Saa ishirini na nne za Nusrat Hanje kutia doa Mihimili mitatu ya Nchi

Dogo huwa unakosea sana. Ni wajibu wa serikali kukusanya kodi,je zikikusanywa na kuliwa?

Kuifananisha Tanzania na SA ya makuburu ni kukosa busara. Tumia akili wakati unajitetea.

Sina chembe ya shaka ya nilichosema japo hakikufurahishi. Uadilifu ni jambo tofauti na ujenzi wa majengo. Fungua kamusi ya kiswahili uone maana ya uadilifu, ukikuta mahali wanasema uadilifu ni kujenga majengo, uje tuendelee na mjadala.
 
Sina chembe ya shaka ya nilichosema japo hakikufurahishi. Uadilifu ni jambo tofauti na ujenzi wa majengo. Fungua kamusi ya kiswahili uone maana ya uadilifu, ukikuta mahali wanasema uadilifu ni kujenga majengo, uje tuendelee na mjadala.
Uadilifu ndio unapelekea leo hii hadi kijiji nilipo taa za barabarani zinawaka. Hii ni sababu ubadhilifu na ufisadi umedhibitiwa.
 
huelewi naona

HAKIMU ALITWA NA NDO ALITOA ODA

Hakimu aliitwa kwani ni mke wa DPP? Taratibu za kisheria zinamruhusu DPP kumuita hakimu usiku ili wakashiriki hila za siasa za kipuuzi?
 
Uadilifu ndio unapelekea leo hii hadi kijiji nilipo taa za barabarani zinawaka. Hii ni sababu ubadhilifu na ufisadi umedhibitiwa.

Narudia tena, kama taa barabarani ndio uadilifu, basi makaburu wa Afrika kusini walikuwa na uadilifu wa hali ya juu.
 
Mahakama haina nguvu zaidi ya DPP. DPP anauwezo wa kumfokea hakim na kumpa Amri. Hujiulizi kwanini mahakama inahukum kwa ushabiki na sio kufata sheria? Kama mahakama haiko huru unategemea nani ataiamini ? Ndio maana mtu anapelekwa jela wether mahaka inataka au haitaki na kutolewa hivyohivyo. Punguza presha saivi wanasheria ni kama wapowapo tu.
 
Katiba iko sabbatical leave! Sasa hivi Spika anazo amri za kuwaagiza akina DPP na wengineo bila kuhojiwa na tayari walikwisha jitengenezea kinga ya Kovidi 19.
 
Paragrapha ya 1,2,3,4 umeandika vizuri sana na naekezo yako ni sahihi kabisa. Lakini paragraph 5 nad ya 6 umepotosha kwa kupindisha maneno ya DPP, na mwishowe paragraph za 7,8,9 ni speculative sana kwa sababu hujasema DPP alimtoaje gerezani, unachukulia kuwa DPP alikwenda akawaambia maafisa wa magereza kumtoa bila kujua kuwa huenda aliripoti mahakamani kuwa amefuta kesi hizo na hivyo mahakama ikatoa amri za kuwatoa, lakini amri hizo zikafika hkwa mkuu wa magereza na process ya kuwaachia ikakamilika muda huo waliotolewa. Kuna mmoja wa mahabusu hao amesema kuwa walipata taarifa mapema sana kuwa watatoka siku hiyo kwa hiyo walikuwa wamejiandaa kutoka, hiyo inonyesha kuwa siyo kweli kwamba walikurupushwa na DPP wawatoe wakati huo huo.
 
Mkuu usihangaike na mbumbumbu wa humu JF. Wakisikia kuwa DPP amewaachia mahabusu wanafikiri anaenda yeye in person kuwatoa. Wakati utaratibu ni lazima removal order itolewe na Mahakama, kuna uwezekano removal order imetolewa mapema lakini process ya kuwatoa ndiyo ilichelewa hadi ikafika huo muda wanaousema kama ilivyokuwa kwa kina Mbowe removal order ilitoka mapema lakini walitoka Segerea jioni. Achana na hao wanasaccos uelewa wao ni mdogo sana.
 
Hivi kwanini Mungu ulinifanya nizaliwe kwenye nchi ya Kiboya namna hii ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…