Ripoti ya CAG imefichua madudu mengi ya awamu ya tano, kulikuwa na ufisadi wa kutisha

Una moyo sana kupambana kuhalalisha haya ya awamu ya tano
Kama wewe ulivyo na moyo wa kuchafua kila kilichofanyika awamu ya tano

Tulia tusubiri hati safi na chafu watu wawajibike na kuwajibishwa
 
Inabidi upambane sana. Image ya mwendazake inachafuka kwa kasi ya mwanga

hakuna mwenye uwezo huo.

mwendazake anachafuka jukwaa la siasa jamiiforus.

amini nakwambia,atatakata hapa hapa jf siasani mwakani tu mwezi kama huu.
 

afadhali wewe umetumia akili.

hata tunawezakuwa na logic tukihoji kwa namna hii.
 
Kama wewe ulivyo na moyo wa kuchafua kila kilichofanyika awamu ya tano
1. Si mimi ninayeichafua awamu ya tano, ni ripoti ya CAG
2. Si kila kilichofanyika katika awamu ya tano, madudu yametajwa kila moja kwenye eneo lake
 
Mbona haya madudu yanaonekana ni mengi awamu ya tano kuliko hata wakati wa awamu ya nne tuliyodhani ni awamu ya upigaji .....!!

hukutakiwa kudhani awamu ya nne ni ya wapigaji,ilikuwa ni ya wapigaji kweli kweli.na ndio wako mbioni kurudi sasa.
 
Magu na azidi kulaaniwa hko aliko, sijui hii nchi alikuwa anaipeleka wapi.
 
wanyonge hawaamini wanachokisikia
 
1. Si mimi ninayeichafua awamu ya tano, ni ripoti ya CAG
2. Si kila kilichofanyika katika awamu ya tano, madudu yametajwa kila moja kwenye eneo lake

Ulishawahi sikia report zingine za CAG au hii ndio ya kwanza?
 
1. Natamani taarifa ile ungeichambua ukaweka hayo madudu moja baada ya lingine tukayajadili hapa.

2. Masuala mengine ni wahusika kuwa wazembe kushindwa kurejesha majibu kwa wakati kwa CAG (kujibu hoja)

3. Nina imani kubwa Bunge litakapojadili mengi yatatolewa ufafanuzi na yataondoka!

4. Tunamshukuru sana CAG ametekeleza maagizo ya mzee marehemu Hayati JPM na Rais wa sasa Mhe. Samia Sukuhu Hassan kama alivyomwambia ukaandike report ya kina ili tuisaidie serikali na kukomesha ufisadi na wizi. Hivyo CAG amefanya kazi yake kwa weledi kama mwalimu wetu Prof. Assad

Tuwe na akiba ya maneno ndg zangu. Tusubiri Bunge lipitie taarifa hiyo kwa kina tujue mbivu na mbichi.

Namshauri Rais wetu mama yetu Mhe. Samia. Kama kuna mtendaji yoyote yupo madarakani na itathibitika kuiletea Serikali hasara na pia uzembe wa kutokujibu hoja za CAG, basi amtoe haraka sana kabla hajamuharibia kazi.
 
Sirikali Ndo Ile Ile, Chama Ndo Kile Kile Na Viongozi Wake Ndo Walewale, Tofauti Ya Kuona Matumaini Ya Mbadiliko Wa Viongozi Ni Ndogo Hata Kwa 2% Hakuna. Sasa Kipi Kinachokufanya Wewe Zumbukuku Utoe Vijembe? Usichokijua Ripoti Hiyo Ilifanyiwa Kazi Tangu Mzee Akiwa Hai, Hayo Ni Matunda Ya Kazi Yake Nzuri, Lilikuwa Suala La Muda Kuiwakilisha Hata Mzee Angelikuwa Hai Leo Ripoti Ingetoka Hiyo Hiyo. Sasa Mwambieni Mama Tunachotaka Sisi Ni Actions
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…