Saa kumi asubuhi nimepishana na katoto kadogo kana begi kubwa mgongoni, hivi shule za namna gani hizi?

Nimeumia sana moyoni!
Unashangaa hayo ndio maisha ya Dar mtoto anaishi mtoto anaishi Goba anasoma Mwenge unafikiri ataamka saaa ngapi? Kuwahi basi ukizingatia anapo ishi mpaka afike kituo cha basi kuna saa 1 bado muda wa kusubilia basi bado konda akita anampakia au anamuacha maisha ya Dar yataka moyo
 
Uongooooo

Uongoooo
 
wengine mazingira yao magumu mfano mtu mwanzo akiishi magomeni kahamia goba kajenga huko lakini mtoto wake bado asoma jangwani mtoto kuamka kwake saa 10 kufika kwenye kituo saa 11 pengine konda anakataa kumpakia mtoto anasota kituoa kila basi likija linamkataa mpaka saa 12 anapada mpaka afike shuleni saa 2 kuludi hivio hivio mvua yake jua lake njaa yake kiu chake maisha ya dar kwa watu wenye kipato kidogo ni shidda sana
 
Jamani!ndio maana serikali inasisitiza vitumike vitabu vinavyochapishwa na Taasisi ya elimu....hizi zitakuwa zile za mtaala wa Cambridge
Hata za cambridge ukikagua hutakuta vitabu vya hivyo. Vitabu vya shule huwa na mihuri, kama ni vitabu vya ziada lazima wazazi walihusika katika ununuzi maana yake tungeona tu
 
Ratiba yatakiwa izingatiwe.

Hapo ni mzazi kuandika kwenye diary kuwa ratiba ifuatwe, muwekee mtoto madaftari husika tu. Akichapwa nenda kapambane nao huko shuleni, wakimfukuza wakurudishie ADA
 
Kuna shida mahali kwenye mindsets za mtu mweusi!!!
Hao waliotuletea hii elimu wanasoma kwa ku relax sana na bado hadi leo hii ni wagunduzi hodari
Sisi tulio ipokea elimu , tunasoma kwa kujitesa sana na hatuvumbui chochote
Wazungu hawana huu ujinga, madaftari na vitabu vingi hubaki shuleni kwenye lockers,
Sisi mzazi anaona sifa mtoto kubebeshwa begi kubwa.

Huko bweni ndo ushoga hufanyika afu twamlaumu Mzungu
 
Kuna dosari kubwa mno katika mtaala mzima wa elimu ya kibongo.

Mfano watoto wa darasa la saba kuambiwa waende shule mpaka jumapili. Siku za kawaida wanawatoa saa 2 usiku. Kuna kipi cha mno wanachosomeshwa sasa hivi ambacho sisi miaka ya 90 hatukukisoma??

Hapo hapo mtoto anabebeshwa rundo la mitabu kama vile anasomea masters ya udaktari.
 
Unakuta mzazi anakuambia hataki mwanae asome boarding halafu kakwake anakaamsha saa 9 usiku kajiandae kwenda shule.
Huyo ni mpumbavu sana,
Mtoto asome karibu na nyumbani.

Mikoa yote shule ziko kila sehemu tena karibu na nyumbani.
 
Ila huwa ni makubaliano ya wazazi na walimu maana wanataka wakajisifu wamepata A
 
Ila huwa ni makubaliano ya wazazi na walimu maana wanataka wakajisifu wamepata A
Sio makubaliano. Naongelea kwa experience. Walipojulisha wazazi haikuwa na mjadala, ilikuwa ni taarifa.
Unaambiwa si moja kwa moja ila kwa kuashiria kuwa ukitaka mlete mwanao hutaki acha.
Sifa zao zinaathiri watoto kwa kiasi kikubwa.
Inafikia wakati mzazi na mtoto hamuonani kabisa. Ukiuliza elimu ya darasa la 7.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…