Ripoti ya CAG imefichua madudu mengi ya awamu ya tano, kulikuwa na ufisadi wa kutisha

Ukiona mtu ni mkali kuna uchafu anaficha.
Mtu msafi aogopi vyombo vya habari.
 
Huu ni muondelezo wa lile liloanza pale Chamwino siku ya tatu baada ya JPM kuzikwa. Wakaitisha hii ripoti jamanyemzo ya kupoza yatokanayo na mchakato wa mazishi. Ndio mafuta waliyo enda kumpaka marehemu haya. Hakuna jipya hapa.
 
Naomba kuuliza hivi hii ni tofauti na ule uchunguzi wa January to March?
 
Hebu nitajie wabunge watatu watakaoweza kupitia hii ripoti kwa kina!

Tunafurahia siasa za kijinga matokeo ndo haya! Tunasubiri Babu Tale achambue!
 
Kaka Mshana wewe ni mzoefu, nadhani unakumbuka ripoti ya 2014 ambapo hoja karibu zote zilipanguliwa! Nadhani hata hizi ngoja ziende Bungeni. Nina mdogo wangu mahali ananiambia watu wanakimbizana kujibu hizi hoja.

Najiuliza walikuwa wapi kabla? Huu ni uzembe wa hali ya juu. Tunaimani na Bi Mkubwa kuwachukulia hatua wahusika kabla hawajaichafua serikali ya awamu ya sita.
  • Ikithibitika wizi na ufisadi fukuzaa
  • waliichelewa kujibu hoja fukuzaaa
  • waliohonga hela pale OR TAMISEMI wakapata hati safi na kwenye ma taasisi ya umma fukuzaaaa! Wakiwemo hao watumishi wa CAG

Wanadamu ni wabaya sana jamani wasimzingue mama!
 

Wawajibike na kuwajishwa
 
Wamesema tuandike Katiba yenye taasisi huru mumekataa sasa kwa nini kila mtu asipigwe

Afu watumishi ndio tumebebeshwa zigo bovu mbwa kabisa hao wapuuzi na marehemu wao

Yaani maccm ni laana ya nchi hii
 
Ilani ya ccm 2020 - 2025 inasema tutaendelea kupambana na rushwa na ufisadi kwa nguvu zote.


Haisemi ufisadi umeisha.

Hata Ulaya kina Morinyo, Messi, Ronaldo mara kwa mara tunasikia aamepelekwa mahakamani kwa kukwepa kodi.

Hata Chadema wabunge wengi walihama mwaka jana sababu ya ufisadi michango yao. Kinachotakiwa ni kuendelea kupambana na ufisadi
 
Ukweli ni kwamba madhambi mengi yanafanyika kwenye giza. Na ukiona kiongozi anataka giza litawale ujue ana nia ya kuficha madhambi.

Na kwa wale wanaosema Marehemu alikuwa sio mwizi, let's assume ni kweli hakuiba. Lakini kama nchi tulimpa pia kazi ya kulinda rasilimali zetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…