Ripoti ya CAG imefichua madudu mengi ya awamu ya tano, kulikuwa na ufisadi wa kutisha

Ripoti ya CAG imefichua madudu mengi ya awamu ya tano, kulikuwa na ufisadi wa kutisha

Una moyo sana kupambana kuhalalisha haya ya awamu ya tano
Kama wewe ulivyo na moyo wa kuchafua kila kilichofanyika awamu ya tano

Tulia tusubiri hati safi na chafu watu wawajibike na kuwajibishwa
 
Inabidi upambane sana. Image ya mwendazake inachafuka kwa kasi ya mwanga

hakuna mwenye uwezo huo.

mwendazake anachafuka jukwaa la siasa jamiiforus.

amini nakwambia,atatakata hapa hapa jf siasani mwakani tu mwezi kama huu.
 
Ripoti ya CAG imefichua madudu mengi ya awamu ya tano, kulikuwa na ufisadi wa kutisha, je Fedha hizi ziliibiwa zilipelekwa nchi gani,au bank gani ? Kwà sababu kwenye mabank hakuna fedha na mitaani hakuna fedha. Je aliyekuwa katibu mkuu wizara ya fedha ,Doto James kwanini asilale kwanza segerea uçhunguzi ukiwa unaendeleaje?

afadhali wewe umetumia akili.

hata tunawezakuwa na logic tukihoji kwa namna hii.
 
Kama wewe ulivyo na moyo wa kuchafua kila kilichofanyika awamu ya tano
1. Si mimi ninayeichafua awamu ya tano, ni ripoti ya CAG
2. Si kila kilichofanyika katika awamu ya tano, madudu yametajwa kila moja kwenye eneo lake
 
Mbona haya madudu yanaonekana ni mengi awamu ya tano kuliko hata wakati wa awamu ya nne tuliyodhani ni awamu ya upigaji .....!!

hukutakiwa kudhani awamu ya nne ni ya wapigaji,ilikuwa ni ya wapigaji kweli kweli.na ndio wako mbioni kurudi sasa.
 
Alikuwa mtu mwema sana
Alikuwa na upendo sana
Aliwajali wanyonge wote
Hakubagua watu kwa imani zao wala mitazamo yao
Alipendwa sana na watu wote
Hakuwa fisadi
Hakuwa mwizi
Hakuwa mbinafsi
Hakuwa na kiburi
Alikuwa shujaa wa Africa
Msiba wake ulifuatiliwa na watu billion NNE na ushee duniani kote

Mwendazake kafa lakini hataoza, na hata akiona hatanuka na akinuka atanukia marashi
wanyonge hawaamini wanachokisikia
 
1. Si mimi ninayeichafua awamu ya tano, ni ripoti ya CAG
2. Si kila kilichofanyika katika awamu ya tano, madudu yametajwa kila moja kwenye eneo lake

Ulishawahi sikia report zingine za CAG au hii ndio ya kwanza?
 
Siku ya leo sijui tuuiteje huko; Mbaya? Au nzuri sana?

Ripoti ya mkaguzi mkuu wa serikali inayoendelea kusomwa muda huu si kwamba tu inawaweka CCM na watetezi wa mwendazake kwenye wakati mgumu sana, lakini tayari imechefua wananchi wengi kwa kiwango kisichomithilika.

Madudu ya SHUJAA WA AFRIKA yanatisha na kutia kinyaa.

Madudu ya MTETEZI WA WANYONGE Yanatia hasira sana.

Chukulia hili moja BILIONI 3.9 kwenye matengenezo ya ndege moja ambayo HAIKUFAA![emoji3064][emoji3064][emoji3064][emoji3064]

Upinzani uliwahi kusema upigaji wa awamu hii utavunja rekodi, watu wakabeza sana. Lakini wakati ni hakimu mzuri. Uongo hupanda lift lakini ukweli hukwea ngazi. Mahakama ya mafisadi inaweza kuanzia pale kwenye nyumba ya milele ya mwendaAzakwe marehemu hayati.

Huu uozo uliendelea kuwekwa wazi peupe hivi tusishangae kuona siku moja marehemu akalikimbia kaburi lake. N itokee kuna kitu kinaitwa maandamano kifanyike[emoji848][emoji848][emoji848] Bila udhibiti imara si ajabu kuwakuta waandamanaji wakilicharaza bakora kaburi la shujaa wa Afrika na kuipopoa mawe picha yake.

Baada ya kusomwa hii ripoti, masikio yote yako kwa Bimkubwa. Je, atasemaje? Watu wamefura kwa hasira. I hope hatawazingua
Mahabusu ziandaliwe za kutosha sasa. Ni zamu ya kubadilisha wapangaji. Karibia kila wizara ina vimeo vya kutisha.
1. Natamani taarifa ile ungeichambua ukaweka hayo madudu moja baada ya lingine tukayajadili hapa.

2. Masuala mengine ni wahusika kuwa wazembe kushindwa kurejesha majibu kwa wakati kwa CAG (kujibu hoja)

3. Nina imani kubwa Bunge litakapojadili mengi yatatolewa ufafanuzi na yataondoka!

4. Tunamshukuru sana CAG ametekeleza maagizo ya mzee marehemu Hayati JPM na Rais wa sasa Mhe. Samia Sukuhu Hassan kama alivyomwambia ukaandike report ya kina ili tuisaidie serikali na kukomesha ufisadi na wizi. Hivyo CAG amefanya kazi yake kwa weledi kama mwalimu wetu Prof. Assad

Tuwe na akiba ya maneno ndg zangu. Tusubiri Bunge lipitie taarifa hiyo kwa kina tujue mbivu na mbichi.

Namshauri Rais wetu mama yetu Mhe. Samia. Kama kuna mtendaji yoyote yupo madarakani na itathibitika kuiletea Serikali hasara na pia uzembe wa kutokujibu hoja za CAG, basi amtoe haraka sana kabla hajamuharibia kazi.
 
Sirikali Ndo Ile Ile, Chama Ndo Kile Kile Na Viongozi Wake Ndo Walewale, Tofauti Ya Kuona Matumaini Ya Mbadiliko Wa Viongozi Ni Ndogo Hata Kwa 2% Hakuna. Sasa Kipi Kinachokufanya Wewe Zumbukuku Utoe Vijembe? Usichokijua Ripoti Hiyo Ilifanyiwa Kazi Tangu Mzee Akiwa Hai, Hayo Ni Matunda Ya Kazi Yake Nzuri, Lilikuwa Suala La Muda Kuiwakilisha Hata Mzee Angelikuwa Hai Leo Ripoti Ingetoka Hiyo Hiyo. Sasa Mwambieni Mama Tunachotaka Sisi Ni Actions
 
Back
Top Bottom