Saa kumi asubuhi nimepishana na katoto kadogo kana begi kubwa mgongoni, hivi shule za namna gani hizi?

Saa kumi asubuhi nimepishana na katoto kadogo kana begi kubwa mgongoni, hivi shule za namna gani hizi?

Nimeumia sana moyoni!
Unashangaa hayo ndio maisha ya Dar mtoto anaishi mtoto anaishi Goba anasoma Mwenge unafikiri ataamka saaa ngapi? Kuwahi basi ukizingatia anapo ishi mpaka afike kituo cha basi kuna saa 1 bado muda wa kusubilia basi bado konda akita anampakia au anamuacha maisha ya Dar yataka moyo
 
Leo nimshuka kutoka basi la mkoani mida ya around saa9 usiku hapa stand ya magu.
Kupanda daladala ya gomz mida hiyo nashangaa kunakatoto kashule moyoni nikajiuliza shule mida hii nani atamfungulia.
Hilo nimoja ya gap watu wenye nia mbaya wanaweza kutumia.
#EeBabaMunguTulindieWatotoWetu
Uongooooo

Uongoooo
 
Ni ujinga na ulimbukeni wa elimu na asilimia kubwa ya wazazi wanaofanya hivyo ni wale ambao hawajaenda shule ila mungu kawabariki kipato aisee hili kundi linatesa watoto mtoto darasa la pili apumziki kama hivyo kamamka sasa tisa anaenda shule kurudi nyumbani sasa tatu usiku maana..akitoka.shule anaenda tution Yani elimu inakuwa Kama utumwa
wengine mazingira yao magumu mfano mtu mwanzo akiishi magomeni kahamia goba kajenga huko lakini mtoto wake bado asoma jangwani mtoto kuamka kwake saa 10 kufika kwenye kituo saa 11 pengine konda anakataa kumpakia mtoto anasota kituoa kila basi likija linamkataa mpaka saa 12 anapada mpaka afike shuleni saa 2 kuludi hivio hivio mvua yake jua lake njaa yake kiu chake maisha ya dar kwa watu wenye kipato kidogo ni shidda sana
 
Jamani!ndio maana serikali inasisitiza vitumike vitabu vinavyochapishwa na Taasisi ya elimu....hizi zitakuwa zile za mtaala wa Cambridge
Hata za cambridge ukikagua hutakuta vitabu vya hivyo. Vitabu vya shule huwa na mihuri, kama ni vitabu vya ziada lazima wazazi walihusika katika ununuzi maana yake tungeona tu
 
Ukitaka kuelewa ni jinsi gani hii SYNDROME ya kufaulisha kwa MAUMIVU YOYOTE YAWAYO kwa mtoto ilivyobebwa na wazazi vs walimu.

1: Jaribu kulieleza hilo siku ya kikao cha wazazi na walimu.

2: Eleza kwenye grupu la usafiri la watoto wa shule

Utaonekana wewe ni mpinga elimu na ufaulu wa watoto.
Ni ulemavu tumeshatwishwa wazazi na wizara iko kimwa.

Pia, watoto wanatembea na mabegi utafikiri wanajifunza kuwa makuli. Mwishowe ni kesi za kutibu migongo ya vijana wadogo kuongezeka.

Vijana wanafikia kuona shule kama adhabu na hatujui ni kwa kiadi gani tunawaumiza ubongo na kutengeneza magonjwa ya afya ya akili vs mengine physical.
Ratiba yatakiwa izingatiwe.

Hapo ni mzazi kuandika kwenye diary kuwa ratiba ifuatwe, muwekee mtoto madaftari husika tu. Akichapwa nenda kapambane nao huko shuleni, wakimfukuza wakurudishie ADA
 
Kuna shida mahali kwenye mindsets za mtu mweusi!!!
Hao waliotuletea hii elimu wanasoma kwa ku relax sana na bado hadi leo hii ni wagunduzi hodari
Sisi tulio ipokea elimu , tunasoma kwa kujitesa sana na hatuvumbui chochote
Wazungu hawana huu ujinga, madaftari na vitabu vingi hubaki shuleni kwenye lockers,
Sisi mzazi anaona sifa mtoto kubebeshwa begi kubwa.

Huko bweni ndo ushoga hufanyika afu twamlaumu Mzungu
 
Kuna dosari kubwa mno katika mtaala mzima wa elimu ya kibongo.

Mfano watoto wa darasa la saba kuambiwa waende shule mpaka jumapili. Siku za kawaida wanawatoa saa 2 usiku. Kuna kipi cha mno wanachosomeshwa sasa hivi ambacho sisi miaka ya 90 hatukukisoma??

Hapo hapo mtoto anabebeshwa rundo la mitabu kama vile anasomea masters ya udaktari.
 
Unakuta mzazi anakuambia hataki mwanae asome boarding halafu kakwake anakaamsha saa 9 usiku kajiandae kwenda shule.
Huyo ni mpumbavu sana,
Mtoto asome karibu na nyumbani.

Mikoa yote shule ziko kila sehemu tena karibu na nyumbani.
 
Kuna dosari kubwa mno katika mtaala mzima wa elimu ya kibongo.

Mfano watoto wa darasa la saba kuambiwa waende shule mpaka jumapili. Siku za kawaida wanawatoa saa 2 usiku. Kuna kipi cha mno wanachosomeshwa sasa hivi ambacho sisi miaka ya 90 hatukukisoma??

Hapo hapo mtoto anabebeshwa rundo la mitabu kama vile anasomea masters ya udaktari.
Ila huwa ni makubaliano ya wazazi na walimu maana wanataka wakajisifu wamepata A
 
Ila huwa ni makubaliano ya wazazi na walimu maana wanataka wakajisifu wamepata A
Sio makubaliano. Naongelea kwa experience. Walipojulisha wazazi haikuwa na mjadala, ilikuwa ni taarifa.
Unaambiwa si moja kwa moja ila kwa kuashiria kuwa ukitaka mlete mwanao hutaki acha.
Sifa zao zinaathiri watoto kwa kiasi kikubwa.
Inafikia wakati mzazi na mtoto hamuonani kabisa. Ukiuliza elimu ya darasa la 7.
 
Back
Top Bottom