Saa ishirini na nne za Nusrat Hanje kutia doa Mihimili mitatu ya Nchi

Saa ishirini na nne za Nusrat Hanje kutia doa Mihimili mitatu ya Nchi

Lumumba kumejaa nyumbu!!
Ni kweli CCM ni nyumbu kwani hata mbugani nyumbu ni wengi kama CCM ndiyo maana CCM ya sasa inaongoza kwa kufanya vitu vya hovyo pasipo kutafakari kabla, ebu jiulize katiba mkuu wa CCM ana phD lakini anapokea ushauri wa cyprian Musiba na akina Le mutuz kubwa jinga unategemea nini hapo?
 
Kimewavua hadi chupi
Sasa nasikia makanda wa CCM hasa wale wakware akina Nape Ndungai kibajaji na wenzao wamejipatia michepuko mipya tokea kwenye hiyo list ya covid 19 , sasa ni mwendo wa Mapenzi kisha kupanga njama za kuidhoofisha chadema badala ya kutumia hizo pesa za walipa kodi kuleta maendeleo
 
Huwa wanatumia uji kufikiri Hawa jamaa, wametuaminisha wapinzani wanapinga maendeleo wapinzani wanachelewesha maendeleo Leo wamebakia pekee yao ajabu wanatumia tena nguvu kubwa kulazimisha wapinzani waingie bungeni hapa tuwaelewe vipi nn wanataka.
Pesa inayotumika CCM kulazimisha kupendwa kwa nguvu na pia kuhujumu kudhoofisha chadema na upinzani kwa ujumla ni pesa nyingi mno ni matumizi mabaya ya pesa za walipa kodi, CCM hatataki kuwekeza kwenye maendeleo wapate kura pasipo kudidimiza demokrasia badala yake wamewekeza kwenye kukandamiza demokrasia kwa gharama kubwa ili iwe sehemu ya wajanja madalali wa siasa huko CCM kupiga 10% kiufisadi, hizo mbinu za kuua upinzani ni Dili zao za kujipatia pesa toka kwa mtukufu kwa njia haramu za kishetani
 
Tatizo CCM ni waongo halafu hawana kumbukumbu. Wao walishawahi kumfukuza mbunge Zanzibar kisha akina Sophia Simba na Bernad Membe lakini leo wanaiandama CHADEMA kwa kuwaondoa wahuni
 
Tatizo la hawa ccm hawajui hesabu. Wanapenda namba ila hesabu hawajui.
Dili jipya la kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu huko CCM ni kuchukua pesa kwa kisingizio cha kurejesha mfumo wa chama kimoja hapo ndipo madalali wa siasa hupiga pesa ndefu tokea kwa mtukufu, wamegundua kuwa mtukufu hataki kuona upinzani unakua ndiyo maana wamemgeuza fursa ya kupiga pesa
 
Toka lini wasomi wa maganda ya korosho wakaaminika?
Filamu za ovyo nchi hii huwa haziishi.Hii ni nyingine tena,tena waongozaji hawajataka ata kuihariri angalau itizamike kwa wenye akili timamu.Alafu walioifanya ni wasomi kabisa wa nchi hii.Kuna mambo ukiyaangalia vizuri unaweza kuona hii nchi nikama bado tuko kwenye ukuaji kifikra.
 
CCM bhana sijui akili walishazipeleka wapi? Mahera anadai majina ya covid 19 yaliletwa na chadema ndio hayo aliyoyapeleka kwa Ndugai.

1. Mahera anadai CHADEMA iliwasilisha hayo majina tarehe 19 November 2020. Tarehe 20 Nov 2020 huyohuyo Mahera akiwa Azam tv alidai tume haijapokea majina ya viti maalumu kutokea CHADEMA. (Angalieni hizi tarehe mtaona nani muongo). Wanasema ukiwa muongo jitahidi uwe na kumbukumbu maana hii ni aibu.

2. Nusrat Hanje: tufanye basi ni kweli Mahera anasema ukweli kuwa Chadema iliwasilisha majina ya viti maalumu. Swali la kujiuliza: Nusrat Hanje alikuwa mahabusu, Chadema wana mamlaka gani nchi hii ya kuweka jina la Nusrat kwenye orodha ya viti maalumu na kuhakikisha wanamtoa mahabusu ili akaapishwe? Hapa ndio ninapowaona ccm either walishatuona watanzania hatuna akili au wao ndio hawana akili. Chadema ina mamlaka gani ya kumtoa mwanachama wake mahabusu ili awahi kuapishwa?

Ushauri wangu kwa chadema. Fungueni kesi mahakamani. Hii kesi ni rahisi sana kushinda. CCM imepanga huu mchezo kiboya sana.

Tunashukuru Nusrat Hanje ametoka mahabusu. Sasa dada wa watu yupo huru.
Wanafungua kesi mahakamani,wakati mahakama ipo chini ya JPM. Hizi sio enzi za Kikwete. JPM alichowafanyia kwenye ubunge majimboni,wanatakiwa akili ziamke. JPM ni Evil in human being body.
 
Utawala wa sheria nchi hii umekoma kwa miaka 5 sasa, ni vyema tukarudi kwenye misingi kama taifa
Sasa hakuna katiba wala Sheria kwani Mwanasheria mkuu wa Serikali sasa ni Mwanasheria binafsi wa CCM siyo watanzania tena, kila kitu ni zidumu fikra zisizo sahihi za mtukufu mwenyekiti wa CCM, wamefunga milango ya kufikiri sasa wanafikiri kwa niaba ya watanzania wote pasipo kujua kuwa watanzania wana Akili nyingi kuliko CCM yote.
 
Hata somo la History tunafundishwa kuwa tulikuwa nyani sasa sijui tunaelekea kuwa nani maana nyani ndio wanakuja kuwa watu
Natafakari sana pale wazungu wanapotuita nyani kama kuna kaukweli fulan hv
 
Wanafungua kesi mahakamani,wakati mahakama ipo chini ya JPM. Hizi sio enzi za Kikwete. JPM alichowafanyia kwenye ubunge majimboni,wanatakiwa akili ziamke. JPM ni Evil in human being body.
Mahakamaccm ni mali binafsi ya CCM ni vigumu chadema ipate haki huko vinginevyo Hakimu au jaji ajitoe mhanga na baada ya kesi hufutwa kazi au kuhamishwa kupelekwa mahakama za vijijini mno
 
Tatizo CCM ni waongo halafu hawana kumbukumbu. Wao walishawahi kumfukuza mbunge Zanzibar kisha akina Sophia Simba na Bernad Membe lakini leo wanaiandama CHADEMA kwa kuwaondoa wahuni
CCM imejaa mapungufu kibao lakini hujidai kuwanyoshea wengine vidole
 
Back
Top Bottom