Ruto, Raila kuelekea Jumatatu, Tanzania tuna mengi ya kujifunza

Ruto, Raila kuelekea Jumatatu, Tanzania tuna mengi ya kujifunza

"Katikati ya lindi la yaliyotukuta Kagera, Mola atufanyie wepesi janga hili lituepuke."

Hata hivyo maisha lazima yaendelee.

Kutokea kwa majirani zetu:

Ilikuwa wiki yenye mengi kutokea Jumatatu iliyopita iliyoshuhudia kimbembe cha kufa mtu, pata shika nguo kuchanika.

Miamba miwili kila mtu kwenye ngome yake ikaendelea kujiwinda na kuvurumishiana magoma ya vita.

Upande wa Ruto:

1. Wakatoa miito rasmi kuomba kama vipi wahisani au hata ICC waingilie kati kumtia adabu Baba kwa wanachokiita utoto tundu wake wa kutaka kuivuruga Kenya.
2. Wakavilaumu vyombo vya habari kwa kuyapatia mileage maandamano yale.
3. CAK (kama ilivyo TCRA ya kwetu) ikavipiga onyo kali vyombo vyote vya habari vilivyo ripoti matukio ya Jumatatu.
4. CAK ikapiga marufuku kufanya coverage yoyote kuhusiana na maandamano. Tishio lile lile pendwa la kupokonywa leseni.

"Tangia jana si radio, gazeti au TV ziliweza kusema lolote kuhusu maandamano yaliyopita au yajayo."

Upande wa Baba:

1. Utamu wa harufu ya ukombozi ukawafanya yeye na wafuasi wake kuongeza dozi ya maandamano kuwa 2 kwa wiki badala ya 1.

"Vyuma vikasubiriwa kuumana."

Wadau wengine:

1. Maaskofu wa RC Kenya kwenye mkutano wao rasmi kuhusu mzozo huu, wakatoa tamko kuwataka wawili hao kuridhiana. Yaani maongezi ya ana kwa ana mezani. Maridhiano!

2. Vyombo vya habari vikakimbilia mahakamani haki yao ya kuhabarisha na kina sisi kuhabarishwa vimekiukwa.

3. Mahakama nayo haikufanya ajizi. Kwenye hukumu iliyotolewa Leo, CAK, chali! Hatua zote alizokuwa kachukua ni batili. Magazeti, Radio na TV zikarejea tulipokuwa.

Tulipo sasa tuko square "A". Jumatatu ni D-Day kwa ari mpya, nguvu na kasi mpya.

Jumatatu polisi hawana kisingizio kwani maandamano yatakuwa halali.

"Kenya wenye nchi wananchi!"

Ishukuriwe Katiba yao bora kabisa waliyokuwa nayo.

Tuipiganie Katiba mpya ndugu zangu. Wenye nchi wananchi tunastahili vilivyo bora.

Source: Nation Media
Post hii ni tumbojoto kwa kilamwanaCCM including me.

Lakini Roho wa Bwana ananiambia yeye ni Mkuu wala nisihofie kusimamia ukweli.

Hongereni Wakenya
 
Kama mahakama ni huru, Kwanini Raila aandamane na kudai haki ya kudhurumiwa kwenye uchaguzi na pia na Mahakama hiyo huru na ya haki. Au mmesahau. Tanzania kwa Mtanzania ni the best.

Mahakama ya Kenya huwezi kulinganisha na mahakama za bongo. Mahakama za Tanzania zitatumia miaka miaka mitano kuamua kesi ya Halima Mdee ila Kenya watatumia siku tano kuamua kesi ya u haguzi wa Rais. Tena ikiendeshwa live.

Sisi mahakama zetu zipo kuinufaisha CCM na Rais aliyepo not otherwise.
 
Kama mahakama ni huru, Kwanini Raila aandamane na kudai haki ya kudhurumiwa kwenye uchaguzi na pia na Mahakama hiyo huru na ya haki. Au mmesahau. Tanzania kwa Mtanzania ni the best.

Halafu masndamano ni kwaajili ya ugumu wa Maisha. Pia wanadai wale wajumbe wa Tume warudishwe.
 
Ruto anashindwaje kumkamata Raila ili mambo yatulie?
 
Wakenya kwa kuuana hawana muda wa kuchekacheka! Inabidi na sisi tupate katiba mpya tufanye hivyo. Hii katiba ya sasa inatuminya - ituachie tufanye kama wenzetu waKenya.
Machinga, mama lishe, bodaboda wanayajua hayo. Siku zote watakiwa mtaji wa wanasiasa
 
Katiba inayochochea machafuko ndiyo nzuri kweli.

Taja kifungu Cha katiba ya Kenya inayochochea vurugu. Sisi tubaki na uchawa kwa Rais kwa kunlamba miguu ila tusiwalazimishe wengine wawe Kama sisi.
 
Kama katiba mpya matokeo yake ni vurugu bora tuendelee na katiba iliyopo

Tuendelee na uchawa na kumlamba miguu Rais?. Watu wa ugumu wa Maisha lakini wanalilia vyumbani kisa uchawa. Chawa akiona maandamano anasema ni vurugu. Tuendelee kumpongeza Rais kila mwaka na kumsifu .
 
1. Kulikoni mtu mmoja kututaka kutokomea Burundi huko kama hatukubaliani naye?
Mpinzani huyo
2. Kulikoni mtu mmoja kututaka tujadili uganga wa kienyeji kama hatukubaliani naye?
Mpeleke mahakamani
3. Kulikoni mtu mmoja kituundia genge la wasiojulikana kutuuwa, kututesa, kutujeruhi, kutupoteza nk kwa sababu hatukubaliani naye?
Wewe na nani....hayupo sasa hivi, nini kinachokuzuia kwenda mahakamani?
4. Kulikoni mtu kutaka tubaki na m@vi yetu kama hatukubaynaye?
Hiyo nayo inahitaji katiba mpya? Maandamano?
5. Kulikoni mtu kutaka kuwaweka bakora Hadi shangazi zetu kama hatukubaliani naye?
Na hilo linahitaji maandamano? Kivipi mkuu utueleweshe.

6. Kulikoni magenge ya walamba asali na wahuni kujimilikisha nchi?
Binafsi ningeanza na aliyesema kuna kulamba asali, aje aseme hilo buyu lipi wapi, zaidi ya hapo ni Msamiati kama misamiati yeyote ile.
7. Nk, nk.
Aisee, hayo kwenye list juu hayasimami katika mahakama yeyote ile duniani. Hakuna! Hakuna Mahakama ambayo unaweza kuthibitisha hayo au Kudai kitu chechote kile! Sembuse ziwe sababu za kudai au kubadilisha Katiba. ya Nchi yeyote ile.
 
Tanzania ni ya Watanzania Kenya ni ya Wakenya.
Wakenya wana Katiba yao na Siasa zao zenye desturi na tamaduni tofauti kabisa na Tanzania.
Katiba ya Tanzania haimkatazi mtu yeyote Kuandamana Tanzania, hivyo basi kudai uhitaji wa Katiba mpya ili watu waandamane hauna mshiko.

Watu wanaandamana kama imetokea Wananchi wanafinywa haki zao za msingi....na hilo halipo Tanzania. Katiba ya Tanzania haimfinyi Mtanzania. Ila naweza kuafiki kuwa Katiba inafinywa. Ati watu waandamane kwa sababu umeambiwa ubaki na mavi yako! Yaani ukafanye uasi wa sheria kwa sababu umeambiwa ubaki na mavi yako! Kwa sababu umeambiwa uhamie Burundi! Ndio maana huu uasi wenu mnaotaka ufanyike Tanzania hautafanyika.
 
Tanzania ni ya Watanzania Kenya ni ya Wakenya.
Wakenya wana Katiba yao na Siasa zao zenye desturi na tamaduni tofauti kabisa na Tanzania.
Katiba ya Tanzania haimkatazi mtu yeyote Kuandamana Tanzania, hivyo basi kudai uhitaji wa Katiba mpya ili watu waandamane hauna mshiko.

Watu wanaandamana kama imetokea Wananchi wanafinywa haki zao za msingi....na hilo halipo Tanzania. Katiba ya Tanzania haimfinyi Mtanzania. Ila naweza kuafiki kuwa Katiba inafinywa. Ati watu waandamane kwa sababu umeambiwa ubaki na mavi yako! Yaani ukafanye uasi wa sheria kwa sababu umeambiwa ubaki na mavi yako! Kwa sababu umeambiwa uhamie Burundi! Ndio maana huu uasi wenu mnaotaka ufanyike Tanzania hautafanyika.
Unaishi sehemu Gani tz? Watu hapa wakitaka kuandamana mara nyingi Huwa hawapewi vibali makusudi Ili magari ya maji ya kuwasha na virungu na mabuti vikawahusu wakikaidi!
Hapo ndio mahali askari wanafanyia practice kupiga wajinga!

WaTz wanapenda sana kuandamana ila Katika majaribio yao kulipatikana mabuti na virungu na maji ya washawasha wakanywea na kina Akwilina walikufa hapo ndo wanachoogopa. Haki ya kuandamana tz Iko kwenye makaratasi tu, au kama ni kuunga juhudi ruksa kuandamana mwaka mzima sio kupinga serikali!
 
Mnalazimisha hila ambazo Mtanzania, Mwananchi wa Mtaani hana. Hila za kutaka dola kwa Lazima. Hila za Viongozi wa Chama.

Haya, Vyama mbadala vimepewa nafasi ya kuuza sera zao, wanafanya nini? Wanatukana wananchi ilihali wakasirike wafikie stage waanze kuvunja sheria, waingie barabarani na kudai Chupi? au Kudai walishwe Ubwabwa badala ya Ugali. Hizo ni hadaa, huko ni kuwatia hasira wananchi pasipo na sababu za msingi. Huo ndio ubinafsi wa Wakuu . Uzeni sera zinazoeleweka.

Kenya, Sera za Raila zilinunulika, hatahivyo kura hazionyeshi hivyo. hatahivyo historia ya ukabila ndio inatoa msukumo huko na ndio kinachotokea hapa Tanzania ingawaje tunajidai sio hivyo. Nani asiyejua hayo? Vita kubwa humu is more cultural, ni vita za matabaka than the actual issues you are raising.
 
Africa ni shida nadhani hata waliopigania Uhuru hawakujia baada ya Uhuru nini kilitakiwa kufanyika kwasababu nguvu KUBWA walielekeza kupata Uhuru bila kujiandaa baada ya Uhuru watafanya nini.
Sasa imehamia kwenye katiba mpya naamini baada ya katiba mpya hawaelewi nini kitafanyika wengine wanadhani katiba mpya itatatua matatizo yote kumbe Pia itatumiwa na adui kukusumbua NCHI zilizoendelea zina katiba nzuri je,wao wapo salama? Je,wewe ukipewa NCHI utakidhi kila hitaji la mwananchi? Afrika tunasafari ndefu sana. Tuombe Kwa Mungu kizazi kijacho kitoke kwenye Giza hili.
 
Back
Top Bottom