila idara na viongozi wake.
 
hiyo bil 60 ni 2019/2020. miaka mitano back ina loss kubwa kuliko hiyo
 
Nafahamu
Kwani hizi report si huwakilishwa hivi kila mwaka?
Mkuu usipoteze muda kujadiliana na watu ambao hawana uelewa mpana wa na masuala ya auditing ,wengi wao humu ndani hawana uelewa mpana na masula ukaguzi, hawawezi kutofautisha kati ya hoja za ukaguzi na wizi, hawajui kwamba CAG ana mamlaka ya kuagiza mtuhumiwa kukamatwa endapo Kuna ubadhilifu umetokea vinginevyo zinabaki kuwa hoja Kama hoja nyingine.
 
No body anataka kuchafua image yake.
and to be honestly kila mtu anajua kazi alio ifanya. yanaonekana kwa macho.

lakin lila shilling ina pande mbili. upande mwingine ndio huo kama report ya CAG inavyosema.

JPM hakuwa mkamilifu.
 
Mkuu wasamehe bure hawana wanashindwa kutofautisha kati ya hoja za ukaguzi na wizi.

Hoja hizi huibuliwa na CAG huzifuta zile ambazo hukosa majibu kwa miaka 3 mfululizo CAG au bunge huagiza vyombo vingine vya Serikali Kama vile TISS ,PCCB POLICE kuchukua hatua .
 

Tatizo letu ni mfumo wa uendeshaji serikali na uwajibikaji, kudhibiti mapato na matumizi

Suluhu ni katiba mpya, ile ilopita kwa raia na kuithibitisha.

Kama tunataka mabadiliko tuanzie hapo.
 
viongozi wa hii nchi hata siwaelewagi Kama kweli wamesoma au laa,maana hata wao wanajishangaa.
Ni wapuuzi tu
 
Io ni loss ya mwaka mmoja acha kupotosha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…