ngalelefijo
JF-Expert Member
- Jun 26, 2012
- 3,966
- 2,596
Ndezipanya kindKENYA NI YA WAMCHI, SIYO YA WAJALUO IF YOU PICKET MY SHOP AND STOP ME FROM SELLING MY WARES, YOU ARE GOING TO BE DISENFRANCHISING ME SO THE LAW MST STOP YOU. WHAT HAPPENS IF PEOPLE ANDAMANA KUPINGA WANAONDAMANA AU WANAANZISHA VIKUNDI VYA ULINZI KUJIHAMI NA WAANDAMANAJI, SI NI VITA?
Wakenya wapo mbali sana ukilinganisha na waTz, kwanza raia wa Kenya walio wengi wanafaham haki zao tofaut na waTz, Tz life inakwenda ilimradi tu, Watawala ndio Miungu na wanaweza hata uza Nchi na Raia wasihoji.
Sasa katiba mpya na tume huru ya uchaguzi waliyo nayo wakenya inawasaidia nn?.malalamiko ya uchaguzi hayaishi,
"Katikati ya lindi la yaliyotukuta Kagera, Mola atufanyie wepesi janga hili lituepuke."
Hata hivyo maisha lazima yaendelee.
Kutokea kwa majirani zetu:
Ilikuwa wiki yenye mengi kutokea Jumatatu iliyopita iliyoshuhudia kimbembe cha kufa mtu, pata shika nguo kuchanika.
Miamba miwili kila mtu kwenye ngome yake ikaendelea kujiwinda na kuvurumishiana magoma ya vita.
Upande wa Ruto:
1. Wakatoa miito rasmi kuomba kama vipi wahisani au hata ICC waingilie kati kumtia adabu Baba kwa wanachokiita utoto tundu wake wa kutaka kuivuruga Kenya.
2. Wakavilaumu vyombo vya habari kwa kuyapatia mileage maandamano yale.
3. CAK (kama ilivyo TCRA ya kwetu) ikavipiga onyo kali vyombo vyote vya habari vilivyo ripoti matukio ya Jumatatu.
4. CAK ikapiga marufuku kufanya coverage yoyote kuhusiana na maandamano. Tishio lile lile pendwa la kupokonywa leseni.
"Tangia jana si radio, gazeti au TV ziliweza kusema lolote kuhusu maandamano yaliyopita au yajayo."
Upande wa Baba:
1. Utamu wa harufu ya ukombozi ukawafanya yeye na wafuasi wake kuongeza dozi ya maandamano kuwa 2 kwa wiki badala ya 1.
"Vyuma vikasubiriwa kuumana."
Wadau wengine:
1. Maaskofu wa RC Kenya kwenye mkutano wao rasmi kuhusu mzozo huu, wakatoa tamko kuwataka wawili hao kuridhiana. Yaani maongezi ya ana kwa ana mezani. Maridhiano!
2. Vyombo vya habari vikakimbilia mahakamani haki yao ya kuhabarisha na kina sisi kuhabarishwa vimekiukwa.
3. Mahakama nayo haikufanya ajizi. Kwenye hukumu iliyotolewa Leo, CAK, chali! Hatua zote alizokuwa kachukua ni batili. Magazeti, Radio na TV zikarejea tulipokuwa.
Tulipo sasa tuko square "A". Jumatatu ni D-Day kwa ari mpya, nguvu na kasi mpya.
Jumatatu polisi hawana kisingizio kwani maandamano yatakuwa halali.
"Kenya wenye nchi wananchi!"
Ishukuriwe Katiba yao bora kabisa waliyokuwa nayo.
Tuipiganie Katiba mpya ndugu zangu. Wenye nchi wananchi tunastahili vilivyo bora.
Source: Nation Media
Kuna ukameWakenya sio walamba asali
Andiko zuri la kisomi, great summery... Limegusa maeneo yote Muhimu............
Hadi mwenge wa uhuru uzimwe.Wakenya kwenye kupigania haki zao ni miamba halisi. Hawana muda wa kuchekacheka na kima.
Kuna kitu watanganyika twende sasa tukajifunze kwa wakenya.
Hadi mwenge wa uhuru uzimwe.
Tuipiganie Katiba mpya ndugu zangu. Wenye nchi wananchi tunastahili vilivyo bora.
Rais Samia, angalia hela za TANAPA zinavyopigwa. TAKUKURU na CAG wanakusaidia nini?
BARUA YA WAZI KWA RAIS WA JMT, MHE. SAMIA SULUHU HASSAN. Kwanza kabisa pongezi kwa kazi nzuri ambazo unaendelea kuwafanyia Watanzania katika kila sekta, ikiwamo hii yetu ya uhifadhi na utalii. Lakini hapa kwetu TANAPA bado tuna kilio cha siku nyingi ambacho hakifanyiwi kazi, labda kwa makusudi...www.jamiiforums.com
Cha moto anakiona je kama:
1. Maandamano ni halali?
2. Live coverage ya media ni guaranteed?
3. Mahakama ni huru hakuna kucheza faulo?
4. Wenye nchi ni wananchi?
Ruto anapumulia machine.
Lengo si kumtoa madarakani. Kuna mambo hataki kuwasikiliza. Kama hataki kuwasikiliza njia zingine halali ndiyo hizi sasa.
"Kwanini wasimtoe sasa kwa mujibu wa katiba kama hafanyi anayopaswa kufanya kwa mujibu wa katiba?"
Maana kamili ya wenye nchi wananchi.
Akili zako mbona ndizo za ku copy na ku paste mkuu?
Wewe hujui kuwa katiba ya Kenya ni bora zaidi kuliko yetu? Hujui ya South Africa ni Bora kuliko yetu?
Au hata hujui vigezo vya kutambua ubora wa katiba?
Au ninyi ni wale ambao mkisikia katiba mpya mnapatwa na msongo mawazo?
Kaeni kwa kutulia msiyoyataka hayana muda mrefu bado.
Kuna wanaopewa viroba pombe bangi na mirungiKwani kuna wanaopelekwa kuandamana kwenye mafuso au kulipwa posho?