Ruto, Raila kuelekea Jumatatu, Tanzania tuna mengi ya kujifunza

Ruto, Raila kuelekea Jumatatu, Tanzania tuna mengi ya kujifunza

Unaishi sehemu Gani tz? Watu hapa wakitaka kuandamana mara nyingi Huwa hawapewi vibali makusudi Ili magari ya maji ya kuwasha na virungu na mabuti vikawahusu wakikaidi!
Hapo ndio mahali askari wanafanyia practice kupiga wajinga
Kuna maandamano karibu nchi tano sita sasa hivi....nionyeshe moja tu ambayo haina polisi na virungu....
!

WaTz wanapenda sana kuandamana ila Katika majaribio yao kulipatikana mabuti na virungu na maji ya washawasha wakanywea na kina
Watanzania hawawezi kuandamana bila ya kuwa na Viongozi. Watanzania hawana hasira na Serikali yao kufika sehemu waseme...tunafanya uasi. Kenya wanafanya uasi kwa sababu ya mambo ya Uchaguzi....na mengineyo waliyoyabandika.
Akwilina walikufa hapo ndo wanachoogopa.
R.I.P Akwilina Na alikuwa mmoja na sio "Walikufa". Jamani mnamtumia sana huyu dada na kampeni zenu mmeshutumu sana Hayati na hili hayupo kujitetea na mmekuwa mstari wa mbele kutoa pongezi, kulikoni?
Haki ya kuandamana tz Iko kwenye makaratasi tu, au kama ni kuunga juhudi ruksa kuandamana mwaka mzima sio kupinga serikali!
Ulitaka haki hiyo iwe wapi? A civil disobedience sio njia ya kutaka katiba. Uandamane ile iwe vipi?
 
Mpinzani huyo

Mpeleke mahakamani

Wewe na nani....hayupo sasa hivi, nini kinachokuzuia kwenda mahakamani?

Hiyo nayo inahitaji katiba mpya? Maandamano?

Na hilo linahitaji maandamano? Kivipi mkuu utueleweshe.


Binafsi ningeanza na aliyesema kuna kulamba asali, aje aseme hilo buyu lipi wapi, zaidi ya hapo ni Msamiati kama misamiati yeyote ile.

Aisee, hayo kwenye list juu hayasimami katika mahakama yeyote ile duniani. Hakuna! Hakuna Mahakama ambayo unaweza kuthibitisha hayo au Kudai kitu chechote kile! Sembuse ziwe sababu za kudai au kubadilisha Katiba. ya Nchi yeyote ile.

Hayasimami kwenye mahakama ya walamba asali lakini si katika mahakama ya wananchi.

Kama hata buyu lilipo hujui Kuna jingine hapa:

Waziri Uweso akisherehea birthday yake nyumbani kwa JK hapa New York, Marekani

Mengine yako Uturuki, UAE, Oman, nk huko.
 
"Katikati ya lindi la yaliyotukuta Kagera, Mola atufanyie wepesi janga hili lituepuke."

Hata hivyo maisha lazima yaendelee.

Kutokea kwa majirani zetu:

Ilikuwa wiki yenye mengi kutokea Jumatatu iliyopita iliyoshuhudia kimbembe cha kufa mtu, pata shika nguo kuchanika.

Miamba miwili kila mtu kwenye ngome yake ikaendelea kujiwinda na kuvurumishiana magoma ya vita.

Upande wa Ruto:

1. Wakatoa miito rasmi kuomba kama vipi wahisani au hata ICC waingilie kati kumtia adabu Baba kwa wanachokiita utoto tundu wake wa kutaka kuivuruga Kenya.
2. Wakavilaumu vyombo vya habari kwa kuyapatia mileage maandamano yale.
3. CAK (kama ilivyo TCRA ya kwetu) ikavipiga onyo kali vyombo vyote vya habari vilivyo ripoti matukio ya Jumatatu.
4. CAK ikapiga marufuku kufanya coverage yoyote kuhusiana na maandamano. Tishio lile lile pendwa la kupokonywa leseni.

"Tangia jana si radio, gazeti au TV ziliweza kusema lolote kuhusu maandamano yaliyopita au yajayo."

Upande wa Baba:

1. Utamu wa harufu ya ukombozi ukawafanya yeye na wafuasi wake kuongeza dozi ya maandamano kuwa 2 kwa wiki badala ya 1.

"Vyuma vikasubiriwa kuumana."

Wadau wengine:

1. Maaskofu wa RC Kenya kwenye mkutano wao rasmi kuhusu mzozo huu, wakatoa tamko kuwataka wawili hao kuridhiana. Yaani maongezi ya ana kwa ana mezani. Maridhiano!

2. Vyombo vya habari vikakimbilia mahakamani haki yao ya kuhabarisha na kina sisi kuhabarishwa vimekiukwa.

3. Mahakama nayo haikufanya ajizi. Kwenye hukumu iliyotolewa Leo, CAK, chali! Hatua zote alizokuwa kachukua ni batili. Magazeti, Radio na TV zikarejea tulipokuwa.

Tulipo sasa tuko square "A". Jumatatu ni D-Day kwa ari mpya, nguvu na kasi mpya.

Jumatatu polisi hawana kisingizio kwani maandamano yatakuwa halali.

"Kenya wenye nchi wananchi!"

Ishukuriwe Katiba yao bora kabisa waliyokuwa nayo.

Tuipiganie Katiba mpya ndugu zangu. Wenye nchi wananchi tunastahili vilivyo bora.

Source: Nation Media
Ndio katiba tunayoitaka.
 
Africa ni shida nadhani hata waliopigania Uhuru hawakujia baada ya Uhuru nini kilitakiwa kufanyika kwasababu nguvu KUBWA walielekeza kupata Uhuru bila kujiandaa baada ya Uhuru watafanya nini.
Sasa imehamia kwenye katiba mpya naamini baada ya katiba mpya hawaelewi nini kitafanyika wengine wanadhani katiba mpya itatatua matatizo yote kumbe Pia itatumiwa na adui kukusumbua NCHI zilizoendelea zina katiba nzuri je,wao wapo salama? Je,wewe ukipewa NCHI utakidhi kila hitaji la mwananchi? Afrika tunasafari ndefu sana. Tuombe Kwa Mungu kizazi kijacho kitoke kwenye Giza hili.

Baada ya katiba mpya nchi itakuwa ya wananchi. Nchi zitaongozwa kwa mujibu wa mahitaji wa wananchi si Kwa mujibu wa matakwa ya walamba asali na wahuni kama Hawa hapa:

Fr_7Zw0WcAAavRN.jpeg


Penye nia pana njia.
 
Back
Top Bottom