Riwaya: Mwanamke Uliyekula Pesa Zangu Nakutafuta

Riwaya: Mwanamke Uliyekula Pesa Zangu Nakutafuta

Hapa tupo wengi sana tunaofuatilia simulizi ya bwana jina moja kaa mbwa. Lete mambo kijana
 
Jina moja kama mbwa anajifanya sterling katika nchi ya watu haha, pili mbona muda unazidi kwenda tu huko uhindini au amesahau kuwa yupo likizo na Dar pande za mwananyamala alishakaa muda mrefu zaidi ya wiki 3?!
 
Sehemu ya 15

Tulikokotana mpaka chumbani, nilipoubamiza mlango tu, msichana akajibwaga kitandani kisha akaniita kwa jicho la kurembua, “Njoo Mako, usiwe bwege kama siku ile… sogea, nisogelee usiogope!”

Sikutaka kuwa bwege kama alivyosema, nilijibwaga kitandani akanidaka kama nyanda aliye mahiri sana. Yakafuata mabusu mafupi na marefu yaliyochagizwa na mipapaso ya hapa na pale, nazo nguo zikajikuta zikiigusa sakafu moja baada ya nyingine, nasi tukabaki katika namna ambayo ilitufanya tuonekane kama tuliotoka kuzaliwa! Matunda yakaliwa.

Baada ya saa mbili kupita, tukiwa tumeloa jasho, jasho jembamba la wazinzi, nilivunja ukimya.

“Hivi sasa ni saa mbili usiku… baba atakutafuta!”

“Umeshiba uchi sasa unanifukuza!” alilalamika msichana, akizichezea nywele zangu, kipilipili toleo la kwanza.

“Ha ha haa!” nilicheka, nikamtazama msichana, kisha wote tukacheka kicheko kirefu. “Sikujua kama we ni mkorofi kiasi hiki,” nilimchokoza.

“Unanisingizia Mako.”

“Haya nijibu swali langu.”

“Baba hayupo… ameenda Kolkata kwenye kazi zake.”

“Kazi gani?”

“Kazi za babangu ni biashara… yeye huuza bidhaa za kitamaduni.”

“Umewahi Kufika?”

“Sijawahi, Kolkata ni mbali sana, ipo chini huko pembezoni mwa nchi yetu.”

“Umewahi kuona japo bidhaa moja ya kitamaduni uliyoletewa na baba yako?”

“Sijawahi, halafu bwana wee, sitaki maswali,” Deepa alifoka, halafu akalegeza sauti na kunitupia swali, “Vipi umechoka?” Kabla sijajibu, mlango ukagongwa. Nikasogea kilipokitasa nikachungulia nione nani aligonga, nikaona miguu ya wanaume wengi, nikahisi hatari.

Nilirudi mpaka alipolala Deepa, lakini naye nilimkuta akivaa nguo zake haraka kisha akaniambia, “Baba amegundua, kasema kupitia meseji hapa… katuma watu wanirudishe nyumbani, wakati tunacheza tulionekana na watu.”

Nilivaa haraka mlango ukiendelea kugongwa, nikamuomba Deepa avue suruali yake abaki na nguo ya ndani tu, japo hakunielewa, alitii. Nguo zake pamoja na simu nikaziweka katika mfuko. Wakati naweka simu, nilijipigia nikaipata namba yake. Mimi nilivalia kaptura ya kuongelea.

“Fungueni mlango, ama tutaongea na wahusika watupatie funguo,” ilisikika sauti ya mwanamume huko nje.

Baada ya maandalizi yangu kuwa tayari, tena tukiwa tumefungua dirisha na tumesimama katika pembe ya dirisha hilo kubwa, nilimsogelea Deepa, “Usiogope,” nilisema kwa upole. “Unaona pale chini? ile ni ‘swimming pool’, na hapa tulipo siyo juu sana, ni ghorofa ya kwanza tu, hivyo tunajirusha na tukitua itakuwa raha msitarehe.”

Msichana alishtuka akawa kama anayekataa kufanya jambo hilo kwa sababu ya hofu, lakini kabla hajafanya lolote, nilimkamata nikaruka naye tukiwa tumetanguliza miguu, kisha kikasikika kishindo, “Chubwiii!” nikaogelea na msichana mpaka katika ngazi za ‘swimming pool’, tukatazamana, wote tukacheka.

“Sasa, vaa nguo zako haraka halafu kimbia nyumbani, nipigie simu ukifika, namba yangu ipo humo inaishia 21,” nilisema, msichana akatii.

Baada ya msichana kuondoka, nilipandisha ngazi kuelekea kwenye chumba changu. Nikakuta wanaume nane wakiwa wamevaa suti nyeusi katika mlango. Nami nikawasukumasukuma nikijipenyeza katikati yao ili nipite, nikaufikia mlango halafu nikafungua na kuingia ndani, ile nataka niufunge, mmoja akauzuia na kufanya wenzake waingie huku akifuata yeye mwenyewe.

“Karibuni, mnataka nini chumbani kwangu?” niliuliza nikilifunga dirisha. Hawakunijibu, walikuwa bize wakitafuta huku na huko kama wangemwona waliyemtaka, lakini hakuwapo wala hakukuwa na dalili zake.

Waliongea Kihindi, wakanitazama kwa jicho kali halafu wakaondoka waliokasirika kama mnyama mwenye pembe moja.

Inaendelea...

Kuwa wa Kwanza Kupokea mwendelezo wa Riwaya hii Kwa kujiunga katika Group la bure WhatsApp, Gusa Hapa Kujiunga

Tupate Wadhamini:

Kwa Mahitaji ya kuandikiwa CV, Barua ya Maombi ya Kazi na Masomo kwa Wanafunzi wanaorudia mitihani, Gusa Hapa Tuwasiliane Whatsapp.
Story tamu kwel, ila kama imepungua ujazo yaan imekua fupi
 
Zirefushe episodes zako na ni bora ziwe zinaishia sehemu inayompa hamasa msomaji ili azisubirie next episodes with curiousity.
 
Zirefushe episodes zako na ni bora ziwe zinaishia sehemu inayompa hamasa msomaji ili azisubirie next episodes with curiousity.
Ingawa sitafanyia kazi japo jambo moja ulilosema, nashukuru kwa ushauri. Asante sana.
 
Msisitizo

Kwa sababu ya mtindo wangu wa uandishi, ukubwa wa riwaya na mengine niyajuayo mimi, sitaweza kuleta kipande chenye zaidi ya maneno 500 kwa siku.

Malalamiko kuwa riwaya ni fupi yanapoteza ladha ya riwaya yenyewe, kwani badala ya kujadili yale yanayojiri kwenye riwaya, sasa tunajadili urefu wake.

Kama mimi nisivyowakera kwa kuwaomba hela ili niwape simulizi hii, basi nanyi acheni kunikera kwa kunihamasisha niongeze urefu wa simulizi badala yake turidhike na kidogo kilichotumwa huku tukisubiri mwendelezo.

mtaacha au niache?
 
Msisitizo

Kwa sababu ya mtindo wangu wa uandishi, ukubwa wa riwaya na mengine niyajuayo mimi, sitaweza kuleta kipande chenye zaidi ya maneno 500 kwa siku.

Malalamiko kuwa riwaya ni fupi yanapoteza ladha ya riwaya yenyewe, kwani badala ya kujadili yale yanayojiri kwenye riwaya, sasa tunajadili urefu wake.

Kama mimi nisivyowakera kwa kuwaomba hela ili niwape simulizi hii, basi nanyi acheni kunikera kwa kunihamasisha niongeze urefu wa simulizi badala yake turidhike na kidogo kilichotumwa huku tukisubiri mwendelezo.

mtaacha au niache?
tushaacha mkuu
 
Back
Top Bottom