Rwanda wamepiga marufuku "Adhana" Alfajiri

Mbona wakati anapitisha sheria ya kuwabana WaKristo hatukuona hoja yako hii ya ubaguzi wa kidini?. Mfano
1. Ni marufuku kulala na kuamka kwa Mkristo kisha kesho yake kujiita nabii au mtume mwenye kumiliki kanisa X bila kuwa na angalau shahada ya Theologia

2. Marufuku makanisani kutumia viongeza sauti wakati wa ibada zao maana ni kelele kwa wengine.


Niishie hapo, usije na hoja nyepesi kuwa Kagame ana ubaguzi wa Kidini bila kuwa na mifano anuai.

PK hana shida kama hao ndugu zetu wanaobagua wenzeo huko visiwani kisa tofauti za kiimani. Yeye moja ni moja kwa wote
 
Saudi Arabia pia, walishakataza Adhana saa 10:50 usiku washaanza makelele, yaani kero kuu, yaani ni kero kubwa, watu hawalali, ni makelele utafikiri miji ya matarumbeta. Ni kero sanaa sanaa.


 
Bado sisi sasa
 
Huku kwetu iwe viseversa makanisa na hizi ministry baadhi kwa kweli mnaboa sana haiwezekani uwalazimishe watu kusikiliza mambo yako hata kama ni mahubiri kila mtu ana haki ya kupata utulivu makelele saa nane za usiku sijui kuna ibada ya kufungua vifungo mnasumbua watu buree Ningeshauri Serikali Mama kama unapita hapa piga marufuku matumizi ya Speakers kubwa kwenye makazi ya watu mnaboa mno WATUMISHI NA MITUME MJIHESHIMU TAFADHALI[emoji122]
 
Sipingi madhumuni ya adhana. Tatizo ni kule kuhusisha wale wasiohusika. Kama ujirani wote ungekuwa ni Waislamu pekee, hapo ingekuwa sahihi kuwachokonoa wale Waislamu kaidi au dhaifu wanaotaka kuendelea kuvuta shuka. Hizo "spiritual admonitions" zitakuwa zinamfika mlengwa na hazimsumbui asiyehusika anayetaka ku-maximize usingizi wake kabla ya kuamka kwenda kupambana na mahitaji ya maisha. Kwa vitu ambavyo haviwezi kutekelezwa msikitini, njia mbadala itafutwe ya kuwafikia walengwa ambayo siyo kero kwa wasiohusika. Kwa mfano, mchana unaofuata ujumbe unaweza kutumwa kwa hao wakaidi ukiwakanya wanayofanya na kuwataka waongoke. Mradi tu asiyehusika habugudhiwi. Kwa maneno ya Rais Mstaafu Mwinyi, "Mbebaji hatabeba mzigo usiomhusu".
 
Hii habari ya 2018 na sio misikiti tu mpaka makanisa yamefungwa
 


Wewe unamsifia Dikteta!!??.
Ni ujinga kuingiza udikteta katika masuala la imani, imani imo moyoni mwa watu.

Adhana ya kiislamu ni nasaha ya kiimani pia mbali na wito wa kuwajulisha watu muda wa swala.

Kupinga utolewaji wa adhana ni kupinga mafundisho ya dini ya kiislamu, adhana haijaanza leo, imeanzishwa na mjumbe wa Mungu Mwanzilishi mtukufu wa Dini ya kiislamu Mtume Muhammad (saw), hivyo kwa maneno mengine kuzuia utolewaji wa adhani ni kupingana na takwa la Mungu kwa mujibu wa Uisilamu.

Tutakaa hapa tukibishana na kuvutana bure na hatutafikia suluhu ila ninachokueleza ni hichi;--

"Kama adhana ni maagizo na maneno ya Mungu na Kagame au yeyote katoa maamuzi ya kuzuia maneno hayo yasitamkwe inavyopaswa ni kiumbe wa Mungu basi Mungu mwenyewe ndiye hakimu"

Tutarudi hapa na tutajulishana matokeo tuombe Mungu atupe uhai tu.
 
Mathayo 6 : 6 Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.

7 Nanyi mkiwa katika kusali, msipayuke-payuke, kama watu wa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi.
 
Baltimayo kwenye Bibliia alisali kwa kupiga makelele miyowe Yesu mwana wa Daudi unirehemu .Maombi yake yakasikilizwa na Yesu akamponya
 
Sioni msingi wa kusumbua watu wengine Kwa makelele Kwa interest ya dini Moja!Uhuru wa mtu unapoishia ndipo wa mwingine unapoanzia!
Inaweza kuwa justified within community ya waislam pekee!
 
Sioni msingi wa kusumbua watu wengine Kwa makelele Kwa interest ya dini Moja!Uhuru wa mtu unapoishia ndipo wa mwingine unapoanzia!
Inaweza kuwa justified within community ya waislam pekee!


"Uhuru wa kutoa adhana nk, unapoishia ndipo uhuru wa wengine unapoanzia", ----you are right and that's the best way to put it.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…