CCM bhana sijui akili walishazipeleka wapi? Mahera anadai majina ya covid 19 yaliletwa na chadema ndio hayo aliyoyapeleka kwa Ndugai.
1. Mahera anadai CHADEMA iliwasilisha hayo majina tarehe 19 November 2020. Tarehe 20 Nov 2020 huyohuyo Mahera akiwa Azam tv alidai tume haijapokea majina ya viti maalumu kutokea CHADEMA. (Angalieni hizi tarehe mtaona nani muongo). Wanasema ukiwa muongo jitahidi uwe na kumbukumbu maana hii ni aibu.
2. Nusrat Hanje: tufanye basi ni kweli Mahera anasema ukweli kuwa Chadema iliwasilisha majina ya viti maalumu. Swali la kujiuliza: Nusrat Hanje alikuwa mahabusu, Chadema wana mamlaka gani nchi hii ya kuweka jina la Nusrat kwenye orodha ya viti maalumu na kuhakikisha wanamtoa mahabusu ili akaapishwe? Hapa ndio ninapowaona ccm either walishatuona watanzania hatuna akili au wao ndio hawana akili. Chadema ina mamlaka gani ya kumtoa mwanachama wake mahabusu ili awahi kuapishwa?
Ushauri wangu kwa chadema. Fungueni kesi mahakamani. Hii kesi ni rahisi sana kushinda. CCM imepanga huu mchezo kiboya sana.
Tunashukuru Nusrat Hanje ametoka mahabusu. Sasa dada wa watu yupo huru.