Saa 11:20 alfajiri unapishana na schoolbus zenye watoto wa miaka 4

Saa 11:20 alfajiri unapishana na schoolbus zenye watoto wa miaka 4

Nina ndugu yangu yeye mwalimu ana hali ngumu sana ila anafyatua watoto kama ana kiwanda cha kufyatua matofali..ana watoto 5 na mtoto wa kwanza ana miaka 9 anamsomesha shule ada 1.2M kwa mwaka primary na mtoto kilaza vibaya...nimemshauri sana kuhusu hela anazotupa ila nagundua ni limbukeni basi namuacha tu.
 
Uyo Nae ni limbukeni wa elimu
 
Sio sasa! Sio sawa! Ila hakuna wa kukataza kwa kuwa itazuia dili, na wakusemea hawapewa dili.
Ni uvunjaji wa haki za watoto.
Watu wa Haki za Binadamu wapo bize kuandaa ya machapisho, makongamano n.k kutetea USHOGA NA USAGAJI.
Wazazi hawawataki watoto waliwatafuta/kuwaomba
 
Tuwaulize wazazi wao maana wapo humu
 
Kwa hali ya sasa jinsi ilivyo ya malezi ya watoto yatupasa tubadilike na kurudia baadhi ya yale malezi tuliyoyapata sisi kutoka kwa wazazi wetu.

Binafsi sitaki kabisa kutesa wanangu eti shule aamke saa kumi na moja alfajiri na nyumbani arudi saa tatu usiku au akakae bweni hiki kitu sikubaliani nacho kabisa.

Tazama watoto wa miaka hii kiakili wanamapungufu fulani kisa kukaa sana shule na hata uelewa wao haupo sawa kwenye kutatua mambo madogo madogo lakini ukiona jinsi walivyosoma mpaka unashangaa huku kafikaje!!?

Usasa umekuja kuharibu sana malezi kwa watoto wetu na sijui kama watu wameshafikiria miaka 30 ijayo kutakuwa na taifa la watu wa aina gani.

Nipo wilaya moja huku kanda ya ziwa naona watoto wanatoka saa tatu usiku yaani mpaka namuuliza mwenyeji wangu hivi hawa watoto wote wanasoma darasa la nne na saba wakati wengine ni huenda darasa la kwanza na lapili.

Kiukweli watoto wa miaka hii wazazi tunawatesa na huu usomaji wa adhabu namna hii.
 
Mimi niliwahi kuwakuta, nadhani ni sa10 ile alfajiri kuenda 11.. Walinigaia lifti nilikua naenda mbali kidogo na ni usiku... maswali yangu nilibaki nayo kichwani nashangaa tu
 
Jamiii ya kimasikini inaishi kwa shida sana..
Haya yote ni matokeo ya umasikini na ujinga.
Tunapata viongozi wajinga na mfumo wa kijinga matokeo yake nikuzalisha jamii ya kijinga.

Suala mtambuka
 
Waziri Elimu, Sayansi Na Teknolojia Yupo
Katibu Wa Wizara Yupo
Afisa Elimu Mkoa Secondary, Msingi Yupo
Afisa Elimu Wilaya Secondary, Msingi Yupo
Mratibu Elimu Kata Yupo

In Jiwe Voice!!!
 
Jamiii ya kimasikini inaishi kwa shida sana..
Haya yote ni matokeo ya umasikini na ujinga.
Tunapata viongozi wajinga na mfumo wa kijinga matokeo yake nikuzalisha jamii ya kijinga.

Suala mtambuka
Ndiyo Ukweli Wenyewe
Nasema Uongo Ndugu Zangu
 
Imekaaje hii?

Saa 11:20 alfajiri unapishana na schoolbus zimebeba wanafunzi wadogo wa miaka 4-6 wakipelekwa mashuleni. Unabaki unajiuliza maswali mengi sana kichwani,
  • Hivi Hawa watoto wameamshwa saa ngapi?
  • Hivi Hawa watoto wameandaliwa kwa MDA gani?
  • Hivi Hawa watoto wamekaa vituoni kusubiria school bus kwa MDA gani?
Wazazi, waalimu,Serikali, jamii na wahusika wote wa Hizi DAYCARE na PRIMARY SCHOOLS mnaofanya hivi mjitafakari sana kwa hili.

HAIINGII AKILINI KABISA

Mm nilikua nawaamsha saa 10 au kumi na nusu usiku
Wanajiandaa na kupata breakfast hadi saa 11 au kumi na moja na nusu
Tunaelekea kwenye basi linawachukua 12 :45 kuelekea shuleni
Wanarudi home saa 11 au saa 12 jioni wanafanya home work kama wanayo
Kama hawana wanangalia TV mpaka saa 2 usiku alafu wanaenda kulala
Lkn ni lazima saa 1 kamili usiku wawe wanakula chakula cha usiku ili ifikapo saa 2 usiku waingie kulala.
Hiyo ni Jumatatu hadi Ijumaa.
Jumamosi na Jumapili usafi binafsi na kurelax kuangalia TV au kufanya homework km ipo au kulala mchn km atapenda au mtoko km upo.
 
😁😄😃
 
Mfumo mbaya wa elimu unaharibu watoto,,, mkuu ukipata pesa mpeleke mtoto international school tena za mtaala wa international Baccalaureate

Hapa Tz ni shule ngapi zenye huo mtaala wa IB?
Mikoa ya kanda ya ziwa na kusini ipo shule yoyote inayotoa elimu kupitia mtaala wa IB au wewe unazungumzia Dar es salaam peke yake?
 
Sasa ss tusio na ajira serikalini tule wapi?? Huo ndio urefu wa kamba yetu acheni tule.
Mzazi kapenda shule iko tabata, yeye anaishi kigamboni sasa kosa ni la mzazi ama nani, acha wazoee shida tangu utotoni watafute njia mbadala wakikua
 
Hapa Tz ni shule ngapi zenye huo mtaala wa IB?
Mikoa ya kanda ya ziwa na kusini ipo shule yoyote inayotoa elimu kupitia mtaala wa IB au wewe unazungumzia Dar es salaam peke yake?
Mwanza ipo shule inaitwa Isamilo International inafundisha huo mtaala
 
Back
Top Bottom