Jamaa hawajui hata kufanya uchambuzi wa report ya CAG wanaendeshwa na ushabiki.Hakuna fedha iliyoibwa labda kama hujui kusoma vizuri
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Jamaa hawajui hata kufanya uchambuzi wa report ya CAG wanaendeshwa na ushabiki.Hakuna fedha iliyoibwa labda kama hujui kusoma vizuri
Jifunze Break Even Point utajua faida inavyoliwa na running cost kwenye biashara mpya...
Angalia mchoro wa BEP
View attachment 1746810
zilikuwa siasa tu. atcl imekuwa iki make hasara way long. sasa ili kulinda image ya mzee.. ilibidi wamsifia sana, hata kutengeneza hela ya gawio ambalo halipo.Hivi kwann tulianimishwa atcl inapata faida wakati sio kweli?
hiyo bil 60 ni 2019/2020. miaka mitano back ina loss kubwa kuliko hiyoHumu 80% ni blabla tu hakuna facts ya maana, ATCL ni loss ya bil 60 kwa miaka mitano, ni loss sio wizi, uendeshaji wa shirika lenyewe, takribani mashirika yote yamekula loss, suali lingekuwa je pamoja na loss ya mashirika yote haya mbona bado wanaendelea na biashara hiyo?.
Mkuu usipoteze muda kujadiliana na watu ambao hawana uelewa mpana wa na masuala ya auditing ,wengi wao humu ndani hawana uelewa mpana na masula ukaguzi, hawawezi kutofautisha kati ya hoja za ukaguzi na wizi, hawajui kwamba CAG ana mamlaka ya kuagiza mtuhumiwa kukamatwa endapo Kuna ubadhilifu umetokea vinginevyo zinabaki kuwa hoja Kama hoja nyingine.Nafahamu
Kwani hizi report si huwakilishwa hivi kila mwaka?
No body anataka kuchafua image yake.Hakuna kitu hapo. Hizi ni mbinu za kuwafanya watu wamsahau SHUJAA.
Wanaona Power yake bado imejaa mioyoni mwa watu, kwa hiyo njia pekee ni kuonesha kana kwamba SHUJAA hakuiweza kazi.
Kwa kutumia akili ndogo kabisa, kama kulikuwa na ubadhirifu huo, aliwezaje:-
(1)Kujenga Ikulu na kuhamia Dodoma ndani ya miaka 5?
(2)Kuifikisha Nchi uchumi wa kati ndani ya miaka 5?
(3)Kuanza kujenga Bwawa la umeme la Mwalimu Nyerere ndani ya miaka 5?
(4)Kuanza Kujenga SGR ndani ya miaka 5?
(5) Kujenga Flyovers kwa miaka 5?
(6)Kununua ndege hizo kwa miaka 5?
Hayo ni machache tu kati ya mengi aliyoyafanya kwa muda mfupi kabisa na ikumbukwe kuwa, Watangulizi wake wote hawakuweza kufanya hata moja kati ya hayo kwa miaka yote 10 waliyokaa madarakani. Kwa sababu hayupo, ndo yanaibuka hayo. Kwa vyovyote vile ilivyo au itakavyokuwa,
Ukweli utabaki pale pale kuwa, JPM alikuwa SHUJAA.
Mkuu wasamehe bure hawana wanashindwa kutofautisha kati ya hoja za ukaguzi na wizi.Wengi wanaopiga debe kudai "madudu" yamefichuliwa hawajawahi kusoma ripoti za CAG, wanadakia ya kusikia tu. Kopi za hii ripoti ya mwaka huu mimi sijaiona, lakini nilishasoma za kila mwaka kwa miaka 11 iliyopita tangu waanze kuziweka mtandani. Utashangaa ukija kusoma hii ukakuta ni sawa kabisa na zile za zamani. Hati chafu ni kama 5% au chini ya hapo kwa nchi nzima.
Shida yetu kubwa ni kwamba tunapojadili haya mambo hatuji na masuluhisho. Na kila mwaka ni yale yale. Upigaji wa kutisha!
Kama jamii tufanye nini ili kuikomesha hali hii? Tunawezaje kuukomesha ufisadi? Kwa nini viongozi wetu wanakuwa hivi? Tufanye nini?
Mwendazake keshalala. Hata tukipopoa mawe na kucharaza bakora kaburi lake hatatusikia. Kimbembe ni kwetu tuliobakia. Ni kweli hatuwezi
Siku ya leo sijui tuuiteje huko; Mbaya? Au nzuri sana?
Ripoti ya mkaguzi mkuu wa serikali inayoendelea kusomwa muda huu si kwamba tu inawaweka CCM na watetezi wa mwendazake kwenye wakati mgumu sana, lakini tayari imechefua wananchi wengi kwa kiwango kisichomithilika.
Madudu ya SHUJAA WA AFRIKA yanatisha na kutia kinyaa.
Madudu ya MTETEZI WA WANYONGE Yanatia hasira sana.
Chukulia hili moja BILIONI 3.9 kwenye matengenezo ya ndege moja ambayo HAIKUFAA![emoji3064][emoji3064][emoji3064][emoji3064]
Upinzani uliwahi kusema upigaji wa awamu hii utavunja rekodi, watu wakabeza sana. Lakini wakati ni hakimu mzuri. Uongo hupanda lift lakini ukweli hukwea ngazi. Mahakama ya mafisadi inaweza kuanzia pale kwenye nyumba ya milele ya mwendaAzakwe marehemu hayati.
Huu uozo uliendelea kuwekwa wazi peupe hivi tusishangae kuona siku moja marehemu akalikimbia kaburi lake. N itokee kuna kitu kinaitwa maandamano kifanyike[emoji848][emoji848][emoji848] Bila udhibiti imara si ajabu kuwakuta waandamanaji wakilicharaza bakora kaburi la shujaa wa Afrika na kuipopoa mawe picha yake.
Baada ya kusomwa hii ripoti, masikio yote yako kwa Bimkubwa. Je, atasemaje? Watu wamefura kwa hasira. I hope hatawazingua
Mahabusu ziandaliwe za kutosha sasa. Ni zamu ya kubadilisha wapangaji. Karibia kila wizara ina vimeo vya kutisha.
Io ni loss ya mwaka mmoja acha kupotoshaHumu 80% ni blabla tu hakuna facts ya maana, ATCL ni loss ya bil 60 kwa miaka mitano, ni loss sio wizi, uendeshaji wa shirika lenyewe, takribani mashirika yote yamekula loss, suali lingekuwa je pamoja na loss ya mashirika yote haya mbona bado wanaendelea na biashara hiyo?.