Ruto, Raila kuelekea Jumatatu, Tanzania tuna mengi ya kujifunza

Ruto, Raila kuelekea Jumatatu, Tanzania tuna mengi ya kujifunza

Kama mahakama ni huru, Kwanini Raila aandamane na kudai haki ya kudhurumiwa kwenye uchaguzi na pia na Mahakama hiyo huru na ya haki. Au mmesahau. Tanzania kwa Mtanzania ni the best.

Mahakama huru inaweza kufanya kazi yake kwa uhuru kama mwenye nchi ni mwananchi. Ndiyo maana CAK mahakamani kaangukia pua. Mwenye kuulinda uhuru wa mihimili dhidi ya uliojichimbia sana ni mwananchi. Hapa ndipo ilipo kazi ya hii katiba sasa. Uhuru iliyonayo mihimili siyo kwa ajili ya kuwa abused.

Mwenye nchi mwananchi. Mwenye nchi siyo mhimili wowote. Mihimili yote inawajibika kwa mwenye nchi. Wowote ukipotoka mwananchi atautia adabu.

Labda kama wewe unadhani mihimili hii haiwezi kupotoka!

Habari ndiyo hiyo.
 
Kuna wanaopewa viroba pombe bangi na mirungi

Sent using Jamii Forums mobile app

Kuna na ambao hawakupewa viroba wala pombe. Kwenye hali hiyo kinachogomba ni namba.

Ukishaifahamu namba kinachofuata inakuwa wengi wape.

Si ndiyo ulio utaratibu wa kistaarabu mjomba?

Usipowaoa watakupokonya. Ndiyo yanayomkabili Ruyo sasa iwapo ataendelea kushupaza shingo.
 
Hao wanapndamana Ni wakenya au waluo?
Wanaoandamana ni hawa hapa:

Screenshot_20230321-071500.jpg

Hao ni wakenya.

Si Ruto, Gachagua wala genge lao la Kenya Kwanza lililowaita kuwa waluo ila wewe Nanjilinji Kilwa huko. Halafu ajabu na kweli wala hujishangai.

Kazi kweli kweli.
 
"Katikati ya lindi la yaliyotukuta Kagera, Mola atufanyie wepesi janga hili lituepuke."

Hata hivyo maisha lazima yaendelee.

Kutokea kwa majirani zetu:

Ilikuwa wiki yenye mengi kutokea Jumatatu iliyopita iliyoshuhudia kimbembe cha kufa mtu, pata shika nguo kuchanika.

Miamba miwili kila mtu kwenye ngome yake ikaendelea kujiwinda na kuvurumishiana magoma ya vita.

Upande wa Ruto:

1. Wakatoa miito rasmi kuomba kama vipi wahisani au hata ICC waingilie kati kumtia adabu Baba kwa wanachokiita utoto tundu wake wa kutaka kuivuruga Kenya.
2. Wakavilaumu vyombo vya habari kwa kuyapatia mileage maandamano yale.
3. CAK (kama ilivyo TCRA ya kwetu) ikavipiga onyo kali vyombo vyote vya habari vilivyo ripoti matukio ya Jumatatu.
4. CAK ikapiga marufuku kufanya coverage yoyote kuhusiana na maandamano. Tishio lile lile pendwa la kupokonywa leseni.

"Tangia jana si radio, gazeti au TV ziliweza kusema lolote kuhusu maandamano yaliyopita au yajayo."

Upande wa Baba:

1. Utamu wa harufu ya ukombozi ukawafanya yeye na wafuasi wake kuongeza dozi ya maandamano kuwa 2 kwa wiki badala ya 1.

"Vyuma vikasubiriwa kuumana."

Wadau wengine:

1. Maaskofu wa RC Kenya kwenye mkutano wao rasmi kuhusu mzozo huu, wakatoa tamko kuwataka wawili hao kuridhiana. Yaani maongezi ya ana kwa ana mezani. Maridhiano!

2. Vyombo vya habari vikakimbilia mahakamani haki yao ya kuhabarisha na kina sisi kuhabarishwa vimekiukwa.

3. Mahakama nayo haikufanya ajizi. Kwenye hukumu iliyotolewa Leo, CAK, chali! Hatua zote alizokuwa kachukua ni batili. Magazeti, Radio na TV zikarejea tulipokuwa.

Tulipo sasa tuko square "A". Jumatatu ni D-Day kwa ari mpya, nguvu na kasi mpya.

Jumatatu polisi hawana kisingizio kwani maandamano yatakuwa halali.

"Kenya wenye nchi wananchi!"

Ishukuriwe Katiba yao bora kabisa waliyokuwa nayo.

Tuipiganie Katiba mpya ndugu zangu. Wenye nchi wananchi tunastahili vilivyo bora.

Source: Nation Media
Katiba inayochochea machafuko ndiyo nzuri kweli.
 
Mimi nilishangaa eti watapokonywa leseni. Kumbe hawajui kuwa Kenya mahakama zao ni tofauti.
 
Uhuru wa kiboya huo Yani mnaandamanishwa kwa maslai ya mwanasiasa

Hali ngumu ya Maisha ni mwansiasa au mwananchi? Hukuona wamama wanalia na masufuria?. Tanzania Hali ngumu ila watu wanalilia vyumbani.
 
Katiba inayochochea machafuko ndiyo nzuri kweli.

Katiba haichochei machafuko ila inampa mwananchi sehemu yake kamili kwenye kuamua hatma ya nchi yake.

1. Kulikoni mtu mmoja kututaka kutokomea Burundi huko kama hatukubaliani naye?
2. Kulikoni mtu mmoja kututaka tujadili uganga wa kienyeji kama hatukubaliani naye?
3. Kulikoni mtu mmoja kituundia genge la wasiojulikana kutuuwa, kututesa, kutujeruhi, kutupoteza nk kwa sababu hatukubaliani naye?
4. Kulikoni mtu kutaka tubaki na m@vi yetu kama hatukubaynaye?
5. Kulikoni mtu kutaka kuwaweka bakora Hadi shangazi zetu kama hatukubaliani naye?
6. Kulikoni magenge ya walamba asali na wahuni kujimilikisha nchi?
7. Nk, nk.

Yote hayo katika uendeshaji wa nchi ambayo ni yetu sote?

Kwani wewe ni mmoja wa wahuni au walamba asali au jamaa yao, mliojimilikisha nchi na kuifanya kuwa yenu?

Mmekuwa wachafu kuliko hata wataleban?

Aibu: Taliban wanapotuzidi kwenye utawala bora

Katiba ya Kenya inamzuia Ruto na genge lake kutoihodhi Kenya kama ndugu hawa:

Waziri Uweso akisherehea birthday yake nyumbani kwa JK hapa New York, Marekani

Habari ndiyo hiyo.
 
Wakenya kwenye kupigania haki zao ni miamba halisi. Hawana muda wa kuchekacheka na kima.
Kuna kitu watanganyika twende sasa tukajifunze kwa wakenya.

Huku Gerald hando kapinga mikopo kaondolewa kazini. Tanzania bado Sana.
 
Mimi nilishangaa eti watapokonywa leseni. Kumbe hawajui kuwa Kenya mahakama zao ni tofauti.

Ruto atakuwa alipewa mwongozo uchwara kutokea bongo na mifano kedekede ya TCRA na kuzima mitandao.

Mwenye nchi mwananchi.

Upuuzi huo ni batili.
 
KENYA NI YA WAMCHI, SIYO YA WAJALUO IF YOU PICKET MY SHOP AND STOP ME FROM SELLING MY WARES, YOU ARE GOING TO BE DISENFRANCHISING ME SO THE LAW MST STOP YOU. WHAT HAPPENS IF PEOPLE ANDAMANA KUPINGA WANAONDAMANA AU WANAANZISHA VIKUNDI VYA ULINZI KUJIHAMI NA WAANDAMANAJI, SI NI VITA?

Tatizo unalazimisha Kenya ifanane na Tanzania. Wanaandamana kupinga ugumu wa Maisha na kukosekana kwa ajira. Kenya vijana wengi hawana ajira. Shida yenu mnalipeleka kikabila.
 
Huku Gerald hando kapinga mikopo kaondolewa kazini. Tanzania bado Sana.
Kuna na yule wa TRL aliyefukuzwa kwa kutoa maoni yake tu kwenye group binafsi la Whatsapp kuhusu Tozo.

Hivi unaoitwa msala wake ulikwisha je, au ndiyo kiliumana moja kwa moja?
 
Wakenya kwa kuuana hawana muda wa kuchekacheka! Inabidi na sisi tupate katiba mpya tufanye hivyo. Hii katiba ya sasa inatuminya - ituachie tufanye kama wenzetu waKenya.

Katiba yetu inatufanya tuwe chawa wa Rais kwa kupenda au kutopenda.
 
Back
Top Bottom