Saa 11:20 alfajiri unapishana na schoolbus zenye watoto wa miaka 4

Saa 11:20 alfajiri unapishana na schoolbus zenye watoto wa miaka 4

Daycare sawa, hata saa kumi na moja waje wamchukue mtoto niwahi kazini au nam drop center nikiwa nawahi foleni. Huko wana vitanda na hulala, huogeshwa, kulishwa, kucheza na kusoma kidogo maana mtoto wa miaka mi3 bado hata haelewi shule ni nini. Jioni nikimpitia au wakimleta nikiwa home tayari hatakama ni saa moja usiku. Mnaopinga Daycare mna house maids wazuri au mmeamua kujitoa muhanga, au mnawatu wa kuwaachia watoto nyumbani au bado hamna watoto au tayari ni wakubwa. Ila zinasaidia sana
Ndio najiuliza hawa wanaolalamika wana watu wa kuwaachia sio bure ila kama bado hawajazaa waache kabisa maana yajayo yanafurahisha
 
Mie naona hawa watu wa haki za binadamu hawafanyi kazi yao. Wamekalia ushoga baadala ya kuwatetea wototo. Sasa mtoto wa miaka minne saa kumi na moja anaenda shule kufanya nini? Kuwatesa tuu watoto.
Shule anafika saa 2 mkuu
 
Huu upuuzi niliukuta wakati dogo aanza Grade 1. Saa 11.30 gari inampitia halafu shule ipo km 10 tu kutoka home. Nikaongea na wazazi kadhaa wakaniambia hawana jinsi ndio utaratibu. Mbishi nikaingia front,nikatafuta wazazi 20 tukatishia kuhakisha watoto. Leo hii gari inapita saa 1 asbuhi shule ileile
Ulifanya Jambo jema Sana, Unapaswa kua mfano Bora kwa wazazi wengine[emoji4][emoji106]
 
vikifika darasani hamna kusoma zaidi ya kusinzia

na mwl akimuona anasinzia anakapitisha tufimbo twa mgongo

ndo mana kizazi cha sasa kina vichwa vigumu
 
vikifika darasani hamna kusoma zaidi ya kusinzia

na mwl akimuona anasinzia anakapitisha tufimbo twa mgongo

ndo mana kizazi cha sasa kina vichwa vigumu
Kuna mdau kasema,
Ndo kizazi hiki kitakuja kutiletea wabunge vilaza was kulala bungeni maana utotoni mwao walilimbikiza Sana usngz.
 
Sasa tutawasaidieje? Maana maamuzi ni yao sie ni kiherehere chetu kuwaonea huruma watoto ambao wazazi wao ni wapumbavu na hawana akili
Sahii kabisa, hoja ijibiwe kwa hoja[emoji106]
 
Shule anafika saa 2 mkuu
Ila anafika kashachoka kinoma na amekosa usingizi ule mtamu. Kwanza mtoto wa miaka minne anatakiwa akurume sarakasi huko na kukimbizana na wengini....tuna watreat watoto kama adults which they are not. Wacha wacheze walale wavunje mikono wacheze mama na baba, tule tumbakishe baba...huo ndio utoto.
 
Ni ujinga uliopitiliza kwa mzazi kumwamsha mtoto wa chini ya miaka 6 saa 11 alfajiri.

At least saa 12 it's fair ingawa nayo ni kumtesa.

Wazazi wengi tunafikiri elimu ya mtoto wa chini ya umri wa miaka 10 ina umuhimu saana kumbe tunajazana ujinga mtupu.
 
Wazazi wengi tunafikiri elimu ya mtoto wa chini ya umri wa miaka 10 ina umuhimu saana kumbe tunajazana ujinga mtupu.
Chini ya miaka kumi ndio hasa mtoto anahitaji msingi bora wa elimu.
 
Kwa hiyo unamtafutia shule kimara wakati wewe unaishi Tabata ?

Wewe baba yako alikuamsha saa 11 kila siju kwenda shule ?
Ndiko alikopata nafasi. Afanyeje sasa.
 
Kwa hiyo unamtafutia shule kimara wakati wewe unaishi Tabata ?

Wewe baba yako alikuamsha saa 11 kila siju kwenda shule ?
Enzi zetu sisi hakukuwa na mashule hayo ya alfajiri.
 
Watoto under 10 waamke saa 12 na nusu.
.maandalizi 30 min...shuleni saa 1 na nusu.

Nje ya hapo mzazi ujue unamtesa mwanao..ulitambue hilo.
Hili sasa ni la shule husika. Kumbuka shule nazo zinapunguza gharama. Haziwezi kuwa na ruti ya watoto wa saa 11...waje wa saa 12.. waje wa saa 2.. utafunga shule...na hutalipa mishahara.

Hili suala ni mtaambuka!!😇🧐🤔🤷
 
Back
Top Bottom