Ruto, Raila kuelekea Jumatatu, Tanzania tuna mengi ya kujifunza

Ruto, Raila kuelekea Jumatatu, Tanzania tuna mengi ya kujifunza

KENYA NI YA WAMCHI, SIYO YA WAJALUO IF YOU PICKET MY SHOP AND STOP ME FROM SELLING MY WARES, YOU ARE GOING TO BE DISENFRANCHISING ME SO THE LAW MST STOP YOU. WHAT HAPPENS IF PEOPLE ANDAMANA KUPINGA WANAONDAMANA AU WANAANZISHA VIKUNDI VYA ULINZI KUJIHAMI NA WAANDAMANAJI, SI NI VITA?
Ndezipanya kind
 
Wakenya wapo mbali sana ukilinganisha na waTz, kwanza raia wa Kenya walio wengi wanafaham haki zao tofaut na waTz, Tz life inakwenda ilimradi tu, Watawala ndio Miungu na wanaweza hata uza Nchi na Raia wasihoji.

Tunayo safari ndefu sana. Angalia post #20.

Kazi kweli kweli.
 
Sasa katiba mpya na tume huru ya uchaguzi waliyo nayo wakenya inawasaidia nn?.malalamiko ya uchaguzi hayaishi,

Katiba ya Kenya inahakikisha kuwa mwenye nchi ni mwana nchi. Inawasaidia kuhakikisha hakuna Mungu mtu.

Unafata matakwa ya watu sivyo unakwenda na maji. Hufuati kuna consequences na ikibidi utafurushwa.

Angalia Kwa miungu watu: nchi ni ya walamba asali Kwa raha zao. Kama haturidhiki mlango wazi kuelekea Burundi.

Disgusting!
 
Ajabu bado kuna wajinga wanaopinga uwepo wa Katiba Mpya Tanzania.

Ukitazama mlolongo wa yale yaliyojitokeza siku za karibuni, kuanzia vyombo vya habari kupewa onyo kali kwa kuripoti taarifa za maandamano, navyo kwenda mahakamani kudai haki yao na wakaipata, hii hatua Tanzania bado tuko nayo mbali sana.

Wakenya wametuacha, tuko nyuma yao, hili halina ubishi na yeyote asiyeliona ni kipofu wa macho na akili, bado yupo gizani.
 
HUYU BABU HANA HEKIMA KABISA, HAPO KITAMBO WAZEE NDIYO WALIKUWA NGUZO ZA AMANI, LAKINI NAONA AJABU KABISA KWA MZEE RAO.
 
"Katikati ya lindi la yaliyotukuta Kagera, Mola atufanyie wepesi janga hili lituepuke."

Hata hivyo maisha lazima yaendelee.

Kutokea kwa majirani zetu:

Ilikuwa wiki yenye mengi kutokea Jumatatu iliyopita iliyoshuhudia kimbembe cha kufa mtu, pata shika nguo kuchanika.

Miamba miwili kila mtu kwenye ngome yake ikaendelea kujiwinda na kuvurumishiana magoma ya vita.

Upande wa Ruto:

1. Wakatoa miito rasmi kuomba kama vipi wahisani au hata ICC waingilie kati kumtia adabu Baba kwa wanachokiita utoto tundu wake wa kutaka kuivuruga Kenya.
2. Wakavilaumu vyombo vya habari kwa kuyapatia mileage maandamano yale.
3. CAK (kama ilivyo TCRA ya kwetu) ikavipiga onyo kali vyombo vyote vya habari vilivyo ripoti matukio ya Jumatatu.
4. CAK ikapiga marufuku kufanya coverage yoyote kuhusiana na maandamano. Tishio lile lile pendwa la kupokonywa leseni.

"Tangia jana si radio, gazeti au TV ziliweza kusema lolote kuhusu maandamano yaliyopita au yajayo."

Upande wa Baba:

1. Utamu wa harufu ya ukombozi ukawafanya yeye na wafuasi wake kuongeza dozi ya maandamano kuwa 2 kwa wiki badala ya 1.

"Vyuma vikasubiriwa kuumana."

Wadau wengine:

1. Maaskofu wa RC Kenya kwenye mkutano wao rasmi kuhusu mzozo huu, wakatoa tamko kuwataka wawili hao kuridhiana. Yaani maongezi ya ana kwa ana mezani. Maridhiano!

2. Vyombo vya habari vikakimbilia mahakamani haki yao ya kuhabarisha na kina sisi kuhabarishwa vimekiukwa.

3. Mahakama nayo haikufanya ajizi. Kwenye hukumu iliyotolewa Leo, CAK, chali! Hatua zote alizokuwa kachukua ni batili. Magazeti, Radio na TV zikarejea tulipokuwa.

Tulipo sasa tuko square "A". Jumatatu ni D-Day kwa ari mpya, nguvu na kasi mpya.

Jumatatu polisi hawana kisingizio kwani maandamano yatakuwa halali.

"Kenya wenye nchi wananchi!"

Ishukuriwe Katiba yao bora kabisa waliyokuwa nayo.

Tuipiganie Katiba mpya ndugu zangu. Wenye nchi wananchi tunastahili vilivyo bora.

Source: Nation Media

Andiko zuri la kisomi, great summery... Limegusa maeneo yote Muhimu............
 
Tuipiganie Katiba mpya ndugu zangu. Wenye nchi wananchi tunastahili vilivyo bora.
 

Kwetu wapi pana nafuu? Tunahitaji katiba mpya itakayo hakikisha mwenye nchi ni mwananchi.

Ngoja Baba anyooshe watu hapa tupate somo.
 
Cha moto anakiona je kama:

1. Maandamano ni halali?
2. Live coverage ya media ni guaranteed?
3. Mahakama ni huru hakuna kucheza faulo?
4. Wenye nchi ni wananchi?

Ruto anapumulia machine.

Kama mahakama ni huru, Kwanini Raila aandamane na kudai haki ya kudhurumiwa kwenye uchaguzi na pia na Mahakama hiyo huru na ya haki. Au mmesahau. Tanzania kwa Mtanzania ni the best.
 
Lengo si kumtoa madarakani. Kuna mambo hataki kuwasikiliza. Kama hataki kuwasikiliza njia zingine halali ndiyo hizi sasa.

"Kwanini wasimtoe sasa kwa mujibu wa katiba kama hafanyi anayopaswa kufanya kwa mujibu wa katiba?"

Maana kamili ya wenye nchi wananchi.

Hao wanapndamana Ni wakenya au waluo?
 
Akili zako mbona ndizo za ku copy na ku paste mkuu?

Wewe hujui kuwa katiba ya Kenya ni bora zaidi kuliko yetu? Hujui ya South Africa ni Bora kuliko yetu?

Au hata hujui vigezo vya kutambua ubora wa katiba?

Au ninyi ni wale ambao mkisikia katiba mpya mnapatwa na msongo mawazo?

Kaeni kwa kutulia msiyoyataka hayana muda mrefu bado.

We ndo mjinga sana.
 
Back
Top Bottom