RUSHWA: Kijana aliyekuwa akiwalaghai na kuwatapeli Maofisa wa Jeshi la Polisi kwa ahadi za ajira akamatwa

RUSHWA: Kijana aliyekuwa akiwalaghai na kuwatapeli Maofisa wa Jeshi la Polisi kwa ahadi za ajira akamatwa

Afande pokea taarifa kuhusiana na mahojiano yaliyofanyika leo Tarehe 04/04/2022 baada ya kukamatwa kwa mtuhumiwa wa makosa ya utapeli David Damas Otieno @ MAJOR GENERAL MRAI miaka 39, kabila mjaruo, kazi mkulima, dini mkristo mkazi wa Dar es salaamu ambaye amekamatwa leo Tarehe 04/04/ 2022 katika eneo la Msamvu wilaya ya Morogoro mjini mkoa wa Morogoro. Ametaja jumla ya matukio 21 aliyowahi kutapeli akapata pesa na mengine aliahidiwa lakini hakupata pesa Kama ifuatavyo:

1. RPC IRINGA _ JUMA BWILE
Aliwasiliana naye Nov. 2021 ili mtoto wake atafutiwe ajira ktk idara ya usalama wa Taifa akamtumia 150,00/= kwa awamu mbli ya Kwanza 100000/= ya pili 50,000/=

2.OCD MUSOMA
Alitaka ahamishiwe Kahama, alituma 250,000/=

3.RPC KAGERA _ REVOCATUS MALIMI
Alitaka nafasi ya ajira ya TAKUKURU kwa kijana wake, alituma 400,000/=.

4. OCD KAHAMA
Alitaka apandishwe cheo, alituma pesa 270,000/= awamu ya kwanza, na awamu ya pili alituma samaki wakubwa Aina ya Sato waliokaangwa kwenye gari la HAPPY NATION la Mwanza Dar es salaamu ambao aliwauza kwa 65,000//=

5. STAFF OFFICER MOROGORO _ KUNGURA. Baada ya kupandishwa cheo kuwa ACP akitokea OCD Mvomero
alitaka kuwa RPC mkoa wa GEITA Ili awe karibu na nyumbani kwao sababu anakaribia kustaafu, hakutuma pesa alishtuka.

6 DEBORA DAUDI MAGRIGIMBA
Alitaka arudishiwe nafasi ya RPC baada ya kuhamishwa KUTOKA RPC SINGIDA KUWA STAFF OFFICER CENTRAL POLICE DAR ES SALAAMU.
Hakutuma pesa waliwasiliana Kama ndugu wakabila moja la wasukuma ingawa mtuhumiwa siyo msukuma.

7. OCD KISHAPU SHINYANGA
Alitaka kupandishwa cheo na ahamishiwe SHINYANGA Mjini kwani KISHAPU ni kijijini Sana
aliahidi kutuma million mbili lakini kabla hajatuma alipata msiba.

8. MICHAEL DELELI _ Aliyekuwa RTO KILIMANJARO
Alitaka arudishiwe kuwa RTO MOROGORO baada ya kuhamishwa kuwa RTO KILIMANJARO, aliahidi kutoa million moja Ila mtuhumiwa alizima simu yake kwa kuwa anajua kuwa anatafutwa na polisi kwa vitendo vyake hivyo vya kutapeli.

9. MZIRAI _ OCS MEATU
Alitaka apandishwe cheo TOKA ASP kuwa SP na ahamishiwe SHINYANGA Mjini au Kahama sababu alikaa na cheo hicho zaidi ya miaka 08. Alituma 60,000/= za voucher.

10. OCD LUANGWA
Alitaka mtoto wake apate ajira ktk idara ya usalama wa Taifa, aliahidi million moja lakini hakutuma.

11. RTO KAGERA
ALitaka awe RTO MWANZA, aliahidi kutoa million moja baada ya siku tatu lakini hakutuma.

12. OCD TARIME
Alitaka kuwa OCD ILEMELA MWANZA
alituma 200,000/=

13 OCD RUVUMA
Alitaka ahamishiwe Bagamoyo karibu na familia yake, aliahidi million moja lakini hakutoa.

14 RCIO IRINGA CHARLES BUKOMBE
Alitaka arudishiwe nafasi ya RTO na apangiwe MOROGORO, aliahidi kutoa zawadi suala lake likifanikiwa.

15.OCD MAGU
Alitaka ahamishiwe kuja Morogoro au Chalinze ili awe karibu na familia yake, aliahidi million moja lakini hajatuma.

16.RTO TARIME LORYA
Alitaka arudishwe Mwanza, alituma 150,000/=

17. OCD MAKETE
Alitaka ahamishiwe Bagamoyo aliahidi zawadi likifanikiwa.

18. OCD ILAMBA _ SINGIDA
Alitaka ahamishiwe wilaya ya Manyoni, aliahidi million moja lakini hakutuma.

19. OCD BIHARAMULO
Alitaka ahamishiwe GEITA
Aliahidi million moja lakini hakutuma.

20. RTO LINDI
Alitaka ahamishiwe Morogoro, aliahidi zawadi akifanikiwa.

21. OCD TANDAHIMBA
Alitaka ahamishiwe Chalinze, aliahidi 500,000/= lakini hakutoa.

Mtuhumiwa baada ya kukamatwa alipekuliwa maungoni ambamo alikutwa na simu tatu:

ITEL MBILI, TECNO MOJA, RADIO CALL MOJA Aina ya BAOFENG NA CHARGER YAKE MOJA, PESA TASLIMU 55,600/= NA CHARGER YA SIMU MOJA. Pia alipekuliwa katika chumba Namba 05 Cha Guest iitwayo THREE ROOF iliyopo maeneo ya Msamvu ambako alikutwa amefikia na vitu vifuatavyo vilichukuliwa:

Bag moja dogo la mgongoni rangi ya ugoro likiwa na nguo mbalimbali, N_ CARD_ 1000, 0000,0058, 9675, na charger ya simu.

Kesi ya KUJIFANYA AFISA WA SERIKALI IMEFUNGULIWA
Naomba kuwasilisha.

USSR
Ni lini sasa tutapata IGP mpya?
 
Mbona pesa kidogo sana hizo?
Ukweli ambao hautasemwa au kutafutwa.
Huyu mkulima alipigiwa simu yeye au aliwapigia?

Ukweli ni kwamba huyu Otieno ndiye aliyewapigia ikiwa anajua status zao halisi kuwa unataka uhamie mahali flani au uliondolewa cheo kwa uonevu.

Anawapigia na kuwaambia yeye ni afisa usalama na kujifanya kuwa anaweza kumsaidia hitaji lake.

Pili kuna watu walilengwa kuchafuliwa kwa makusudi na askari wenzio.

Hivyo tapeli anapewa taarifa zao naye tapeli anapita mule mule.

Askari wana majungu sana.
 
Ukweli ambao hautasemwa au kutafutwa.
Huyu mkulima alipigiwa simu yeye au aliwapigia?

Ukweli ni kwamba huyu Otieno ndiye aliyewapigia ikiwa anajua status zao halisi kuwa unataka uhamie mahali flani au uliondolewa cheo kwa uonevu.

Anawapigia na kuwaambia yeye ni afisa usalama na kujifanya kuwa anaweza kumsaidia hitaji lake.

Pili kuna watu walilengwa kuchafuliwa kwa makusudi na askari wenzio.

Hivyo tapeli anapewa taarifa zao naye tapeli anapita mule mule.

Askari wana majungu sana.
Huyo anayeitwa Tapeli mimi namchukulia kama mtu makini sana. Tena mwenye influence
 
Hii imekuja si kwa bahati mbaya ila ili tijue uozo uliojaa ndani ya jeshi la polisi. Sasa ni wazi tumejua kumbe vyeo na uhamisho hutolewa kwa rushwa ndani ya polisi. Mambo ya ajabu kabisa. Sasa kama wakubwa hao ndo wanahaha ns rushwa Hawa vijana wa vyeo vya chini hali ikoje? Ni aibu kubwa kwa jeshi la polisi. Ila nimeshangaa kutomkuta RPC wa Kinondoni akiomba kupelekwa hata mkoani ili apumue baada ya kuhenyeshwa na Kibatala.
 
Mbna hao watu wengi wanataka kupelekwa Bagamoyo, kuna nn huko? [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Na Morogoro trafiki wanapapenda Sana wakati ndipo penye ajali nyingi kwanini?
 
Achaga mazarau sasa picha iko wapi?

Mbona yule wa Zanzibar picha mlileta?
 
Itakuwa vyema kama na Mh sana Mama Samia anaufatilia.
Nimejikuta nawaza hivi: yaani hotuba zenyewe anaandikiwa karatasi 6 anasoma 1 atapata nafasi ya kufuatilia uozo huu kweli?.....acha niishie hapa!
 
Huyu anatakiwa apewe tuzo na sio kufunguliwa mashtaka bali amefanya kazi ya kutuambia kuwa Jeshi la police halina uadilifu na nafasi zao zinapatikana kwa hongo.

Kwa jicho jingine huyo jamaa sio raia tu ila atakanwa kama kawaida 🥲🥲🥲
 
Back
Top Bottom