Rostam Aziz: Hakuna mwekezaji atakubali kuwekeza halafu umwambie aende Mahakama ya Kisutu ambapo Majaji wanaweza kupigiwa simu na watu wa Serikali

Yametimia
 
Kasema kweli mfano dangote aliwahi sema akiwa na matajiri wenzie huko uzunguni hivi Tanzania ni nchi hatari kwa wawekezaji
 
Mahakama zote ziko hivyo. Hata hizo mahakama za nje za mabepari zipo kwa ajili ya kulinda masilahi ya serikali za mapepari. Kesi zako ukizipeleka huko kwao lazima utanyolewa, nao vile vile kesi zao wakizileta huku kwetu lazima watanyolewa. Sisi tunachagua kwenda kunyolewa tunapoporwa rasilimali zetu. Wao hawataki tuwanyoe wanapotupora rasilimali zetu. Tuna akili kweli? Lazima tuzinduke!
 
Watu wanasahau magu alisema hivi serikali ni miimili 3 lakini muimili 1 imejichimbia chini kuliko hiyo 2 nini maana yake,mbona majaji na sipika hawakutoka hadharani kumwambia aombe radhi[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
 
Alichosema ni ukweli mchungu ambao unagusa karibu nchi zote za Afrika isipokuwa nchi chache sana, e.g. South Africa.
Mahakama zetu wenzetu wa Magharibi wanaziita "Kangaroo Courts", kiasi kwamba haziaminiki kabisa.
Bora uamini wazee wa kimila huwa wanatenda haki na siyo hizi mahakama za mchongo, upatikanaji wa mahakimu/majaji ni wa mchongo hauko huru
 
Rostam ulimi haukuteleza sema hana tu huo muda wa hide and seek na majaji ila ndiyo ukweli wenyewe.
 
Ndio ukweli wenyewe huo.Bila shaka wahusika watakurupuka huko kuja kukanusha na kupayuka badala ya kujibu hoja
 
Nakazia Mahakama zetu takataka.
 
Huu ndiyo ukweli mtakatifu mahakama haziko huru nchi hii bali ni kitengo cha sheria cha serikali. Rais anaweza kufanya lo lote hata kuinyima fedha za kuendeshea shughuli za mahakama na hakuna atakachofanywa!
Inasikitisha sana
 
Yuko Sahihi. Na Tusitegemee uwekezaji mkubwa hapa nchini Ikiwa Mahakama si chombo huru. Angalia Mahakama za Kenya Rais Hafurukuti
 
Simu moja tu hakimu anapindisha hukumu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…