Rwanda yatuma majeshi yake mpakani na nchi ya DRC Congo, yasema iko tayari kwa vita!

Rwanda yatuma majeshi yake mpakani na nchi ya DRC Congo, yasema iko tayari kwa vita!

Gari la walinda amani huko Congo(MONUSCO) lilianguka,likakutwa na magunia ya mchanga wa madini.

Hivyo ndivyo MONUSCO wanavyolinda amani huko Congo.View attachment 2403378
Hivi viroba vinajazwa mchanga na kuweka kwenye gari hizo za mapigano ili ikitokea limekanyaga Bomu la ardhini basi asikari na vifaa vikivyopo ndani hawapati madhara makubwa na zile fragmentation (vipande au chembechembe za chuma) za Bomu na sio madini kama unavyotaka kupotosha.
 
Hivi viroba vinajazwa mchanga na kuweka kwenye gari hizo za mapigano ili ikitokea limekanyaga Bomu la ardhini basi asikari na vifaa vikivyopo ndani hawapati madhara makubwa na zile fragmentation (vipande au chembechembe za chuma) za Bomu na sio madini kama unavyotaka kupotosha.
Danganya Toto jinga masikio Kama Popo.
 
Tanzania has strong ties with DR Congo, in case Rwanda wakaishambulia Congo there will be no hasitation kwa Tanzania kutuma msaada kwa Congo. Kama tuliweza kuwafurumusha M23 kipindi kile na kuharibu mahusiano ya kidiplomasia kati yetu na Rwanda, this time wacha ijirudie kwakuwajumlisha na jeshi la Rwanda lililopo mpakani.
 
Zama za VIJANA wa nyerere kuwaaachia Madaraka vijana walio na damu CHANGA umefika

Muhoz kaneirubaga na Ivan kagame wanafaa Sana!!

Mawazo HURU

"Mbona wakati wa joseph kabila akiwa kitalani hakukuwa na hizo!!?

Ina Maana alikuwa na genleman agreement na na pk!?

Kwa Hiyo felix tshesekedi kapiga u-turn kinyume na makubaliano yake na kabila junior!!?

Kama tshesekedi hana backup kutoka mataifa mama ya ukanda huu asije angukia pua kutoka kwa jasusi mkongwe wa enzi na enzi Pk!!

Matokeo ya hizi kelele zitatoa mwelekeo Mpya wa ukanda huu!!

Mkuu

Hopefully hii kitu iko GRANTED

Kabla ya hizi mambo zote alikuwepo hapo
 
Kuwe na madini hao walalahoi wayaangalie tu hawana shida nayo? madini gani Kwa uwingi huo wa kwenye viroba hayana hata ulinzi? Wewe ndio unadanganya watoto wasioelewa.
😄😄 basi Kumbe hata kusema Rwanda& Uganda inaiba madini Congo Ni uongo,maana wanaibaje wkt Walalahoi wanaangalia tu Kama vile hawana shida nayo 😄😄
 
Rwanda imetuma wanajeshi kwenye mpaka wake na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, saa chache baada ya DRC kumfukuza balozi wa Rwanda kwa madai ya DRC kwamba serikali ya rais Paul Kagame inawaunga mkono waasi wa M23.

Msemaji wa serikali ya Rwanda, Alain Mukurarinda amesema kwamba “wakiamua kutangaza vita dhidi ya Rwanda, nasi tupo tayari kuchukua hatua kali, maana hata sasa wanapoendelea kuchukua hatua kama hizo, haina maana kwamba Rwanda imelala usingizi mzito.”

Taarifa ya Serikali ya Rwanda ilisema kwamba ‘inasikitishwa na hatua ya DRC kumfukuza balozi Vincent Karega.”

Taarifa hiyo imeendelea kusema kwamba “wanajeshi wa Rwanda wameimarisha usalama kwenye mpaka na DRC na wanaendelea kufuatilia hali ilivyo nchini DRC” kufuatia mapigano makali kati ya waasi wa M23 na wanajeshi wa Serikali.

Baraza la ulinzi la DRC linaloongozwa na Rais Felix Tshisekedi, lilimuamuru balozi wa Rwanda kuondoka nchini humo ndani ya muda wa saa 48, kufuatia ripoti kwamba Rwanda ilikuwa imetuma kikosi maalum cha kijeshi kuwasaidia waasi wa M23 katika sehemu za Kivu Kaskazini, Mashariki mwa DRC.

Ripoti za DRC pia zinadai kwamba Rwanda imetuma wanajeshi katika wilaya ya Rubavu, mpakani na DRC kuwasaidia waasi wa M23.

Rwanda imekuwa ikikanusha kila mara, ripoti za kusaidia waasi wa M23 na kusisitiza kwamba kinachoendelea DRC ni swala la usalama wa ndani ambalo lazima lishughulikiwe na serikali ya Kinshasa.

Madai ya serikali ya Rwanda
Rais wa Rwanda Paul Kagame

Rais wa Rwanda Paul Kagame
Katika taarifa kwa vyombo vya habari, msemaji wa serikali ya Rwanda amesema kwamba “ushirikiano unaendelea kati ya jeshi la DRC na waasi wa FDLR, na jaribio lao la kulenga sehemu za mpakani na Rwanda kwa mashambulizi na kueneza habari za chuki kuhusu Rwanda.”

Rais wa DRC Felix Tshisekedi Tshisekedi ameamuru maafisa wa usalama kuhakikisha kwamba raia wa Rwanda wasiingie DRC, huku Rwanda ikitaka raia wake kutokwenda DRC.

“Mimi kama msemaji wa serikali ya Rwanda, nawashauri raia wa Rwanda kufikiria mara mbili kabla ya kuingia DRC,” amesema Alain Mukurarinda, msemaji wa serikali ya Rwanda.

Tshisekedi anatarajiwa kulihutubia taifa kuhusu uhasama kati ya DRC na Rwanda na mapigano ya M23.

Hivi karibuni, Tshisekedi alifanya mabadiliko makubwa katika uongozi wa jeshi la DRC na kutuma idadi kubwa ya wanajeshi na silaha katika sehemu za Kivu Kaskazini, kupigana na kundi la waasi la M23.

Mashambulizi ya M23

Wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa walijeruhiwa Jumamosi kutokana na shambulizi la kundi la waasi wa M23 katika sehemu ya Kiwanja, Rutshuru, Kivu Kaskazini.

Waasi wa M23 wamekataa kuondoka mji wa Bunagana licha ya viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuwataka kuondoka sehemu hiyo na kuacha mapigano.

source: Voice of America
Rwanda ITAENDA kupigwa mgoma na kufutika in 7days yani pu pu mchezo umekwisha
 
Madini gani wkt alipotoka tu Huku kufika Congo tu wanajeshi wake wamepewa kichapo heavy mpk eneo lao jingine likachukuliwa,ili kuficha aibu na kubadili upepo wa kisiasa Tshisekedi akaona amfukuze huyo balozi.Akikaa Vibaya na Goma itachukuliwa.

Congo Ina tatizo la Uongozi,Hakuna Uzalendo kwa nchi Yao,Rushwa etc

Yaani maeneo yako yanachukuliwa na waasi Muda huo rais Yuko na viongozi wake Kinshasa(Stampede) kwny shoo kubwa ya fally Ipupa wanakula zao Maisha.

A Failed State.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Wakuu ni kwamba kagame kashindikana kabisa au ni nchi hazijaamua tu kumvalia njuga?
Ziamue mara ngapi? [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Wangeamua mda tyuuh, ila wanaogopa kichapooooo.
 
EAC imejaa marais wanafiki sana. Wakienda Congo wanaongea hivi wakienda Rwanda wanaongea vingine.

Hawana uchungu na Wacongo wanaoteseka. Hivi Museveni au Samia wana uwezo wa kumuonya Kagame?! Never!
Wao wacongo wajikomboe wenyewee, kutwaa kujichubua na kukata viuno, mbna bado watachapika had akili iwakae vyema.

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Congo watrain snipers waingie kwa huyo paka shume wahakikishe wanafahamu ratiba zake wakimlenga akapotea basi na amani ya Congo itapatikana siku hiyo.

Silaha wazi disassemble leo inavuka triger, kesho magazine hadi vitimie wamlie timing wamu eliminate ashakuwa shida huyu.
 
Kosa walilofanya ni kumpa Kabarebe awe Chief of Staff Congo baada ya kumpindua Mobutu na kumuweka Kabila.
Intelijensia yote Congo Rwanda wanayo mkononi ndo mana wanajiamini
 
Back
Top Bottom