Rostam Aziz mmiliki mpya wa tiGO Tanzania na Zantel

Kuna siku uliandika kitu kizuri Sana kuhusu hawa watu kutoka Asia kwamba wanachofanya wanakusanya mitaji huko wanakuja kuwekeza kama wazawa wakati kiuhalisia wanatumia mitaji ambayo inatoka nje hivyo kutokuwa na mizania katika ushindani....
Leo naona umeandika hivi kwamba watanzania hatuna jicho la kuona fursa...
Kweli mwenzako akusanyiwe pesa za mafuta huko aje Nazo halafu wewe utegemee pesa ya kilimo cha jembe la mkono mnashindana vipi hapo.
 
Hatuwezi kuwa nchi inayoingilia uhuru wa wafanyabiashara kwa 100% ili wanyonge wafurahishwe kwa kuaminishwa kuwa unyonge wao unasababishwa na matajiri. Tupambane kutafuta fursa halali, ukiipata fursa mawazo ya kumuona mfanyabiashara ni adui na kutaka aje raisi awanyooshae hayatakunyemelea.
 
watu wanatumia opportunity, tuendelee kusubiri wanasiasa waweke mambo sawa na sisi tuwe matajiri maana tunaamini kwa wanasiasa..
Tuwasubiri mpaka lini ?

Kuna kipindi ulikuwa unawalalamikia wafanyabiashara wenye asili ya Asia ila leo unawapongeza....haya bhana tumekuelewa.
 
chanel ten inaonekana itarudi tena kwake rostam.
 
Tuwasubiri mpaka lini ?

Kuna kipindi ulikuwa unawalalamikia wafanyabiashara wenye asili ya Asia ila leo unawapongeza....haya bhana tumekuelewa.

hahahahahaha ni ngumu sana kunielewa..

ninapopaswa kuwalalamikia nawalalamikia na ninapopaswa kuwapongeza nawapongeza...
naulalamikia upande wao wagiza ambao wengi hawausemi ukweli wake..
ila nawapongeza kwenye upande wao mwingine wa maisha na system zao za kuwekeza kwa manufaa ya ukoo...

Bado msimamo wangu uko pale pale, hawa sio wenzetu wapo hapa kutumia kigezo cha uzawa ili kutupiga kwa kucheza na opportunity zilizopo ambazo sisi weusi tumepumbazika hatuna dili nazo...
 
Siyo ugeni na uzawa. Kiushindani si sawa mtu kumiliki kampuni mbili zinafanya kazi moja. Ni kama mtu umiliki Simba na Yanga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…