Dogo nisikilize mimi hapa.
Kamwe usimhukumu mtu bila kuwa na uhakika wa jambo unalomtuhumu nalo. Nilikuwa kama wewe kipindi fulani. Binti wa watu asipojibu hata texts zangu tu kwa wakati naumia sana na kupata mawazo mabaya. Na kuna jamaa walikuwa naye karibu sana; nikamhukumu kwamba alikuwa anatoka naye. Siku moja nilichukua simu yake ndipo nilikaujua ukweli na niliishia kuona aibu sana. Nilichojifunza ni kuwa na open communication...na kuambiana ukweli hata kama ni ukweli unaouma namna gani!
Nasisitiza tena. Kamwe usimtuhumu mtu bila kuwa na uhakika. Kama kuna jambo una wasiwasi nalo muulize. Usiporidhika na jibu lake fanya uchunguzi na kama anakuchiti mwishowe utajua tu maana mapenzi kamwe huwa hayafichiki.
Na unapoanza kufanya uchunguzi wako uwe umejiandaa kisaikolojia hasa kama unampenda sana. Je, ukikuta ni kweli anakuchiti una kifua cha kuweza kumuacha maana sasa hivi ni tuhuma tu lakini tayari kuna kitu kinakuniga. Vipi ukikuta kweli jamaa wanamtindua huko? Kama huna kifua cha kumuacha basi acha hata usimchunguze.
[emoji3591][emoji3591][emoji3591] By the way, unafikiri kuchapiwa kunaepukika, hasa siku hizi - tena kwenye long distance relationship kama yako? Wewe huna demu mwingine? [emoji2221][emoji2221][emoji2221]
View attachment 2987421