Saa 11:20 alfajiri unapishana na schoolbus zenye watoto wa miaka 4

Kuna hawa pia wa darasa la nne nao ni mateso tu. Wanaambiwa waripoti shuleni saa 12 asubuhi kila siku. Wanarudi nyumbani saa 11 jioni halafu wanarudi tena shuleni saa 12 jioni mpaka saa 3 usiku kila siku. Jumamosi pia wanaenda.
Hivi mtoto wa darasa la nne anasoma nini muda wote huo?
Elimu imekuwa mateso kwa watoto kisa shule zinatafuta sifa za kuonekana zinafaulisha zinabaki kukaririsha watoto.
 
Baba zenu walioa mama zenu wakawa wa mama wa nyumbani wakawasimamia nyie mkaenda shule mkarusi mkakuta chakula, mkapata mda mkaenda kucheza mkajumuika na ndugu na jamaa kwenye shughuli mbali Ile nyie Sasa Leo maisha kusaidizana mnataka kuzaa uku malezi mnawachia wadada wakazi na makonda wa school bus maana mama anamkaa saa kumi baba hivyo hivyo na mkitoka kazini hamuendi nyumbani mama anapita bar baba naye hivyo hivyo

Matokeo yake watoto wanakuwa na tabia mbaya pamoja na kusoma shule nzuri ila wanaishia pabaya ebu nenda uswahili au vijijini kama utakuta mtoto kundi kubwa la mashoga au wasagaji au watumia unga
 
Kwenda shule sio ishu kama ni 3yrs ishu shule isiwe mbali na eneo mnaloishi,wangu ana 3yrs anasoma jirani na nyumbani basi linamfata saa 1 na 30 asubui!
Anakua ashaamka mwenyewe mida hiyo wala haamshwi awahi basi
 
Huu ni ujinga
 
Kuna shule huku inafosi mtoto darasa la nne akae shule kama mzazi hutaki umpeleke mwanao saa 12 asubuhi kasorobo awe shule na kutoka saa mbili usiku.
 
Watu wanafanywa fursa bila kijijua. mmoja aliniambia hana mtu wa kumwachia watoto akienda kazini. Nikamwambia ni cheap kumwajiri mwalimu mmoja aje kucheza na watoto nyumbani kuliko kuwapeleka day care.
Ni kutesa watoto tu
 
Mama d wa ukweeee
Mama mwenye busara zake
Nmekubali
Si umeona ulivyoshusha nondo

Ova
 
Kuna shule huku inafosi mtoto darasa la nne akae shule kama mzazi hutaki umpeleke mwanao saa 12 asubuhi kasorobo awe shule na kutoka saa mbili usiku.
Darasa la nne? Kwanza hata huo mtihani wa darasa la nne ni kupoteza pesa na kusumbua watoto. Hauna maana yeyote ile. La nne mtoto bado ni wa kubembeleza aipende shule sio kumpa ratiba kama anasomea rocket science.
 
Darasa la nne? Kwanza hata huo mtihani wa darasa la nne ni kupoteza pesa na kusumbua watoto. Hauna maana yeyote ile. La nne mtoto bado ni wa kubembeleza aipende shule sio kumpa ratiba kama anasomea rocket science.
Changamoto sana
 
Uko sawa 100% Mama D. Mtoto wa miaka 4 unamwamsha kwa alarm? Huyu anatakiwa alale mpaka aamke mwenyewe usingizi unapomwisha.
Kuna haja ya waalimu kuanza kuspecialise kwenye private schooling kwa watoto. Watapata sana watu
 
Tabata kuna shule nzuri kibao mf Tusime, St Mary, Crist the King,Reminant nk na bado kama ikiwezekaa unampeleka Loyola ambayo ipo Mabibo, kwani Mabibo na Tabata ni pua na mdomo.

Sometimes ni show off na ujinga ujinga.
 
Hakuna kitu kinanikera kama kumwamsha mtoto saa 11 alfajiri, unawahi nini? Masaa mawili ya alfajiri?

Mtoto aamke saa moja kamili asubuhi, then muda wa kuondoka shule kurudi nyumbani ongeza masaa mawili.
 
Point.
Sent from my SM-G610F using JamiiForums mobile app
 
Uko sawa 100% Mama D. Mtoto wa miaka 4 unamwamsha kwa alarm? Huyu anatakiwa alale mpaka aamke mwenyewe usingizi unapomwisha.
Kuna haja ya waalimu kuanza kuspecialise kwenye private schooling kwa watoto. Watapata sana watu

Wazazi wanazaa halafu hawataki kulea, wanajidai wanapeleka watoto shule ila sio kweli! Wanachofanya ni kuwanasukumia watoto kuepuka majukumu ya malezi

Kuna wakati unakuta vitoto vidogo miaka 2 na nusu, 3, 4, 5 boarding au kwenye school bus alfajiri unapata huruma hadi unatamani kumwomba Mungu awanyime wazazi wao hiyo pesa ya kuwapeleka huko.

Ukisikia pesa inakutumia badala ya wewe kuitumia ndio hapo
 
Kwa nini tusiwe na hulka ya kuboresha shule zilizopo karibu na mazingira yetu, hii tabia ya kuamsha watoto saa 11 sio poa hata. Mtoto aamke 12, aandaliwe vizuri hadi saa moja aende shule akiwa fresh.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…